Tuwe wakweli - Uwezekano wa katiba mpya kabla ya 2015 upo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe wakweli - Uwezekano wa katiba mpya kabla ya 2015 upo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Massenberg, Oct 18, 2011.

 1. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Zingatia yafuatayo halafu upime uwezekano wa katiba mpya kabla ya 2015:

  1 - Mijadala ya katiba mpya inaendeshwa kwenye TV mijini wakati kuna watu wengi sana vijijini hata katiba ni nini hawajui. Uwezekano wa kila mtu kufikiwa na kuelewa umuhimu wa katiba mpya ndani ya miaka minne ni mdogo hasa ikizingatiwa serikali haina mpango wa kupata hiyo katiba hivyo basi tofauti na miradi ya ukimwi na malaria hawatatoa msaada wowote kuwafikia wananchi na habari ya katiba mpya.

  2 - Tabia za viongozi kuendelea kuvunja utaratibu na kupuuzia maslahi ya nchi bila woga (brazen confidence) kwa sababu wanajua hawataruhusu kuwepo katiba itakayowaadhibu kwa hiyo hawana cha kuogopa. Mfano ni huo wa Pinda kuuza nchi kwa Wamarekani bila ridhaa ya wananchi. Ipo pia tabia sugu ya kurithishana na kupeana nyadhifa ili kuendeleza kulindana siku za baadaye. Iko mifano mingine chungu nzima.

  3 - Uongozi uliopo madarakani umefanya madudu mengi yasiyoelezeka na kwa sababu hiyo utahitaji kuwepo serikali itakayowalinda kwa gharama yoyote ile.

  4 - Hekaheka za makundi yaliyomo CCM kupigania urais 2015 zinatokana na uhakika walio nao kuwa hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea na kuleta katiba mpya na kwamba rais ajaye atatoka CCM watu watake wasitake.
  Mipango inayosukwa ni ya kutotoa fursa ya katiba inayohitajika.

  5 - Namna ambavyo mchakato wa katiba umepangwa kufanyika inawanyima wananchi fursa ya kuumiliki na badala yake serikali ndiyo inauendesha kiulaghai. Je, serikali hii itakuwa tayari kusimamia mkakati utakaoiweka yenyewe na CCM kitanzini pindi utakapokamilika? Haiwezekani.(Tafuta picha ya Jaji Werema halafu uiangalie sura yake kwa sekunde kadhaa nadhani utanielewa vizuri. Ile si sura ya mabadiliko!).

  6 - Ukiangalia upunguzwaji wa madaraka kwa rais kama ambavyo katiba mpya tutapenda iwezeshe ni kwamba kwa hulka za wanasiasa wa Kitanzania ni jambo gumu mno kukubaliana nalo. Hii inatokana na utamaduni wa ubadhirifu na kulindana ambapo rais atataka apate fursa ya, kwa mfano, kuchagua wakuu wa vyombo vya dola watakaolinda ufedhuli wake pamoja na wakuu wa mikoa na wilaya watakaofanikisha madili yake huko kwenye mikoa husika.

  7 - Wananchi wengi hatuna mapenzi ya dhati kwa nchi yetu. Hii inatokana na sababu kadhaa lakini mojawapo ni kukata tamaa na kukubali matokeo na hivyo kutokuwa na msukumo wa kutaka mabadiliko hata kwa lazima. Hii inasababisha hata wale walio mstari wa mbele kudai mabadiliko waonekane kama kichekesho maana watu wanaamini mambo hayatakuja kubadilika. Wengi bado wanadhani au kuona kuwa wanaharakati na vyama vya siasa ndiyo wenye jukumu la kubadilisha mambo wakati hili ni jukumu la kila mtu.

  8 - Tofauti na nchi zingine sisi tuna hulka ya uoga hasa wa kupambana kudai haki zetu. Hii inasababishwa na watu wengi kutokujua haki zao na kwamba haki hudaiwa maana ni mali yako, mfano, maana mara nyingi utasikia watu wakisema, "Tunaiomba serikali..." Serikali haiombwi bali inatakiwa itekeleze majukumu yake kwa sababu ni haki ya wananchi ambao ndiyo wenye serikali. Kwa sababu hii ninahofia hata siku serikali ikisema hakutakuwa na katiba mpya watu watalalamika tu kwenye vyombo vya habari halafu basi maisha yataendelea, mifano ya namna hii iko mingi.

  9 - Asilimia kubwa ya vyombo vya habari ni madalali wa kurudisha nchi nyuma. Hivi vinapaswa kushika usukani wa kuwaongoza wananchi kuelekea kwenye katiba mpya lakini kwa kutokuwa na uzalendo vingi vinatumika hata kuponda juhudi za mabadiliko. Rushwa na maslahi ya haraka haraka vimeharibu kabisa uwezo na utashi katika vyombo hivi hapa nchini.

  Hizi ndizo hofu zangu, naomba kuwasilisha.
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hofu uliyonayo kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya si kwako tu ni kwa Watanzania wengi, hasa pale Serikali inapokuwa hainania ya dhati katika kuleta demokrasia nchini. Kunadalili nyingi tu ambazo ni kielelezo kuhusiana na hofu hiyo, lakini tuiulize Serikali kamakweli inajua madhara ya kutokupitishwa kwa Katiba mpya? Kikubwa kabisa ngoja tusubiri Bunge lijalo kama mchakato huo utawasilishwa Bungeni, kisha makamanda wetu watatuambia la kufanya.
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kuna ugumu kwa kweli. Na wengi tuna imani ndogo kama wewe. Ila usiseme waTZ ni waoga. Ujue kama JKN asingeng'atuka,miaka 10 ama 15 iliyopita tungeshang'oa Magogoni! Hivi sasa tunaendeshwa kwa mtindo wa kung'atwa na kupulizwa. Sasa watakapolewa,na ukilewa unajisahau..basi, vijana wa kipindi hicho (pengine hakiko mbali) wataingia mitaani. Sisi hatuli mikate kama Msumbiji ambako bei yake ikipanda,watu wanaandamana. Sisi tutakuwa na chanzo tofauti..wajua tumeghilibiwa kiasi cha kutosha. Ikifika wakati huo hata hutajua support inatokea wapi. Hatuombei tufike huko lakini! Ila wenye madaraka wasome thread yako,waelewe wewe uliyeandika ni mmoja ila unawakilisha nafsi MILIONI MOJA! Asante.
   
 4. T

  Topical JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nashangaa aise hii kitu muhimu sana imekosa msukumo..wa haraka..

  Katiba mpya ni muhim wakuu
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  When I fought for revolution I started with 82 men.If I had to do it again,I will need 10 or 15! Nothing is impossible if you have Absolute Faith and Plan of Action.. [Fidel Castro]
   
Loading...