Tuwe wakweli: Wabunge wa Zanzibar wanawawakilisha nani bungeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe wakweli: Wabunge wa Zanzibar wanawawakilisha nani bungeni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngekewa, Apr 14, 2011.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jamani nakwazwa na mawazo kila siku kujaribu kuona logic ya mfumo huu wa Bunge wa kuwashirikisha Wabunge wa Zanzibar. Huwa najiuliza wanawawakilisha nani hasa? Naomba jamvi linipe elimu juu ya hili.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni sehemu ya JMT hivyo nako kuna majimbo ya uchaguzi kama bara.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ngekewa,
  Mkuu wangu kusema kweli siasa za Bongo zinachekesha sana..Na hakika hili sio swali jepesi kama tunavyofikiria.

  Katika maswala ya Muungano hawa wabunge hawatambuliki Zanzibar isipokuwa Bunge la Zanzibar ndilo lenye nguvu ktk maamuzi mengi yenye maslahi ya Zanzibar..Mfano mkubwa ni huo Muswada wa katiba mpya wanataka ufikishwe bunge la Zanzibar kwanza, hali wanao wabunge wawakilishi ndani ya Bunge la Muungano.. Kutolipeleka zanzibar wanadai kwamba wanatengwa, sasa sijui hao waliopo Bunge la Muungano wanawakilisha kina nani!

  Haya ukitazama ktk ndoa ya CUF na CCM, ni hawa Wabunge wa CUF Zanzbar waliopinga kumpa kura zao mgombea wa Chadema ktk kiti cha Uspika kwa maagizo toka Zanzibar, lakini waulize CUF watakwambia muafaka uliopo baina ya CCM na CUF unahusu Visiwani tu na wapo tayari kushirikiana na Chadema hali kura zao zinakwenda CCM kwa maagizo kutoka Zanzibar..

  Kifupi ni hivi Wazanzibar wameamua kutazama maslahi ya Zanzibar kwanza, hilo ni jambo jema na ndivyo inavyotakiwa..lakini kwa makosa kama ya Waislaam, mimi hujiuliza ni toka lini CCM au Utawala wa bara ukawa marafiki zao?.. something is very wrong na siasa za tanzania maanake sielewi kabisa huu Uadui wa CUF Na Chadema umetoka wapi baada ya kuwa pamoja toka mwaka 2000 ghafla, muafaka umekufa na CUF ni marafiki na CCM bara na visiwani..
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mswada huu ndugu yangu si Mswada kama Miswada mengine ambayo hujadiliwa na kupitishwa Bungeni.

  Mswada huu unahusu Muungano wa nchi mbili zilizoungana ingawa tulieungana nae hayupo.

  Kinachozungumzwa ni utaratibu ambao haukufutwa kutokana na dharau za kawaida tu.

  Hata hivyo, tukio hili limetusaidia sana kwani kabla ya hizo taratibu za kukusanya maoni kuanza, Wazanzibari wameshapeleka ujume kuwa "uvamizi" huu ambao nyinyi mnauita Muungano, hatuutaki.

  Hayo mambo ya udini na u CUF na u CCM hapa si pahala pake, anzisha thread yake.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu mbona munkari umepanda?.
  Naa ajabu, kwani huo Muswada hapa ni mahala pake?
  Na iweje katiba inayohusu Muungano usioupenda iwe issue kwako hali huutaki Muungano, hiyo katiba mpya ya nini kwako tena!...Na mnafanya nini bungeni haswa ikiwa mnataka kuitenga..
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hiki ni kizungumkuti ambacho umefika wakati sasa kukiondowa sawa na misururu ya mambo yasiyoleta tija yoyote kwa pande zote mbili. Kwa upande mmoja mfumo huu si chengine bali ni changa la macho kwa Wazanzibari wahisi wako kwenye Muungano wakati ukweli wenyewe ni kuwa wako katika kutawaliwa. Upande wa pili ni upotevu wa pesa usio na maana yoyote badala ya kutumia pesa hizo kwa manufaa ya wananchi wote zinatumika ili kucheza mchezo wa kisiasa.


