Tuwe wakweli: Ubunge umekuwa rahisi na usiotisha tena. Kuna wa kulaumiwa au kupongezwa?

Nimechoka kila ninapo pangusa page za Instagram naona watia nia ambao wengi wao wanatia mashaka kama wana uwezo wa kupambanua hoja za msingi katika taifa, upande wa wenzetu upinzani si mbaya kwa watu wao waliojitokeza wengi wao wanao uwezo.
 
Mimi si mtu mzima sana ingawa nami najongea miaka ya kuweza kugombea Urais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba yetu ya sasa(miaka 40). Hatahivyo, nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa siasa na mambo ya kinchi tangu nikiwa mdogo. Leo, nitalizungumzia Bunge kama Mhimili mmojawapo wa dola. Mingine, wengi mnajua, ni Serikali na Mahakama. Nimeanza kulifuatilia Bunge lililokuwa likiongozwa na Hayati Chief Adam Sapi Mkwawa.

Bunge hili chini ya Hayati Mkwawa lilikuwa la chama kimoja: CCM. Lakini, Wabunge walipambana kwa hoja na kulipuana kwa shahidi mbalimbali. Mbunge alipokuwa akisimama kuchangia hoja au kutoa hoja, kiti cha Spika na Wabunge wenzake walitega sikio vya kutosha kusikia 'madini' ya Mbunge husika. Ilikuwa ni hoja juu ya hoja, vijembe, kebehi na matusi havikuwepo. Kama ni 'upinzani' basi ilikuwa ni kutofautiana kwa mawazo na hoja.

Likafuata Bunge la Spika Pius Msekwa. Lilifanana pakubwa na lile la Chifu Mkwawa ingawa hili lilikuwa na Wabunge kadhaa wa upinzani kama wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi. Hatahivyo, hoja kinzani zilitolewa hata na Wabunge wa CCM. Katika Bunge hili, kashfa za kifisadi ziliibuliwa na wapinzani na hata Wabunge wa CCM. Ndipo paliposhamiri hoja nzito za Mzee Mzindakaya na wengineo (mfano kumhusu Waziri Mbilinyi na Waziri Simba).

Likaja Bunge la Hayati Samwel Sitta. Bunge la Viwango na Ubora. Likajionyesha na kujisimamia hivyo. Hoja, kutoka CCM na wapinzani zikawa motomoto na za uhakika. Bunge hili lilimuweka kwenye chati Balozi Slaa, kwa kumtaja mmoja. Baadaye likaja Bunge la Mama Makinda. Ufanano mkubwa wa Mabunge haya ya Hayati Sitta na Mama Makinda ni 'uhuru' wa Wabunge kutoa hoja zao na kutumia tafiti kujenga hoja zao. CCM na wapinzani walifanana katika hilo.

Baadaye, hivipunde, likaja Bunge la Spika Ndugai. Hakika, Bunge hili lilianza vyema katika kufuata nyendo za watangulizi wake. Halafu, mambo yakabadilika. Bunge likawa sehemu ya 'mapambio', 'kejeli', 'vijembe', matumizi makubwa ya maneno ya kuudhi na kutweza na kadhalika. Katika hali hiyo, Wabunge wengi wa upinzani wakajikuta kwenye wakati mgumu wa kukumbana na adhabu za mara kwa mara. Si kwamba wa CCM hawakuwa wakitenda makosa, ila wingi wao na kiti cha Spika viliwabeba.

Bunge la Ndugai limeonyesha taswira la Bunge lijalo. Limeonyesha uzito au urahisi wa Ubunge na kuwafanya maelfu ya watanzania kutamani kuwa Wabunge. Kiukweli, kama ni wa CCM wanaamini kuwa wakiwa Wabunge hali itakuwa ile ile. Wanajiamini na kuona kuwa hakuna haja ya 'hard work' katika Ubunge wao. Kwa wapinzani, wao wanatamani na kuamini kwenda kuendelea kupambana na kiti cha Spika. Hoja zinawekwa kando. Labda yaonekana hoja si ajenda tena ya Bunge lijalo. Mambo yamekuwa rahisi na kila mtanzania anaweza kuwa Mbunge.

Kuna wa kulaumiwa au kupongezwa kwa kufikisha hali hii ya Bunge na Ubunge kwa ujumla?
Wabunge wengi kwenye awamu hii ya kwanza ya Magufuli wame prove kuwa ni vilaza na vichwa maji.

Tulikuwa tunaona matamko mbalimbali Ya paul Makonda akiwadhihaki wabunge, lakini cha ajabu na yeye anataka kujiunga na hilo kundi ambalo kwa wakati huo alikuwa analiona si lolote si chochote.
 
