Tuwe wakweli, ziara ya Rais Magufuli mikoa ya Iringa na Morogoro ilijaa kauli za kibaguzi na utengano wa kitaifa

Inamaana Magufuli kamuogopa diwani wa chadema pale Mkula kaenda kukaa na Lijuakali wa kilombero, Suzan Kiwanga na Pr J,
mbona pointless tu hapo
Ndo maana kuna bi mkubwa mwanzoni kasema "mgazeti mreeeeefu"
 
Ahsante sana mleta mada. Umeongea ukweli mtupu. Rais aache ubaguzi na chuki! Utadhani siyo baba wa wote. Je rais siyo baba wa wote?
 
Inamaana Magufuli kamuogopa diwani wa chadema pale Mkula kaenda kukaa na Lijuakali wa kilombero, Suzan Kiwanga na Pr J,
mbona pointless tu hapo
Ndo maana kuna bi mkubwa mwanzoni kasema "mgazeti mreeeeefu"
Usi cherry pick mzeeiya. Ujumbe mpana hapo siyo suala la huyo diwani. Bali ni kujirudiarudia kwa kauli za, na matendo ya kibaguzi ya Rais Magufuli.
 
rwanda na burundi ndyo wenye hulka hzo za ubaguzi wa ukabila ukija kwetu huku utakuwa mbaya sna.
 
Ziara ya Rais katika mikoa ya Iringa na Morogoro,ni wazi imeendelea kumfungua Rais machoni pa watu wenye jicho lililokuwa na unafiki kuhusu msimamo wake juu ya Watanzania na umoja wa kitaifa.

Ziara hii iliyoambatana na hotuba nyingi za hapa na pale,zinaendelea kufungua nafasi ya wananchi kumuelewa Rais wao kupitia matamshi yake na hotuba zake.Ndani ya hotuba za Rais unaweza kuona dhamira yake haswa ni nini,sababu kwa wajuzi wa hisia/mawazo, hupata dhamira ya mtu kupitia matamshi yake.

Hotuba za Rais zinaonyesha kuwa bado uongozi wetu katika nchi unahitaji mfumo mpya,utakaoongozwa na sheria mpya na mabadiliko makubwa ya kikatiba na kimfumo.Yaani licha ya "ukali" na "utumbuaji" wa watendaji wa serikali,bado huko ngazi za chini kuna uozo mtupu.

Uozo huu unatokana na kuwa na "One Man Show",mtu hatendi kwasababu anaogopa sheria,bali anamuogopa mtu mmoja ambaye yupo Dsm na anaweza amalize miaka mitano bila kufika eneo lake la kiutendaji na kujua kero za wananchi,lakini kama kungekuwa na sheria pamoja na katiba imara,itakayoimarisha mifumo ya kiutendaji,basi hata watendaji wadogo wangeendana na "dhamira" ya Rais katika kufikia maendeleo ya pamoja.

Hotuba nyingi za Rais ni malalamiko tu,kila jambo au tatizo la kimaendeleo linamsubiri Rais aliye Ikulu ya Dsm,na ni ukweli kuwa Rais mwenyewe kuna maeneo hayajui kwa sababu ya ukubwa wa kijiografia wa nchi.Huko Kilolo wana matatizo yanayomsubiri Rais ambaye kabla hajafika Ikulu,anakutana na matatizo ya Mlimba na Ifakara,akiwa na matatizo ya Mlimba na Ifakara kichwani,Rais anakutana na mgogoro wa ardhi ambao umewashinda wasaidizi wake katika vijiji vya Melela.

Hawa wananchi wa Mlimba wanazalisha karibu nusu ya mchele unaoliwa Tanzania Mashariki na kati,wanachangia katika pato la Taifa kwa kilimo,lakini mapato hayo yanaenda kujenga uwanja wa ndege sehemu nyingine na wao wanatembea kwenye barabara ya vumbi kila mwaka,kwenye safari ya masaa manne kufika makao makuu ya Wilaya Ifakara,wao wanatumia siku mbili.Huu ni mgawanyo wa hovyo sana wa rasilimali za nchi unaosababishwa na mifumo mibovu ya uendeshaji wa nchi.

Jambo jingine liliibuka kwenye ziara hii ya Rais,ni muendelezo wa lugha za kutugawa na kutengeneza mpasuko wa Kitaifa.Kauli hizi zinatoka kwa Rais mwenyewe,ambaye ni kiongozi wa nchi na "Chief Councellor".

Ni ukweli kuwa Rais amekuwa anahubiri kila mahali kuwa uchaguzi umekwisha,sasa ni maendeleo tu hakuna uvyama wala siasa,na kwamba maendeleo hayana chama

Lakini yeye kama kiongozi,kwa kujua au kutokujua amekuwa anaendelea kuhutubia kauli za kiubaguzi na kugawanya Taifa.

