Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,745
- 5,446
Wadau, salaam! Kwa kawaida mimi hutafakari kila jambo linalotokea nchini mwetu.
Wiki iliyopita rais wetu mpendwa JPM alifanya teuzi kwa nafasi za makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya ili kuboresha utendaji wa serikali. Hata hivyo miongoni mwa wateule ni Adam Malima aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara, na Alexander Mnyeti kuwa mkuu wa mkoa ambao siukumbuki.
Nimewataja hao wawili kwa kuwa Adam Malima alikuwa na kesi ya jina mahakamani kwa tuhuma za kumzuia askari wa jeshi la polisi kutimiza wajibu wake na baada ya uteuzi wake DPP amefuta kesi dhidi yake. Alexander Mnyeti yeye anachunguzwa na PCCB kwa tuhuma za rushwa na kwa kitendo cha DPP kumfutia kesi Malima sidhani kama PCCB wataendelea na uchunguzi dhidi ya Mnyeti.
Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa mfano wa mke wa Kaisari kutuhumiwa kusaliti ndoa yake na Kaisari akamwacha. Alipoulizwa sababu za kumwacha mkewe ilihali ilithibitika kuwa tuhuma dhidi yake hazikuthibitishwa; Kaisari alijibu kuwa mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
Hata kama wateule hao wa rais wanatuhumiwa tu, kimaadili na kwa kanuni za utawala bora uteuzi wao haukupaswa kufanyika hadi baada ya vyombo vinavyohusika -PCCB na Mahakama kuwasafisha dhidi ya tuhuma zao.
Ili kujenga utawala wa sheria kama ambavyo serikali ya JPM imekuwa ikisisitiza, ni vema Rais ajiepushe na teuzi za namna hiyo ili kujenga heshima yake binafsi, heshima ya taasisi yake,na heshima ya serikali na vyombo vyake vya dola kwa ujumla.
Vv