Tuwe wakweli, ukiondoa Wahindi na Waarabu tunabakia na nini Tanzania?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Itabakia NSSF, Tanesco, CRDB, NMB labda na mwendo kasi, hata ubishi wa mpira utaisha Tanzania kwani bila ya Wahindi /Waarabu hakuna Simba, Yanga wala Azam.

I mean, sisi watu weusi inabidi tuamke kwa kweli. Idi Amini alifukuza Wahindi baadaye wakaenda kuwapiga magoti warudi, kuna jamaa (mweusi mwenzangu) alitaka kunipiga ngumi kisa nimemuongelea MO asivyotaka kusikia, nilitafakari nikakosa jibu.

Sasa hivi Tanzania hata Utalii bila ya kampuni za Wahindi hakuna kitu, BTW Wahindi Tanzania nzima ni < 200 000 sisi tuko zaidi ya milioni 45.

Heri ya Mwaka mpya 2021
 
Mkuu mbona unajidharau sana inamaana hujaona Vitego uchumi Vingi vilivyowekezwa sisi kama sisi Viwanda vya nondo, vya Cement, Hospital, Mabank, , Timu za mipira na uwekezaji mwengine we unaona wahindi na Waarabu tuu acha kuzungua mkuu
 
Tuendelee kujifukiza. Ah eti kujifukiza. Maisha yaendelee bro maana bado haijatokea ikitokea tutajua tunafanyaje.

Kichwa BoX
 
Hili ni Jambo dogo tu,

Youtuber wa Tanzania kawekewa vikwazo vizito, anachungulia Jela muda wowote.

Kufungua YouTube channel Tanzania leseni $900 wakati huo huo kama unarusha Drone unatakiwa kulipia $100 kila mkoa unakoenda.

Cha Ajabu, juzi Serikali imempokea na kumpa hadhi ya kitaifa Youtuber "Mzungu" ambaye hana maajabu zaidi ya hawa wa kwetu.

Katika mazingira hayo unatarajia mtu mweusi apige hatua kivipi?

Na Je, utafanikiwa katika yapi kwa jambo kubwa?
 
Sidhani kama ni kweli, kwani hata Kenya ni hivyo hivyo Uchumi wote na Makampuni makubwa ni ya Wahindi, na Kenya hawajawahi kuwa na ujamaa, ...
Hata kenya angalau kuna weusi wanazo hela. Lakini na wao ni yaleyale.
1. Hofu ya kupinduana.
2. Kuendeleza mali ya urithi.
3. Connection na watu wazito.
4. Kampuni zingine ni za vigogo ila hao wahindi/waarabu wapo kama pambo/cover/barakoa.


Nchi za kiafrika ambazo zilikuwa na waarabu/wahindi wachache zilipitia majanga ya kupinduana na vita za wenyewe kwa wenyewe.
Mfano fatilia historia ya.
1. Nigeria (walipinduana mno)
2. Ghana (walipinduana mno ila JJ Rawlings ndio alipindua wa mwisho na kuleta demokrasia)
3. Msumbiji (Frelimo vs Renamo)
4. Angola
5. Sudan ya kusini (Salva kiir vs Riek machar)
6. Rwanda
7. Congo DRC
8. CAR
9. Liberia
10. Sierra Leone

Zipo nyingi mno. Hofu ya kupinduana na vita imeleta haya mambo. Maana mtu akipata hela anawapa pesa maluteni kanali au mabrigedia au magenerali kisha wanapindua uongozi. Au wanaanzisha kikundi cha waasi ili kuingia madarakani.
 
Back
Top Bottom