  Nilikuwa nkishangaa kwanini mbali yakejeli na masimango wanayopata Wazanzibari kwa suwala la matumizi na michango, bado hakuna Mtanganyika yeyote anaelipigia kelele hili. Jawabu nilioipata ni kuwa Watanganyika wanaelewa kafara hii lakini wanajuwa kuwa hii ndio shikizo la kuikamata Zanzibar.

  Si wapinzani si Chama tawala ambao wako tayari kulizungumzia hili na hata watu binafsi watakejeli na kutusi lakini kwenye ukweli huu hawafiki. Ndugu zetu wa Tanganyika mnatupenda Wazanzibari tuendelee kuwa mikononi mwenu na hili ni kwa umoja wenu viongozi na wananchi.

  Nimejaribu kuangalia mantiki ya kuwa Bunge linazungumzia mambo ya Tanganyika lakini Wazanzibari wanakuwa sehemu ya Bunge. Nimekuwa nikiangalia mantiki ya wajibu wa wabunge ikiwa ni kuwatetea wananchi kwa maslaha yao lakini Bunge letu linatetea maslaha ya Watanganyika peke yao! Nimekuwa nikiangalia nini kazi ya Mbunge ambayo ni kumwakilisha mwananchi na kujiuliza iwapo hakuna kinachomuhusu Mzanzibari anawakilishwa kwa maana gani? Nimekuwa nikjiuliza Mbungee kutoka Zanzibar anapokuwa kwenye kamati fulani za mambo yanayoshughulikia Tanganyika anakuwepo kama mtaalamu au kama mwananchi wa Tanganyika? Msururu wa kujiuliza ni mrefu na sipati jibu! Pengine waliona busara zaidi wanifafanulie!
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu.

  Zanzibar unaweza kusema ni sehemu ya JMT, lakini kwa usahihi ni kusema Zanzibar ni mbia katika JMT.

  Mkuu. Kwa sisi kuukataa ukweli huu haijatusaidia wala haitatusaidia.
  Mkuu pia hii inayoitwa "bara" ni upotoshaji...lini jina Tanganyika liligeuka "bara".

  Pitia huu muswada wa kukusanya maoni ya "katiba mpya"... imeandikwa Tanzania bara na Tanzania Zanzibar....kwa nini isiwe Tanzania Tanganyika na Tanzania Zanzibar?

  Mkuu, naelewa msimamo wako kuhusu Tanganyika lakini Tanzania au Tanzania bara au bara si mbadala wa jina Tanganyika.

  Sehemu, ardhi iliyokuwa inaitwa Tanganyika haijahama ipo pale pale kama ilivyo sehemu,ardhi ya Zanzibar.

  Huu usanii tuuache...sio rahisi kuufuta utaifa wa watu popote duniani. Na katika hali za leo,watu wanaweza kuwa na uraia zaidi ya mmoja.

  Rev. Mtikila anatukumbusha kila siku kuhusu nchi yetu ya asili.

  Pia pitia hii doc uone serikali ya Muungano inafanya pia kazi za serikali ya sehemu ipi?
  and for the exclusive authority of the said Parliament and
  Executive in such matters throughout and for the United Republic
  and in all other matters in and for Tanganyika;

  8.-(1) Subject to the provisions of this section, on and after Union
  Day the existing law of Tanganyika and of Zanzibar shall continue
  to be the law in the territories of Tanganyika and of Zanzibar respectively,

  Articles.znz+Tngk[1]

  Hata hivyo nakubaliana na wewe kuwa Zanzibar kuna majimbo ya uchaguzi wa wabunge ambao wataiwakilisha Zanzibar katika bunge la Muungano.
  Lakini kwa msimamo wangu wabunge hawa hapaswi kushiriki mijadala Bungeni yanapojadiliwa mambo yasiyo ya Muungano. In fact bunge la Muungano lingekuwa dogo tu kwa kuiga model ya bunge la EAC.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu usiwalaumu Bara bure ktk mfumo dume wa Kiutawala. Labda wewe hufahamu kwamba Zanzibar wanahusika sana ktk muundo wa bunge la muunganoambapo viongozi wa chama CCM bara na visiwani wamefikiria tu nafasi zao ktk Ulaji na sii kuwawakilisha wananchi..