Mimi nina lawama kwa mzee kikwete alitelekeza katiba mpya kwa hali ya sasa hatuhitaji mbunge anayejua kusoma na kuandika tu ,diwani angekuwa ni diploma,mbunge awe na shahada,rais awe na shahada na uzoefu lakini kwa kweli kikwete .....
Akiharibu Mwana CCM ni sawa,waliopo CCM huwa wakiamua hakuna wa kuhoji au kurekebisha?Tanzania siyo mali ya CCM.Mbona mnashindwa kuelewa jambo hili rahisi.
 
Ndugu mleta hoja.
Umeanza kwa kuweka historia unayofahamu wewe kuhusu bunge la tanzania, ukijaribu kuhalalisha kile kinachoitwa leo kuwa ni bunge dhaifu.
Kwa asili binadamu ni mgumu kukubali madhaifu yake kama ilivyokea kwa Ndugai vs Prof Assad.
Sababu mbili zimetajwa sana kuwa ni chanzo cha bunge letu kuwa dhaifu na hivyo kila mmoja kuona anaweza kuwa miongoni mwa watunga sheria.
Sababu hizi ni kiwango cha elimu na umaskini katika jamii, ingawa tunajisifu kama taifa kwa kupaa na kuingia uchumi wa kati kabla ya wakati!
Nakumbuka spika aliyemaliza muda wake, job ndugai, aliwahi kutamba kuongoza bunge lenye wasomi wengi wa ngazi za uprofesa, uzamivu,uzamili shahada na astashahada. Kuliko mambunge yote yaliyowahi kuwepo tangu Tanzania au tanganyike iwepo.
Lakini kiukweli bunge hili lenye idadi kubwa ya wasomi na huku wengi wakiwa wafanyabiashara wenye ukwasi mkubwa, ndio hao waliotufikisha mahali pa chombo hicho kupoteza mvuto wake.
Nyani Ngabu, kasema vyema kuwa, tusiifanye kazi ya ubunge kuonekana zaidi sana ya kazi nyingine. Nionacho mimi ni kweli tunapeleka watu sahihi kwa kazi sahihi?
Nakumbuka wakati wa hoja G55 bungeni ya akina Ulimwengu, bunge halikuwa na idadi kubwa ya wasomi wabobevu" kama wa sasa lakini tuliona likifanya kazi yake, kwa kujenga hoja,tena zenye mantiki.
Lini katika bunge hili la kisasa umesikia mshahara wa waziri umeshikiliwa? Wwsomi hawa wanaona vitu kwa kutumia nini?
Mchangiaji mmoja kanena vyema kuwa, ubunge wa sasa unafuata umaarufu badala ya akili na uchungu wa nchi. Kwangu mimi hivi ndio vingejuwa vigezo kwa kila mpiga kura kuelimishwa na avitumie kuchagua mwakilishi wake.
Mchanganyiko unaotokana na vigezo hivyo kufanya kazi ya kuwakilisha wananchi ukichagizwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi unaweza kurejesha hadhi ya bunge letu.
 
Hata kama kazi ya kuwakilisha wananchi si ndogo, hiyo haina maana kazi hiyo ndo iwe ngumu na ya kutisha!

Kwa nini iwe ngumu? Ugumu wake ni nini hasa?

Zaidi, kwa nini itishe?

Uchaguzi wako wa maneno umekosa umakini [pengine kuliko hata hao uliolenga kuwakosoa].

Kuwakilisha wananchi siyo sayansi ya maroketi ya kwenda angani wala si upasuaji wa ubongo.
We una akili fupi sana
 
Kwny Bunge la 2020-2025 Spika anatoa tangazo:

" kikao chetu cha mchana khs Muswada wa kuruhusu matumizi ya Nishati ya Nuclear kuzalishia umeme ataanza Mh. Harmonizer kuchangia hoja then atafuatiwa na Mh. Steve Nyerere akitoka hapo Mh. Kingwendu nae anatoa hoja zake huku Mh. Musukuma akipewa dakika tano za kuongea na tutafunga kikao chetu kwa hoja za Mh. Babu tale.'

Hakika hili litakua bunge la kisayansi.
 
Nami natarajia something unpredictable to happen from 2020...

Magufuli kaleta siasa za kuboa ile mbaya, kama ingekuwa ni kwenye soka, ni sawa na ile team inayocheza kwa kupack basi. Kwenye siasa za aina hiyo huwezi kutabiri nini kitatokea, maana sehemu kubwa siasa inakosa ushindani halisi, bali inategemea mtazamo wa refarii.
 
Back
Top Bottom