sukankanwa
Member
- Nov 20, 2013
- 92
- 8
Tatizo mawaziri wote wanalinda naslai ya chama,bora wafisadi serikalini kuilinda ccm,ndiyo maana fedha zinaliwa wa kuwapigia kelele hayupo zaidi ya kufanya usanii.
Tatizo si Rais wala Mawaziri wake isipokuwa ni wananchi wenyewe kuhongwa kipindi cha uchaguzi na kukubali kuchagua viongozi wabovu kwa hiyo sisi ndo wabovu,hatutaki kukataa rushwa
Kila taarifa ya CAG na ile ya kamati za bunge kuhusu mahesabu ya serikali zinapowasilishwa bungeni ndio mwanzo wa kusema nchii mawaziri akiwemo waziri mkuu ni mizigo na wanapaswa kufukuzwa.
Hata hivyo,mabadiliko yoyote ya serikali hii ya awamu ya nne ni mpaka bunge lishinikize licha ya uozo na uzembe wa watendaji hawa ukiwa ni jambo la wazi kabisa.
Sasa watanzania wenzangu,tukiwa wakweli na tusiwe na hata chembe ya unafiki,hapa tatizo ni mawaziri au Raisi anaewateua?
Labda swalil la msingi ni kuwa ikiwa anaewateua atakuwa muwajibikaji itawezekana mawaziri wawe wazembe?
Naomba maoni yako.
Nadhani si Rais wala Mawaziri wenye matatizo, nadhani system nzima ndiyo yenye matatizo, yaani system yenyewe ndiyo ipo hivyo. Tunachohitaji ni vyama 2 au 3 tu vya siasa.
Kila taarifa ya CAG na ile ya kamati za bunge kuhusu mahesabu ya serikali zinapowasilishwa bungeni ndio mwanzo wa kusema nchii mawaziri akiwemo waziri mkuu ni mizigo na wanapaswa kufukuzwa.
Hata hivyo,mabadiliko yoyote ya serikali hii ya awamu ya nne ni mpaka bunge lishinikize licha ya uozo na uzembe wa watendaji hawa ukiwa ni jambo la wazi kabisa.
Sasa watanzania wenzangu,tukiwa wakweli na tusiwe na hata chembe ya unafiki,hapa tatizo ni mawaziri au Raisi anaewateua?
Labda swalil la msingi ni kuwa ikiwa anaewateua atakuwa muwajibikaji itawezekana mawaziri wawe wazembe?
Naomba maoni yako.
Ok, kwa hiyo tukiwa na vyama vitatu kama CCM, TLP na UDP Basi matatizo ndio yataisha?