Tuwe wakweli, tatizo la nchi hii ni Mawaziri au Rais wa nchi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Kila taarifa ya CAG na ile ya kamati za bunge kuhusu mahesabu ya serikali zinapowasilishwa bungeni ndio mwanzo wa kusema mawaziri akiwemo waziri mkuu ni mizigo na wanapaswa kufukuzwa.

Hata hivyo,mabadiliko yoyote ya serikali hii ya awamu ya nne ni mpaka bunge lishinikize licha ya uozo na uzembe wa watendaji hawa ukiwa ni jambo la wazi kabisa.

Sasa watanzania wenzangu,tukiwa wakweli na tusiwe na hata chembe ya unafiki,hapa tatizo ni mawaziri au Raisi anaewateua?

Labda swalil la msingi ni kuwa ikiwa anaewateua atakuwa muwajibikaji itawezekana mawaziri wawe wazembe?

Jambo lingine la kutafakari na kujiuliza ni kuwa kwa hii katiba inayompa Raisi madaraka makubwa ya kuweza kuwa hata "dikteta" lakini bado Raisi anaonekana kuwa dhaifu kiutendaji,je, huu sio ushahidi mwingine kuwa Raisi kazi imemshinda?

Naomba maoni yako.
 
Kila taarifa ya CAG na ile ya kamati za bunge kuhusu mahesabu ya serikali zinapowasilishwa bungeni ndio mwanzo wa kusema nchii mawaziri akiwemo waziri mkuu ni mizigo na wanapaswa kufukuzwa.

Hata hivyo,mabadiliko yoyote ya serikali hii ya awamu ya nne ni mpaka bunge lishinikize licha ya uozo na uzembe wa watendaji hawa ukiwa ni jambo la wazi kabisa.

Sasa watanzania wenzangu,tukiwa wakweli na tusiwe na hata chembe ya unafiki,hapa tatizo ni mawaziri au Raisi anaewateua?

Labda swalil la msingi ni kuwa ikiwa anaewateua atakuwa muwajibikaji itawezekana mawaziri wawe wazembe?

Naomba maoni yako.

Q
Ameshabadili mawazir mara kadhaa lakin hali bado ni ile ile which concludea that Rais Dhaifu kama alivyosema mh Mnyika
 
Rais ni mbovu na hivyo siku zote kuchagua mawaziri wabovu,,,kwa ujumla wote ni wabovu.Unless unataka tatufa cause..then Rais atabaki kuwa Mbovu wa kwanza anayezaa wabovu wengine.
 
Huu ndio ukweli ambao hausemwi bungeni.Mimi naamini wabunge wengi hawataki kusema ukwelu huu kuepuka kumuudhi Raisi na hivyo kujiweka katika mazingira magumu ya kukosa uwaziri endapo baraza la mawaziri litavunjwa.

Kwa mfano,kutotekelezwa kwa maazimio mbalimbali ya bunge,mfano azimio kuhusu Richmond,Jairo na mengine mengi ni tatizo la waziri mkuu pekee bila Raisi kuwakingia kifua watu hawa?

Wabunge acheni unafiki,mnapaswa kupiga kura ya kutokuwa na imani na raisi na sio hao mawaziri mizigo.
 
Nadhani si Rais wala Mawaziri wenye matatizo, nadhani system nzima ndiyo yenye matatizo, yaani system yenyewe ndiyo ipo hivyo. Tunachohitaji ni vyama 2 au 3 tu vya siasa.
 
Mkuu hebu fafanua kidogo.

Kwa katiba hii, Raisi anashindwaje kutimiza wajibu wake?

Hata kama system ni tatizo but not to this extent!
 
Nadhani si Rais wala Mawaziri wenye matatizo, nadhani system nzima ndiyo yenye matatizo, yaani system yenyewe ndiyo ipo hivyo. Tunachohitaji ni vyama 2 au 3 tu vya siasa.
Hiyo idadi itafikiwa mara vyama vya siasa vitakavyokuwa vigumu kuvianzisha na kuviendesha ..haswa ianpokuwa ngumu kupata wanachama na kuja na kitu kipya cha kuwavutia...
 
Nadhani si Rais wala Mawaziri wenye matatizo, nadhani system nzima ndiyo yenye matatizo, yaani system yenyewe ndiyo ipo hivyo. Tunachohitaji ni vyama 2 au 3 tu vya siasa.

System ni nini? Sheria za nchi? What is it exactly do you mean by system?
 
Kila taarifa ya CAG na ile ya kamati za bunge kuhusu mahesabu ya serikali zinapowasilishwa bungeni ndio mwanzo wa kusema nchii mawaziri akiwemo waziri mkuu ni mizigo na wanapaswa kufukuzwa.

Hata hivyo,mabadiliko yoyote ya serikali hii ya awamu ya nne ni mpaka bunge lishinikize licha ya uozo na uzembe wa watendaji hawa ukiwa ni jambo la wazi kabisa.

Sasa watanzania wenzangu,tukiwa wakweli na tusiwe na hata chembe ya unafiki,hapa tatizo ni mawaziri au Raisi anaewateua?

Labda swalil la msingi ni kuwa ikiwa anaewateua atakuwa muwajibikaji itawezekana mawaziri wawe wazembe?

Naomba maoni yako.

Tatizo ni kizazi kilichopo cha watawala na watawaliwa
 
Nadhani si Rais wala Mawaziri wenye matatizo, nadhani system nzima ndiyo yenye matatizo, yaani system yenyewe ndiyo ipo hivyo. Tunachohitaji ni vyama 2 au 3 tu vya siasa.

Inaonekana unalijua tatizo ila unajifanya aghali sana mpaka ubembelezwe kufafanua tuuuuu
 
Rais hana tatizo. Hao wanaosema kama huwezi kulipia umeme tumia kibatari ndio wanaomwangushag
 
Haya ni matokeo ya matatizo kuanzia juu mpaka Kwa mwananchi Wa kawaida!
Hakuna Cha wabunge, mawaziri, Na ata Huyo top wao!
Kote ni shida!
Na Kwa mfumo huu uliopo Wa vitu kwenda ilimladi, yani sisi Tz bado sana!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom