Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,679
- 149,864
Habari wadau,
Kama ilivyo kwa Majaji na Majeshi kutoruhusiwa kujihusisha na siasa kutokana na nature ya kazi, vile vile kuna umuhimu wa kuwa na sheria kama hii kwa waandishi wa habari kwani hata nao kwa nature ya kazi yao,wanaweza kutumika/kufanya kazi zao bila kuzingatia maadili ya Taaluma yao ili tu kumfurahisha kiongozi fulani serikalini kwa matumaini ya kupata nafasi fulani ya uteuzi kama vile Ukuu wa Wilaya, n.k.
Tuwe na sheria ambayo itaruhusu mwanahabari kuteuliwa kushika nafasi yoyote ile kama tu atakuwa ametimizi muda wa angalau miaka miwili au mitatu tangu aache au kustaafu kujihusisha na kazi ya uandishi wa habari katika chombo chochote kile.
Nasema hivi kwasababu kuna uwezekano mkubwa kuwa baadhi ya waandishi wanatumia kalamu au camera zao vibaya wakitegemea kulipwa fadhila fulani au hata kwa kuahidiwa vyeo fulani fulani na hivyo kupotosha umma na wakati mwingine hata huchangia kupatikana kwa viongozi wabovu.
Waandishi wawe eligible kwa nafasi zingine za utumishi wa umma ambazo zitahusisha kufanyiwaa interview lakini si nafasi za uteuzi wa moja kwa moja.
Sheria hii pia ihusishe Waamiliki wa Vyombo vya Habari kwani hawa huenda wakawa ni hatari kuliko hata Waandishi wenyewe.Mnaposikia mmiliki wa chombo fulani cha habari anatakiwa kulipwa fadhila,basi ni lazima mujiulize mara mbilimbili kama chombo chake kilizingatia maadili ya utangazaji.
Tunapoambiwa fani ya habari ni muhimili mmoja wapo wa dola,inatubidi tuwe makini sana na muhimili huu kama ilivyo kwa mhimili wa Mahakama ambao Majaji wake hawaruhusiwi kujihusisha na shughuli za kisiasa.
Tunaweza kuwa ni nchi ya kwanza duniani kuwa na sheria ya aina hii ila naamini tulipofika tunahitaji kuwa na sheria ya aina hii au inayofanana na hii