popiexo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 742
- 182
Ndugu zangu wa TZ tukiwa bado tunasubiri ndoto za mchana za JK kutimia hebu tukumbushane ndoto hizo na sehemu alikoziotea
Je hakuna hatua za dharura tunazoweza kuchukua?
- Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
- Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
- Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
- Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
- Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
- Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
- Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
- Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
- Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
- Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
- Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
- Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
- Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
- Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
- Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
- Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
- Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
- Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
- Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
- Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
- Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
- Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
- Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
- Kujenga bandari Kasanga Rukwa
- Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
- Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
- Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
- Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
- Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
- Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
- Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
- Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
- Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
- Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
- Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
- Kulinda haki za walemavu - Makete
- Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
- Kujenga barabara Musoma Mto wa Mbu Arusha - Arusha
- Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
- Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma Kaliua,Tabora
- Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
- Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
- Kuwafidia wanakijiji ngombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
- Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
- Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha Arusha mjini
- Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
- Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
- Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti Ngorongoro
- Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
- Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
- Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
- Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
- Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
- Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
- Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
- Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
- Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
- Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
- Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
- Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
- Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
- Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
- kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) Ruvuma
- Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania Ruvuma
- Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
- Mtwara kuwa mji wa Viwanda Mtwara
- Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
- Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
- Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
Je hakuna hatua za dharura tunazoweza kuchukua?