Tuwe serious na uongozi wa nchi yetu

Chendembe

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
416
462
Wanabodi kiongozi ni kioo cha anaewaongoza. Kazi kubwa ya kioo ni kuangalia mwonekano wako au wa kitu ambacho macho hauwezi ona moja kwa moja. Vivyo hivyo kwa kuwa kiongozi, jamii inayoongozwa utazamwa na kupimwa kutokana na kiongozi wake.

Sinashaka na uongozi wa juu wa nchi yangu Tanzania, ila ninamashaka na watu wa karibu na uongozi huo ambao wanawajibaka katika kupendekeza wateuliwa.

Kuna dosari kubwa katika mfumo wa uteuzi wa viongozi na hata katikati idara ya utumishi katika kuteua wakuu wa vitengo, Taasisi na idara za serikari.

Process hii ya uteuzi inaathiliwa saana na ukabila, ukanda na ukada. Athali ya hayo ni kubwa mno kuliko udini hapa Tz na inapelekea kuteuliwa na kupewa dhamana wasiofaa.

Natamani kuona busara na hekima nyingi kwa wakuu wa wilaya na mikoa, hivyo, nilitarajia kuona viongozi wakomavu katika kuongoza na si ukada.

Labda macho ya wateuwaji yanaona zaidi yangu, lakini baadhi ya wateule hapana.
Niwatakie mabadiliko mema ya kiutendaji na uongozi uliotukuka wateuliwa wote.
 
Wanabodi kiongozi ni kioo cha anaewaongoza. Kazi kubwa ya kioo ni kuangalia mwonekano wako au wa kitu ambacho macho hauwezi ona moja kwa moja. Vivyo hivyo kwa kuwa kiongozi, jamii inayoongozwa utazamwa na kupimwa kutokana na kiongozi wake...
Mstari wako wa tatu, tayari unafuta kila kitu ulichozungumzia katika mistari iliyotangulia.

Mimi naunga mkono hoja yako. Kuna umuhimu mkubwa sana wa nchi hii sasa kujua viongozi wetu wanapatikana kwa njia zipi.

Hatuwezi kuwa nchi ya kuokoteza tu kiongozi yeyote na kumkabidhi madaraka ya juu kabisa bila hata kujua huyo kiongozi katokea wapi. Historia ya hivi karibuni imeonyesha udhaifu mkubwa kabisa katika taratibu za kuwapata watu wanaotakiwa kuongoza taifa hili.

Kwa hali ilivyo sasa mamluki yeyote anaweza akawa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa nchi hii bila kikwazo chochote.
 
Katiba na sheria nyingine za nchi ziko wazi kabisa jinsi viongozi wote wa nchi wanavyopatikana.Kwa hawa viongozi wote walioteuliwa karibuni hakuna mahali katiba na sheria za nchi zimekiukwa.
Mstari wako wa tatu, tayari unafuta kila kitu ulichozungumzia katika mistari iliyotangulia.

Mimi naunga mkono hoja yako.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa nchi hii sasa kujua viongozi wetu wanapatikana kwa njia zipi.

Hatuwezi kuwa nchi ya kuokoteza tu kiongozi yeyote na kumkabidhi madaraka ya juu kabisa bila hata kujua huyo kiongozi katokea wapi. Historia ya hivi karibuni imeonyesha udhaifu mkubwa kabisa katika taratibu za kuwapata watu wanaotakiwa kuongoza taifa hili.

Kwa hali ilivyo sasa mamluki yeyote anaweza akawa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa nchi hii bila kikwazo chochote.
 
Katiba na sheria nyingine za nchi ziko wazi kabisa jinsi viongozi wote wa nchi wanavyopatikana.Kwa hawa viongozi wote walioteuliwa karibuni hakuna mahali katiba na sheria za nchi zimekiukwa.
Kuna mambo mengi sana hayatamkwi kwenye katiba wala sheria, lakini yanapofanyika watu hujiuliza maswali mengi.

Uko sawa, hakuna aliyeteuliwa mwenye sifa zisizotambuliwa na sheria au katiba, hiyo haizuii watu kuhoji baadhi ya sifa walizonazo wateuliwa hadi wawe wateule kwa nafasi zao.

Na wala sijaona mtu akihoji humu JF uhalali wa wateuliwa kuhusiana na matakwa ya katiba au sheria. Wewe umeona bandiko lolote linalohoji juu ya hilo?

Katiba haitamki kila jambo na wala haizuii kutumia akili kufanya jambo lisilokatazwa na katiba au sheria.
 
Kuna mambo mengi sana hayatamkwi kwenye katiba wala sheria, lakini yanapofanyika watu hujiuliza maswali mengi....
Sijaona, ndio maana nimesema tuwe serious na uongozi, tusidemke tuu kwendana na miluzi inayopigwa.
 
Nilikuwa namjibu mkuu 'Yoda' aliyeandika kuhusu katiba au sheria kutokiukwa katika teuzi; lakini siyo neno, kwa sababu wewe na mimi tunakubaliana juu ya hili.
 
