Tuwe na sauti moja ya kudai Tume Huru ya Uchaguzi

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Ndugu watanzania na wazanzibari muliopo ndani na nje ya nchi.

Tumeona jitihada za viongozi wa upinzani ukidai tume huru ya uchaguzi, Sisi tunaona tume ya uchaguzi hata ikiwa huru kuna mifumo mengine inaweza kuingilia tume, kuiteka tume kama ilivyo fanyika Zanzibar Oct 2015

Badala ya kwenda kwenye tume huru, twende kwenye katiba mpya, katiba tulio nayo ni ya mfumo wa chama kimoja, katiba mpya ni muhimu kuliko uchaguzi mkuu.

Katiba ya sasa inabinya haki za binadamu, kisiasa na kijamii, pia mfumo hata wa muungano haupo usawa na una mapungufu toka kuasisiwa.

Tuwe na one voice

Vyama vya siasa, NGOs na Human rights na wananchi tuungane pamoja, tutumie kila njia kufikisha ujumbe na waelewesha wananchi maudhui ya kudai katiba mpya na kuweka kipao mbele kuliko hata chaguzi.

Naamini kama tukiwa na sauti moja na kuondoa maslahi ya kisiasa na kuweka maslahi ya taifa zima, tutashinda kwa hili.

Katiba mpya ndio nguzo muhimu kwa mahitaji ya leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Wazanzibari waungeni mkono wanaodai Tume huru.

..hata isipopatikana mtakuwa mmepata marafiki wa kuwaunga mkono ktk madai yenu ya katiba mpya.

..ni muhimu sana kwa Wazanzibari kuwa sehemu ya harakati zinazoendelea huku Tanganyika.
 
swadakta !
 
Huwezi kusema upo huru wakati upo jela, eti kwa sababu tu huna pingu mkononi, huwezi kusema upo huru wakati una kifungo cha nje, kuwa na tume huru kwa katiba tulio nayo ni sawa kuwa kifungo cha nje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nauliza tu Kama katiba ni Mali ya watanzania,wananchi na katiba ndo inatoa cheo cha rais,inatoa tume ya uchaguzi etc.Hiyo katiba au tume huru mnaidai kwa Nani?Au wananchi wa Tanzania hatujitambui sisi ni akina Nani?
 
Tume huru ni nini?
 
We jamaa una maswali magumu
 
Tume huru ni nini?
Mkuu Mimi sio mtaalamu wa kiswahili Ila nadhani tume huru ni chombo huru chenye kinga na mamlaka ya kufanya kazi na maamuzi bila kuingiliwa na mtu Wala taasisi yoyote na wajunbe wake wanspatikana kwa njia huru huku sifa za kuwania nafasi ama ya kuteuliwa au kuajiriwa na tume hiyo zikiwa wazi na mtu yeyote ambaye ni mtanzania mwenye sifa akiwa na uwezo either kuteuliwa au kuajiriwa na tume hiyo.for more details consult your kamusi ya kiswahili about neno huru
 
Ndugu watanzania na wazanzibari muliopo ndani na nje ya nchi.

Tumeona jitihada za viongozi wa upinzani ukidai tume huru ya uchaguzi, Sisi tunaona tume ya uchaguzi hata ikiwa huru kuna mifumo mengine inaweza kuingilia tume, kuiteka tume kama ilivyo fanyika Zanzibar Oct 2015

Badala ya kwenda kwenye tume huru, twende kwenye katiba mpya, katiba tulio nayo ni ya mfumo wa chama kimoja, katiba mpya ni muhimu kuliko uchaguzi mkuu.

Katiba ya sasa inabinya haki za binadamu, kisiasa na kijamii, pia mfumo hata wa muungano haupo usawa na una mapungufu toka kuasisiwa.

Tuwe na one voice

Vyama vya siasa, NGOs na Human rights na wananchi tuungane pamoja, tutumie kila njia kufikisha ujumbe na waelewesha wananchi maudhui ya kudai katiba mpya na kuweka kipao mbele kuliko hata chaguzi.

Naamini kama tukiwa na sauti moja na kuondoa maslahi ya kisiasa na kuweka maslahi ya taifa zima, tutashinda kwa hili.

Katiba mpya ndio nguzo muhimu kwa mahitaji ya leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili suala lilishafikishwa katika vyombo vya kutafasiri sheria na kutoa haki. Chombo cha mwisho chenye maamuzi ya kutoa haki na kutafasiri sheria ni Mahakama ya rufaa. Ilitoa hukumu kuwa tume ya uchaguzi (NEC) ipo huru na inafanya kazi kwa mujibu wa Katiba na sheria.
Hao Wakurugenzi mnaohofia watapendelea CCM huwa wanakula kiapo kwa mujibu wa sheria ili wafanye kazi kwa uhuru bila upendeleo.
Kila chama kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi kinaweka mawakala kwa ngazi zote ili kuhakikisha hakuna dhuluma.
Ninachoona Chadema wameshindwa uchaguzi hata kabla ya filimbi kupulizwa.Na kwa mantiki hii bora hata msipoteze pesa kuweka wagombea.
 
Back
Top Bottom