Akiwa Iringa,ama kwa kujua au kutokujua,Rais amesikika akitamka hadharani kuwa kwa sasa hatapeleka maendeleo Kaskazini mwa Tanzania,maendeleo atayapeleka sehemu nyingine za Tanzania,na hata sekta ya utalii anataka iimarike mkoa wa Iringa kama kitovu cha utalii wa nyanda za juu kusini.Na akasisitiza kuwa "Kaskazini kwa sasa wasubirie kwanza kuhusu maendeleo"

Kauli hii haikupaswa kutoka kwa Raia namba moja,ambaye watu wote walimpigia kura.Hata kama alikuwa na lengo la kuweka msisitizo kuwa anataka kuzindua "Southern Highland Circuit Tourism",hakuwa na haja ya kusema hawezi kupeleka maendeleo Kaskazini.Unaligawanya Taifa,unapandikiza chuki,unapanda mbegu ya utengano,tafuta maneno mazuri ya kuelezea unapoongea na Taifa.

Maeneo alimopita na kukuta uongozi wa vyama vya upinzani,Rais alitoa kauli za kibaguzi sana.Hii linapaswa kusemwa tu,maana yeye sio malaika,ni mavumbi na ipo siku mavumbini atarudi kama sisi wengine.

Uzinduzi wa barabara ya Migori-Fufu,ulipaswa kufanyika katika kijiji cha Migori katika kata ya Migori,lakini sababu kata hiyo inaongozwa na diwani wa CHADEMA na mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA basi uzinduzi ukahamishwa ukapelekwa mbele katika kijiji cha Kihorogota.

Kule Morogoro,uzinduzi wa daraja pamoja na ujenzi wa barabara ulifanyika ktk jimbo la Kilombero na majimbo jirani kama Mikumi,Mlimba na Ulanga yalihusika.Huku kote Rais akihutubia,anahutubia kwa kauli za mgawanyiko tu wa kisiasa.Huyu ni mtu anayeamini anaweza kukubalika na kila mtu duniani.

Alipokuwa kijiji cha Mkula katika kata ya Mang'ula,ambapo eneo hili linaongozwa na wenyekiti wengi wa vijiji wa upinzani na madiwani wa upinzani,Rais ameonekana kuhubiri kauli za mgawanyiko katika Taifa.

Wakati Mwanza Rais alitamka kuwa wananchi wasihamishwe wala kubomolewa mpaka wafikie muafaka sababu wao ndio waliompigia kura,huko Kilombelo Rais anasema huo mgogoro wa wananchi haumuhusu,na kwamba yeye kama Rais hajaja kutatua mgogoro wa ardhi bali kufungua daraja.Hizi ni kauli za Rais mmoja,ambaye huku anasema wananchi wasibomolewe,lakini huku hataki kusikia anashirikishwa katika kusaidia wananchi wasibomolewe.

Rais anakosa "Political Tolerance" ambayo anaitamka bila kuitenda.Hoja ya matatizo ya wananchi ikitokewa na mbunge wa upande wa pili,anaibuka anasema "we si umechaguliwa na wananchi,ulisubiri mie ndio nije?Jamani wananchi si mnaona watu mnaochagua?",lakini hoja ikiletwa na mbunge wa chama chake,ya aina ileile,anaibuka na kusema mliniletea jembe kwelikweli.Hizi ni kauli za mtu anayehubiri kile asichokitenda.

Inatakiwa huyu mtu akumbushwe kuliunganisha Taifa,asiwe anatembea na kauli za kihoro cha uchaguzi wa 2015.Kila mahali analazimisha kutoa pesa na kila anapotoa,kama ni kata au kijiji cha upinzani,basi atamuita hata mwenyekiti wa kitongoji wa CCM aje apokee hizo pesa pamoja na wa upinzani,lakini penye diwani wa CCM atampa peke yake na majigambo kuwa pesa n ya CCM wakati ni makato ya kodi ya Watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Maana dhana ya kodi,ni pesa inayotoka kwa wananchi,inayomlisha Rais na familia yake na wasaidizi wake.Haitolewi kama hisani,bali ni haki na stahiki ya mwananchi katika kile anachochangia kwenye kulijenga Taifa lake toka katika kipato chake cha kila siku kinachobebwa na serikali kwa jina la kodi.Hizi ni kodi za wananchi wote,toka muuza vitumbua kwenye mtaa wa masempele pale Tabora,mpaka muuza mbao wa Mufindi na msafirishaji wa magari toka Japan kuja Tanzania.
Wewe bwana anza kwa kutoa declaration of interest kuwa mlipeleka maendeleo sehemu moja kwingine kukasahaulika. Inakuuma kujikuta walioachwa nyuma sasa nao wamepata mtetezi.
 
Ni taaluma iliyojaa frustrated staff kwa sababu wengi wao walishindwa kutimiza taaluma ya ndito zao aidha baada ya kufeli form four au six. Ualimu ikawa taaluma pekee ya kukimbilia katikati ya frustrations hizo. Mwisho wa hayo ni ukatili wa ajabu na robo mbaya.

I guess you are right. Ni waalimu wachache sana ambao wako kwenye hiyo taaluma kwa kupenda. Wengi wamelazimika kuwa huko baada ya plan A au hata B kushindwa so wanajikuta wanadondokea huko kwenye plan C ualimu. Hata jiwe alisoma degree kwa mature entry. Ni kama polisi nao ni hivyo hivyo wengi hawakuwa na wito wa kuwa mapolisi wamelazimika kuwa hivyo. So ni ma-frustrations mwanzo mwisho usipokuwa makini wanaweza kukuambukiza, tuwe makini na namna ya kudeal nao.

Bahati mbaya simfahamu mshauri wa kiroho wa rahisi ila ana kazi kubwa sana ya kuomba, kufundisha biblia kdg japo mistari michache na maana yake, counselling etc kwani ninavyoona kiukweli kbs hali si shwari yatupata kwa pamoja kuchukua hatua.
 
Ziara ya Rais katika mikoa ya Iringa na Morogoro,ni wazi imeendelea kumfungua Rais machoni pa watu wenye jicho lililokuwa na unafiki kuhusu msimamo wake juu ya Watanzania na umoja wa kitaifa.

Ziara hii iliyoambatana na hotuba nyingi za hapa na pale,zinaendelea kufungua nafasi ya wananchi kumuelewa Rais wao kupitia matamshi yake na hotuba zake.Ndani ya hotuba za Rais unaweza kuona dhamira yake haswa ni nini,sababu kwa wajuzi wa hisia/mawazo, hupata dhamira ya mtu kupitia matamshi yake.

Hotuba za Rais zinaonyesha kuwa bado uongozi wetu katika nchi unahitaji mfumo mpya,utakaoongozwa na sheria mpya na mabadiliko makubwa ya kikatiba na kimfumo.Yaani licha ya "ukali" na "utumbuaji" wa watendaji wa serikali,bado huko ngazi za chini kuna uozo mtupu.

Uozo huu unatokana na kuwa na "One Man Show",mtu hatendi kwasababu anaogopa sheria,bali anamuogopa mtu mmoja ambaye yupo Dsm na anaweza amalize miaka mitano bila kufika eneo lake la kiutendaji na kujua kero za wananchi,lakini kama kungekuwa na sheria pamoja na katiba imara,itakayoimarisha mifumo ya kiutendaji,basi hata watendaji wadogo wangeendana na "dhamira" ya Rais katika kufikia maendeleo ya pamoja.

Hotuba nyingi za Rais ni malalamiko tu,kila jambo au tatizo la kimaendeleo linamsubiri Rais aliye Ikulu ya Dsm,na ni ukweli kuwa Rais mwenyewe kuna maeneo hayajui kwa sababu ya ukubwa wa kijiografia wa nchi.Huko Kilolo wana matatizo yanayomsubiri Rais ambaye kabla hajafika Ikulu,anakutana na matatizo ya Mlimba na Ifakara,akiwa na matatizo ya Mlimba na Ifakara kichwani,Rais anakutana na mgogoro wa ardhi ambao umewashinda wasaidizi wake katika vijiji vya Melela.

Hawa wananchi wa Mlimba wanazalisha karibu nusu ya mchele unaoliwa Tanzania Mashariki na kati,wanachangia katika pato la Taifa kwa kilimo,lakini mapato hayo yanaenda kujenga uwanja wa ndege sehemu nyingine na wao wanatembea kwenye barabara ya vumbi kila mwaka,kwenye safari ya masaa manne kufika makao makuu ya Wilaya Ifakara,wao wanatumia siku mbili.Huu ni mgawanyo wa hovyo sana wa rasilimali za nchi unaosababishwa na mifumo mibovu ya uendeshaji wa nchi.

Jambo jingine liliibuka kwenye ziara hii ya Rais,ni muendelezo wa lugha za kutugawa na kutengeneza mpasuko wa Kitaifa.Kauli hizi zinatoka kwa Rais mwenyewe,ambaye ni kiongozi wa nchi na "Chief Councellor".

Ni ukweli kuwa Rais amekuwa anahubiri kila mahali kuwa uchaguzi umekwisha,sasa ni maendeleo tu hakuna uvyama wala siasa,na kwamba maendeleo hayana chama

Lakini yeye kama kiongozi,kwa kujua au kutokujua amekuwa anaendelea kuhutubia kauli za kiubaguzi na kugawanya Taifa.