  Na ndio maana hatuna nchi inayojulikana kama bara ili mradi Zanzibar kama nchi ndogo isimezwe na kunyimwa nafasi hizi bungeni laa sivyo pengine kungekuwa na wabunge wasiozidi kumi ktk bunge la Jamhuri..Na kibaya zaidi ni kwamba ktk maswala ya Muungano mengi hayana mjadala isipokuwa serikali iliyopo madarakani hutuburuza wote, bara na visiwani.

  Wazanzibar hata kama mnawakilishwa na wabunge zaidi ya mia moja kwa dhana ya maslahi ya Zanzibar bado haiwezi kuwasaidia kitu kwani sisi Bara pamoja na kuwa na zaidi ya robo tatu ya Wabunge wote, hakuna la maana linalofanyika bara..tena naweza sema Zanzibar inabadilika haraka sana kiuchumi kuliko hata bara na sababu kubwa ni uwakilishi na wabunge wengi wa Zanzibar ni wazaliwa na wakazi wa majimbo wanayogombea tofauti na bara ambako wananchi humwona Mbunge wao mara moja au mbili kwa mwaka mzima..Sasa sijui nao tuwaulize huwakilisha kina nani? Lakini kama umechunguza sana wabunge hao hao wa Zanzibar baada ya miaka yao bungeni hujikita Bara na kutafuta makazi huko ya kudumu.. kwa hiyo kinachompeleka Dodoma ni kutafuta makazi bara..

  Kwa pamoja nadhani ipo sababu kubwa ya kudai maendeleo yetu toka kwa wabunge hawa kwani Utekelezaji wa shughuli zote za serikali imekuwa ni mchezo wa kuigiza pande zote mbili..Tanzania inakabiriwa na tatizo kubwa la uongozi - Responsibility na Acccountability ni maadili ya kigeni kwetu...Fedha za serikali zinaliwa nje ndani na ndio maana hesabu za matumizi ya serikali hazikubaliani na kibaya zaidi ktk matumizi hayo hayo hakuna kilichojengwa..Miaka yote tunafungiwa mbuzi ktk gunia..

  Mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali amekuta madudu kila wizara za serikali na mashirika ya Umma, na zaidi ya hapo kamati za Bunge pia zimekuta hakuna kilichojengwa wala kununuliwa kulingana na gharama zilizokuwa ktk mahesabu..Hivyo tunaibiwa ktk makaratasi na tunaibiwa tena on the ground ktk ujenzi wa taifa..

  Hivyo mkuu wangu una kila haki ya kuuliza kwani unafikiria Wabunge kuwakilisha Zanzibar pasipo kujua kwamba dhumuni la Ubunge wao ni kuwakilisha matumbo yao... at no time Wabunge wetu wamewakilisha haswa matakwa ya wananchi labda tuanze sasa na Zanzibar mnaweza kutoa mfano mzuri kwa kuanzia..
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Kelele za kuwa wabunge kutoka Zanzibar ni wengi tunapiga au huzisikii?

  Mimi kama wewe naona ni ufujaji wa fedha.
  Lakini pia sikubaliani kuwa na Bunge la Muungano lenye wabunge wengi kama hivi sasa. Bunge la muungano lingekuwa dogo kama la wabunge 30, 40 tu. Wabunge hawa wangewakilisha sehemu zao, yaani Tanganyika na Zanzibar kama katika EAC.

  Halafu lingekuwepo bunge la Tanganyika hili ndio lingefanya kazi kama bunge la ndani kama vile ambavyo ninyi mnalo lenu la "Baraza la Wawakilishi".

  Nafikiri maneno umeyamaliza uliposema yanayofanyika ni mchezo wa kisiasa tu ambao unaongeza utata wa Muungano. Si ajabu kuwa baada ya miaka 47 hakuna nchi nyengine iliyotaka kujiunga nasi katika muungano huu.
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hili zengwe na mkanganyiko wa muungano can only be solved by serikali tatu. Nashangaa CUF wamekaa kimya baada ya kuwa moja ya muundo wa serikali, hali kampeni zao zote kama walivyo Chadema walipigia debe kufanikisha swala hili.

  Kuwepo serikali ya Tanzania visiwani (Zanzibar), Serikali ya Tanzania Bara (Tanganyika) na Serikali ya Muungano (Tanzania). Ila hapa napo patakuwa na mambo mengine kibao kwenye nyuso za kimataifa, haswa kwenye swala la wabunge na uwakilishi wao. Lakini serikali ya Uingereza mbona wanaonekana kuweza? Wao huko nawao si ni yale yale... Kuna Wales assembly, Scottish Assembly, Northern Ireland na Bunge la Uingereza!!! Kama wao na lile Bunge la Ulaya, sasa je nasisi tutakapoongezea na lile Bunge la Afrika mashariki na lile la uwakilishi bara Africa sijui wawakilishi wetu watatoka kwenye Bunge lipi, la muungano, Zanzibar au Tanganyika??!
   
 11. A

  Albimany JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Sera ya Serekali Tatu utakapoisikia popote ndani ta Tanzania Unapaswa kujua kua Ni CUF ndio waanzilishi wa sera hiyo.

  Jengine Utakaloliona kuhusu mageuzi ya kisiasa ndani ya Tanzanie hile ujue kua kilianzia Zanzibar kwanza baadae ndio kikafika Tanganyika.

  Hii ndio kusema Zanzibar nikicha cha Tanzania.
   
 12. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Nilikusudia kwamba hizi ni hoja zinazojitegemea ndugu yangu na si vyenginevyo.

  Ndio tumeanza kuchukua hatua za kujinasua hivyo na uvamizi wenu.

  Kweli kabisa Muungano huu siupendi and cant wait to see your backs.
   
 13. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Ngugu yangu umeanza kwa kutaka isilaumiwe Bara kwa mfumo huu na kujaribu kuhalalisha matumizi mabaya ya fedha eti kwa vile hata hao Wabunge wa bara hawaleti maendeleo.

  Hili linanifanya nizidi kuamini ile dhana yangu kuwa Bara mko tayari kutowa muhanga ili muendelee kuikalia Zanzibar. Hata hivyo bado hujanieleza hawa Wabunge wa Zanzibar wanawakilisha kitu gani Bungeni. Imani yangu ni kuwa mbunge anakuwa mtu wakati kati ya waliomtuma na maamuzi ya kimaendeleo kutoka Bungeni. ikiwa hivyo ndivyo na Wazanzibari mambo yao yanashughulikiwa na Serikali ya Mapinduzi na kule kuna chombo kinachoitwa Baraza la Wawakilishi, sasa hawa Wabunge na Bunge lenyewe lina kazi gani kwa Zanzibar?
  Unatwambia kuwa Wabunge wa zanzibar wakimaliza muda wao wanabaki Tanganyika na kuwa lengo lao hasa ni kutafuta makazi. Naam uko sahihi kwa hilo lakini hili ndio liwe sababu ya kupoteza fedha na kuacha kufanya yaliyo namaana ?
  Zanzibar tuko wachache na zaidi ya kejeli zenu kuwa mnatubeba hatuoni tabu kwa ndugu zetu kujitajirisha na mfumo huu lakini tunachotaka ni kwenu ndugu zetu wa Tanganyika muache unafiki wa kusema mnatubeba na huku kumbe mnatowa hongo ili mzidi kutuweka katika himaya yenu na kama si hivyo basi tuwe wakweli tuwe na BUNGE LA MUUNGANO!
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Tatizo letu Watanzania nikutaka kwenda mbele kabla ya kuhakikisha kuwa hapa tulipo tumeondowa matatizo. Mimi sikubaliani na kuufananisha Muungano wetu na wa nchi nyengine. Muungano ni wa Nchi mbili huru na hatukubaliana kuifanya kuwa nchi moja. Tatizo sas kila upande unavutia kwake na kama ilivyo desturi alie mkubwa ndie aliye na nguvu. Uingereza si muungano wanchi huru katika dunia yetu ya sasa. Zanzibar hadi 1977 ilikuwa inajiendesha kama nchi huru, kuifananisha na Uingereza ni sawa na kufananisha chiefdoms kabla ya kuja wakoloni.
   
