johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,915
- 141,870
- Thread starter
- #41
Chadema walifanya mchakato wa ndani wa kuwapata wagombea wa viti maalumu?Utaratibu wa viti maalum unapaswa kuwa hivi.
1. Uchaguzi mkuu ukishafanyika, tume ya uchaguzi inatangaza nafasi za viti maalum kulingana na kila chama kilivyopata kura.
2. Chama husika kinafanya mchakato wake wa ndani kupendekeza majina ya wanawake kutoka chama chao. (Kila chama kina utaratibu wake wa ndani kulingana na katiba ya chama husika, na mchakato huo unaweza kuanza hata kabla ya uchaguzi, lakini hauwezi kukamilika mpaka uchaguzi uishe. Kwanini? Huwezi kujua chama kitapata nafasi ngapi kabla ya uchaguzi)
3. Chama husika kinaweka orodha ya majina iliyoyapendekeza kwa umma.
4. Katibu mkuu wa chama husika anawasilisha orodha ya majina yaliyopendekezwa na chama chake kwenda NEC.
5. NEC inaweka wazi kwa umma orodha ya majina ya wanawake waliopendekezwa kupewa hivyo viti maalum.
6. NEC inawasilisha rasmi hiyo orodha kwa spika wa bunge.
7. Spika wa bunge anaweka wazi kwa umma orodha ya majina ya wanawake wa chama husika walioteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum.
8. Wabunge walioteuliwa wanaampa ndani ya bunge mbele ya spika siku ya kikao cha bunge.
Kwa kawaida huwa wanatumia utaratibu gani?