Akiwa Iringa,ama kwa kujua au kutokujua,Rais amesikika akitamka hadharani kuwa kwa sasa hatapeleka maendeleo Kaskazini mwa Tanzania,maendeleo atayapeleka sehemu nyingine za Tanzania,na hata sekta ya utalii anataka iimarike mkoa wa Iringa kama kitovu cha utalii wa nyanda za juu kusini.Na akasisitiza kuwa "Kaskazini kwa sasa wasubirie kwanza kuhusu maendeleo"

Kauli hii haikupaswa kutoka kwa Raia namba moja,ambaye watu wote walimpigia kura.Hata kama alikuwa na lengo la kuweka msisitizo kuwa anataka kuzindua "Southern Highland Circuit Tourism",hakuwa na haja ya kusema hawezi kupeleka maendeleo Kaskazini.Unaligawanya Taifa,unapandikiza chuki,unapanda mbegu ya utengano,tafuta maneno mazuri ya kuelezea unapoongea na Taifa.

Maeneo alimopita na kukuta uongozi wa vyama vya upinzani,Rais alitoa kauli za kibaguzi sana.Hii linapaswa kusemwa tu,maana yeye sio malaika,ni mavumbi na ipo siku mavumbini atarudi kama sisi wengine.

Uzinduzi wa barabara ya Migori-Fufu,ulipaswa kufanyika katika kijiji cha Migori katika kata ya Migori,lakini sababu kata hiyo inaongozwa na diwani wa CHADEMA na mwenyekiti wa Kijiji wa CHADEMA basi uzinduzi ukahamishwa ukapelekwa mbele katika kijiji cha Kihorogota.

Kule Morogoro,uzinduzi wa daraja pamoja na ujenzi wa barabara ulifanyika ktk jimbo la Kilombero na majimbo jirani kama Mikumi,Mlimba na Ulanga yalihusika.Huku kote Rais akihutubia,anahutubia kwa kauli za mgawanyiko tu wa kisiasa.Huyu ni mtu anayeamini anaweza kukubalika na kila mtu duniani.

Alipokuwa kijiji cha Mkula katika kata ya Mang'ula,ambapo eneo hili linaongozwa na wenyekiti wengi wa vijiji wa upinzani na madiwani wa upinzani,Rais ameonekana kuhubiri kauli za mgawanyiko katika Taifa.

Wakati Mwanza Rais alitamka kuwa wananchi wasihamishwe wala kubomolewa mpaka wafikie muafaka sababu wao ndio waliompigia kura,huko Kilombelo Rais anasema huo mgogoro wa wananchi haumuhusu,na kwamba yeye kama Rais hajaja kutatua mgogoro wa ardhi bali kufungua daraja.Hizi ni kauli za Rais mmoja,ambaye huku anasema wananchi wasibomolewe,lakini huku hataki kusikia anashirikishwa katika kusaidia wananchi wasibomolewe.

Rais anakosa "Political Tolerance" ambayo anaitamka bila kuitenda.Hoja ya matatizo ya wananchi ikitokewa na mbunge wa upande wa pili,anaibuka anasema "we si umechaguliwa na wananchi,ulisubiri mie ndio nije?Jamani wananchi si mnaona watu mnaochagua?",lakini hoja ikiletwa na mbunge wa chama chake,ya aina ileile,anaibuka na kusema mliniletea jembe kwelikweli.Hizi ni kauli za mtu anayehubiri kile asichokitenda.

Inatakiwa huyu mtu akumbushwe kuliunganisha Taifa,asiwe anatembea na kauli za kihoro cha uchaguzi wa 2015.Kila mahali analazimisha kutoa pesa na kila anapotoa,kama ni kata au kijiji cha upinzani,basi atamuita hata mwenyekiti wa kitongoji wa CCM aje apokee hizo pesa pamoja na wa upinzani,lakini penye diwani wa CCM atampa peke yake na majigambo kuwa pesa n ya CCM wakati ni makato ya kodi ya Watanzania wote bila kujali vyama vyao.

Maana dhana ya kodi,ni pesa inayotoka kwa wananchi,inayomlisha Rais na familia yake na wasaidizi wake.Haitolewi kama hisani,bali ni haki na stahiki ya mwananchi katika kile anachochangia kwenye kulijenga Taifa lake toka katika kipato chake cha kila siku kinachobebwa na serikali kwa jina la kodi.Hizi ni kodi za wananchi wote,toka muuza vitumbua kwenye mtaa wa masempele pale Tabora,mpaka muuza mbao wa Mufindi na msafirishaji wa magari toka Japan kuja Tanzania.
Well said!
 
Back
Top Bottom