Tuwe wakweli, zaidi ya Mbowe nani ana uwezo wa kuiongoza CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,507
141,233
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Mbowe ndiye kiongozi pekee mwenye uwezo wa kuivusha Chadema uchaguzi wa 2020.

Awali niliamini kuwa Tundu Lisu ataweza kuvaa viatu vya Lisu lakini baada ya kumshuhudia akiingia katika 18 za Zitto Kabwe kuaminika kwake kunaleta mashaka.

Demokrasia haikatazi mtu mmoja kuongoza kwa muda mrefu ili mradi tu awe anakubalika kwa anaowaongoza.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hilo swali linawaiza sana bavicha.
Chadema ni kama chama cha kifamilia. We fikiria wanamtegemea Mbowe pekee,
 
M
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Mbowe ndiye kiongozi pekee mwenye uwezo wa kuivusha Chadema uchaguzi wa 2020.

Awali niliamini kuwa Tundu Lisu ataweza kuvaa viatu vya Lisu lakini baada ya kumshuhudia akiingia katika 18 za Zitto Kabwe kuaminika kwake kunaleta mashaka.

Demokrasia haikatazi mtu mmoja kuongoza kwa muda mrefu ili mradi tu awe anakubalika kwa anaowaongoza.

Maendeleo hayana vyama!
Mawazo mfu kama nihivyo basi akifa anazikwa nachadema inazikwa unatuletea mambo yanchi Jirani nakule ambapo mazishi yanaendelea watapita nchi navyama japo vinaweza kubadilika majina lakini vitakuwepo
 
Watu Wana leta propaganda. Lakini kikweli Mbowe is the Real Deal.... At least for.now.

Mbowe hana mvuto wa kuwa mgombea wa Urais lakini ndiye pekee kwa sasa anayeweza kuwaweka CDM na UKAWA pamoja.
 
Kuivusha? Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola siyo kuvuka uchaguzi.

Hata Jahazi Asilia itavuka uchaguzi wa 2020 na haiongozwi na Mbowe!
Siyo kila chama cha siasa kina lengo la kushika dola......usikariri mkuu.

TLP ya Lyatonga Mrema kwa mfano haina lengo hilo!
 
Mkitoka hapo mnamsema Mugabe kwa kung’ang’ania madaraka na kutoandaa Mrithi wake

Chadema ni kama kikundi cha Wachekeshaji tu
Kuna tofauti ya kung'ang'ania na kung'ang'anizwa usisahau hilo.

Manji wa Yanga kwa mfano alikuwa anang'ang'anizwa kuendelea kuwa Rais japo muda wake uliisha!
 
Siyo kila chama cha siasa kina lengo la kushika dola......usikariri mkuu.

TLP ya Lyatonga Mrema kwa mfano haina lengo hilo!
Kwa hiyo CDM nayo kwa sasa lengo lao ni kuvuka uchaguzi kama TLP?

TLP ipo hapo kwa sababu hizo hizo unazozipigia chepuo.
 
M

Mawazo mfu kama nihivyo basi akifa anazikwa nachadema inazikwa unatuletea mambo yanchi Jirani nakule ambapo mazishi yanaendelea watapita nchi navyama japo vinaweza kubadilika majina lakini vitakuwepo
Umeambiwa " kwa sasa".......uwe unaelewa!
 
Back
Top Bottom