 15. N

  Nonda JF-Expert Member

  #15
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Katika hili tatizo ulilolisema hapa, naona unayo point.
  Ukiangalia kauli kama hii

  Au nyengine nyingi tunazozitoa kuwa Zanzibar ni ndogo na wakaazi kidogo bila ya kutoa uzito wa kuwa nchi ya Zanzibar iliunganisha mambo na Tanganyika na hivyo kuwa mbia mwenye haki sawa, huwa ndio sababu ya mkorogo na utata unaoendelea.

  Ikitokea kila mtanzania kuelewa dhana hii ya kuwa Zanzibar ni mbia sawa wa Muungano basi matatizo au kero zitaanza kushughulikiwa kwa stahili ile inayopasa. Yaani kwa majadiliano ya pende mbili zilizounda muungano wenyewe kama wabia wa joint venture.

  Ili kufanyika hili, linategemea political will na nia njema ya viongozi hasa wa upande wa Tanganyika katika kurekebisha kosa hili ambalo limedumu tokea kuasisiwa kwa muungano huu.

  Kwa kujaribu na kufanya kila juhudi na kila mbinu kuipunguzia mamlaka na kuishusha hadhi nchi mbia ndio kosa litakaloleta maafa siku za usoni. Au zitapelekea Wazanzibari kuukana Muungano kama ambavyo dalili zimejitokeza sasa wakati wa ukusanyaji maoni juu ya Muswada wa "Katiba mpya".

  Kama viongozi wetu bado wana nia na hamu ya Tanzania iendelee kuwepo basi ni lazima wafanye ujasiri wa kurudi katika njia sahihi ya kuheshimu mikataba ya kimataifa baina ya nchi zinazoingia mikataba hiyo. Zanzibar haikuwa annexed but we behave as we did just that!

  Nimesema inahitaji ujasiri kwa sababu italazimu hii tunayoiita "bara" au Tanzania bara ichukue hadhi ,nafasi yake na jina lake la asili ambalo kwa miaka kadhaa sasa limekuwa ni taboo kusikika au kutamkwa.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana, sera ya serikali 3 imeanzishwa na group of 55. Sidhani kama CUF walikuwemo kwenye kundi hilo.
   
 17. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  "Kama viongozi wetu bado wana nia na hamu ya Tanzania iendelee kuwepo basi ni lazima wafanye ujasiri wa kurudi katika njia sahihi ya kuheshimu mikataba ya kimataifa baina ya nchi zinazoingia mikataba hiyo. Zanzibar haikuwa annexed but we behave as we did just that"

  Mkuu kwa tulipofikia, hata hao Viongozi wakitaka, sisi Wazanzibari hatuutaki huu unaoitwa "Muungano" maana si Muungano. Hii inatokana na sababu kubwa mbili.

  Kwanza ni kuwa wanaofaidi imedhihirika kuwa ni viongozi fulani tu wa hizi pande mbili na pili hauwezi kurekebishika ila kuuvunja na kama kuna haja ya kuwa pamoja, basi kama ulivyosema, utokane na misingi ya kuheshimiana.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwangu mimi naona wanajiwakilisha wenyewe! Wazee wa posho Hao kwa kisingizio cha muungano
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sikufikiria kuwa iko siku mawazo yangu na kizee wewe yatalingana. Katiba mpya inakuja haya ya manufaa binafsi tuyaweke pembeni.
   
 20. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hoja zako ni nzuri na nimezipenda hasa.

  Kwako nna suala dogo tu, jee mambo yasio ya Muungano, Zanzibar itasemewa na nani huko EAC?

  Tafakari Mkuu na hili pia.
   
Loading...