Wanabodi kiongozi ni kioo cha anaewaongoza. Kazi kubwa ya kioo ni kuangalia mwonekano wako au wa kitu ambacho macho hauwezi ona moja kwa moja. Vivyo hivyo kwa kuwa kiongozi, jamii inayoongozwa utazamwa na kupimwa kutokana na kiongozi wake...
Huu ni mchakato wa cloning. Hakuna vetting process hapo.
Halafu hayo ma-clone ndiyo wenyeviti wa kamati za usalama

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Kuna haja ya kuwa na utulivu wa kutosha kwa viongozi wetu, miluzi ni mingi, na wahenga walisema "Miluzi mingi upoteza Mbwa"
 
Sijaona, ndio maana nimesema tuwe serious na uongozi, tusidemke tuu kwendana na miluzi inayopigwa.
Saizi uongozi ni zawadi na kutafuta kupendwa na kila mwananchi. Kiongozi yupo radhi afanye jambo lolote hata kuteua mtu yeyote tu ilimradi asifiwe na aonekane mwema , weledi unawekwa pembeni.
 
Katiba na sheria kutotamka mambo mengi sana ambayo ni muhimu katika kuongoza nchi nalo ni tatizo kubwa sana.Kwa namna hiyo kila mtu anaweza kufanya vile anvyofikiri ni vyema na akawa sahihi.
Kuna mambo mengi sana hayatamkwi kwenye katiba wala sheria, lakini yanapofanyika watu hujiuliza maswali mengi.

Uko sawa, hakuna aliyeteuliwa mwenye sifa zisizotambuliwa na sheria au katiba, hiyo haizuii watu kuhoji baadhi ya sifa walizonazo wateuliwa hadi wawe wateule kwa nafasi zao.

Na wala sijaona mtu akihoji humu JF uhalali wa wateuliwa kuhusiana na matakwa ya katiba au sheria. Wewe umeona bandiko lolote linalohoji juu ya hilo?

Katiba haitamki kila jambo na wala haizuii kutumia akili kufanya jambo lisilokatazwa na katiba au sheria.
 
Katiba na sheria kutotamka mambo mengi sana ambayo ni muhimu katika kuongoza nchi nalo ni tatizo kubwa sana.Kwa namna hiyo kila mtu anaweza kufanya vile anvyofikiri ni vyema na akawa sahihi.
Hapana.

Katiba haitakiwi iseme kila kitu; katiba ya namna hiyo haipo duniani, hata misahafu nayo haisemi kila kitu

Katiba inaweka mambo ya msingi, ambayo ndiyo sheria kanuni na taratibu nyingine huelezea kwa upana wake, na inapotokea mkanganyiko wa utafsiri wa sheria zinazotungwa kukinzana na katiba, hapo ndio huwepo Mahakama ya Katiba kufafanua lengo la katiba katika eneo hilo la mkanganyiko lilikuwa ni lipi.

Hata hiyo haitoshi, bado kutakuwa na mambo chungu nzima yasiyoainishwa sehemu yoyote, lakini yanafanywa kwa kutumia 'common sense'.

Katika uteuzi wa viongozi kwa mfano, pamoja na katiba kutozuia yeyote mwenye sifa asipewe uongozi, lakini litakuwa ni jambo la ajabu sana kwa kiongozi mwenye akili za kuvukia barabara pekee apewe uongozi na wananchi au mteuzi, eti kwa vile katiba haizuii mtu huyo kuwa kiongozi.
 
Wakoloni walikuwa na common sense yao wakaweka utaratibu wa kuwapatia mafunzo maalumu ya muda mrefu watu waliokuwa wanawaanda kuja kuwa watumishi katika koloni lao, sisi pia tunaweza kuiga utaratibu huo au tukazifanya nafasi nyingi zaidi za uongozi ni za kuchaguliwa, au nafasi zote muhimu za kuchaguliwa ziridhiwe na kamati maalum ya bunge.

Vinginevyo kila mtu ana common sense yake ndio maana wakati wewe unalaumu na kulaani kuna wengine wanashangilia na kudemka.

Yaani huna shaka na uongozi wa juu lakini una mashaka na wanaoteuliwa na uongozi wa juu! Hii ni fallace labda ufafanue hapa.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Wakoloni walikuwa na common sense yao wakaweka utaratibu wa kuwapatia mafunzo maalumu ya muda mrefu watu waliokuwa wanawaanda kuja kuwa watumishi katika koloni lao, sisi pia tunaweza kuiga utaratibu huo au tukazifanya nafasi nyingi zaidi za uongozi ni za kuchaguliwa, au nafasi zote muhimu za kuchaguliwa ziridhiwe na kamati maalum ya bunge.

Vinginevyo kila mtu ana common sense yake ndio maana wakati wewe unalaumu na kulaani kuna wengine wanashangilia na kudemka.
Ninakubaliana na sehemu kubwa ya andiko lao, hasa kuhusu wakoloni. Lakini usisahau, hapa hapa nasi tumekuwa na utaratibu huo kwa muda mrefu hadi ulipokuja kuvurugwa, sababu sizijui.

.Chuo cha Kivukoni na vyuo kadhaa hapa nchini hiyo ndiyo kazi iliyokuwa vikiifanya. Kwa hiyo utaratibu huo sio mgeni, ulikuwepo.

Kuhusu huo mstari wako wa mwisho, sina haja ya kuujibu, kwa sababu inaonyesha umeuweka tu kuendeleza mjadala, huku ukijuwa hauna maana yoyote.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom