Tuwe makini tusiwe kama Wanigeria!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
Watanzania ibabidi tuwe makini sana. Badala ya kuiga kila kitu kutoka nchi nyingine tuangalie kwanza je nchi yetu ikoje na miaka 20 ijayo itakuwaje.

1. Tanzania ya sasa 66% ya Watanzania wana miaka chini ya 24!.
2. Tuna ajenda za Maendeleo lakini hatuna agena kubwa ya kulenga hawa vijana na watoto
3. Mfumo wa elimu umepitwa na wakati
4. Watu wengi wanakimbilia mijini

Wasiwasi wangu ni matabaka makubwa ya Watanzania kutokana na sisi kutokuwa na mikakati na vijana wetu yataleta system tofauti za maisha. Mfano tutaanza kutekana, kuwa na shule zaidi za matajiri na masikini, hospitali za matajiri na masikini, maduka ya matajiri na masikini. Tutazidi kuwa na fensi kubwa kwenye nyumba zetu. Hivyo tutakuwa na nchi ambayo ni nzuri kwa wachache na mzigo kwa wengi kama ilivyo Negeria.

Je tufanyaje kuepusha haya

1. Tubadilishe mfumo wa elimu. Tufundishe zaidi technologia kwenye shule ili tuongeze ubunifu na ushindani kwa watoto wetu huko mbele mfano Form 5 and 6 zinaweza kuwa muda wa kusoma kitu ambacho unaweza kutumia programming, software applications, technicians kwenye gas, oil n.k badala ya kusoma mpaka form 6 halafu huna skills zozote za kutumia kwenye maisha au kazi

2. Tuangalie jamani mfumo ya bank. Hatutaweza kuendelea kama mfumo wa bank hausaidii biashara ndogondogo kukua. Sababu mojawapo ni kwamba mfumo wetu ni wa mtaji sasa kama mikopo haipatikani na ikipatikana ni 20% riba hatutaweza kushindana.

3. Tubadilishe mfumo wa Afya kutoka kuuguza na kutibu kwenda kwenye kupunguza magojwa na kuzuia magojwa. Mfano nchi yetu ni ya vijana na magojwa mengi yanayo gharimu yanatokana na kisukari na moyo. Haya magojwa yote yanaweza kupunguzwa kwa elimu kama kufanya mazoezi, vyakula na kupima afya. Badala ya kuwa na vituo vya afya pekee kungekuwepo na team za Dr, Nurse ambao wanazunguka vijijini kutoa huduma na elimu , chanjo n.k. Yaani siku hizi kuna mpaka CT za mobile, vipimo vya sukari vya betri au hata solar vipo. Vilevile serikali inatakiwa kuweka sheria wazi ili tuweze kusaidia nchi tuungane na universities mbalimbali duniani madoctor na kuwe na uwazi wa kodi ili tuweze kusaidia vifaa badala ya kuleta vitu halafu vipigwe minada.

4. Tuweke sera kila mtanzania awe na skill fulani badala ya kuwa na vijana wengi wababaishaji. Kama ilivyokuwa lazima kwenye JKT kwa mwaka iwe lazima kila mtu awe mtaalamu wa kitu fulani kwasababu kama mtu hachangii kwenye uchumi ina maana sisi ndiyo tunampa lishe

Wanasiasa wenzetu angalieni #3 nilituma hii message muda lakini hilo bado ni muhimu.
Zitto ,Mwigulu Nchemba
 
Pigania usalama wako kwanza Mkuu.

Jiwe hana muda mchafu huo, yuko busy kuchuma yeye na GENGE lake la kina BASHITE, TULIA, MABEYO, DOTTO JAMES, KIJAZI, MNYETI
 
Watanzania ibabidi tuwe makini sana. Badala ya kuiga kila kitu kutoka nchi nyingine tuangalie kwanza je nchi yetu ikoje na miaka 20 ijayo itakuwaje.

1. Tanzania ya sasa 66% ya Watanzania wana miaka chini ya 24!.
2. Tuna ajenda za Maendeleo lakini hatuna agena kubwa ya kulenga hawa vijana na watoto
3. Mfumo wa elimu umepitwa na wakati
4. Watu wengi wanakimbilia mijini

Wasiwasi wangu ni matabaka makubwa ya Watanzania kutokana na sisi kutokuwa na mikakati na vijana wetu yataleta system tofauti za maisha. Mfano tutaanza kutekana, kuwa na shule zaidi za matajiri na masikini, hospitali za matajiri na masikini, maduka ya matajiri na masikini. Tutazidi kuwa na fensi kubwa kwenye nyumba zetu. Hivyo tutakuwa na nchi ambayo ni nzuri kwa wachache na mzigo kwa wengi kama ilivyo Negeria.

Je tufanyaje kuepusha haya

1. Tubadilishe mfumo wa elimu. Tufundishe zaidi technologia kwenye shule ili tuongeze ubunifu na ushindani kwa watoto wetu huko mbele mfano Form 5 and 6 zinaweza kuwa muda wa kusoma kitu ambacho unaweza kutumia programming, software applications, technicians kwenye gas, oil n.k badala ya kusoma mpaka form 6 halafu huna skills zozote za kutumia kwenye maisha au kazi

2. Tuangalie jamani mfumo ya bank. Hatutaweza kuendelea kama mfumo wa bank hausaidii biashara ndogondogo kukua. Sababu mojawapo ni kwamba mfumo wetu ni wa mtaji sasa kama mikopo haipatikani na ikipatikana ni 20% riba hatutaweza kushindana.

3. Tubadilishe mfumo wa Afya kutoka kuuguza na kutibu kwenda kwenye kupunguza magojwa na kuzuia magojwa. Mfano nchi yetu ni ya vijana na magojwa mengi yanayo gharimu yanatokana na kisukari na moyo. Haya magojwa yote yanaweza kupunguzwa kwa elimu kama kufanya mazoezi, vyakula na kupima afya. Badala ya kuwa na vituo vya afya pekee kungekuwepo na team za Dr, Nurse ambao wanazunguka vijijini kutoa huduma na elimu , chanjo n.k. Yaani siku hizi kuna mpaka CT za mobile, vipimo vya sukari vya betri au hata solar vipo. Vilevile serikali inatakiwa kuweka sheria wazi ili tuweze kusaidia nchi tuungane na universities mbalimbali duniani madoctor na kuwe na uwazi wa kodi ili tuweze kusaidia vifaa badala ya kuleta vitu halafu vipigwe minada.

4. Tuweke sera kila mtanzania awe na skill fulani badala ya kuwa na vijana wengi wababaishaji. Kama ilivyokuwa lazima kwenye JKT kwa mwaka iwe lazima kila mtu awe mtaalamu wa kitu fulani kwasababu kama mtu hachangii kwenye uchumi ina maana sisi ndiyo tunampa lishe
Mbona "it's too late" matabaka yapo tena "income inequality yetu" ni kubwa kuliko ya Nigeria kuna shule za wenye uwezo ambazo masikini hata mkichanga uko mzima hamwezi kusomesha mtoto japo mwaka mmoja shule kama Feza Tangankia ada ni 25m.....hospitali niyaleyale hospitali ya Mwananyamala wakinamama wanao taka kujifungua wanakaa wanne wanne kitanda kimoja wengine wanalala chini wakati hospitali ya ocean Rd kila mjamzito ana chumba chake.....wewe unaongelea Tz ipi?
 
Watanzania ibabidi tuwe makini sana. Badala ya kuiga kila kitu kutoka nchi nyingine tuangalie kwanza je nchi yetu ikoje na miaka 20 ijayo itakuwaje.

1. Tanzania ya sasa 66% ya Watanzania wana miaka chini ya 24!.
2. Tuna ajenda za Maendeleo lakini hatuna agena kubwa ya kulenga hawa vijana na watoto
3. Mfumo wa elimu umepitwa na wakati
4. Watu wengi wanakimbilia mijini

Wasiwasi wangu ni matabaka makubwa ya Watanzania kutokana na sisi kutokuwa na mikakati na vijana wetu yataleta system tofauti za maisha. Mfano tutaanza kutekana, kuwa na shule zaidi za matajiri na masikini, hospitali za matajiri na masikini, maduka ya matajiri na masikini. Tutazidi kuwa na fensi kubwa kwenye nyumba zetu. Hivyo tutakuwa na nchi ambayo ni nzuri kwa wachache na mzigo kwa wengi kama ilivyo Negeria.

Je tufanyaje kuepusha haya

1. Tubadilishe mfumo wa elimu. Tufundishe zaidi technologia kwenye shule ili tuongeze ubunifu na ushindani kwa watoto wetu huko mbele mfano Form 5 and 6 zinaweza kuwa muda wa kusoma kitu ambacho unaweza kutumia programming, software applications, technicians kwenye gas, oil n.k badala ya kusoma mpaka form 6 halafu huna skills zozote za kutumia kwenye maisha au kazi

2. Tuangalie jamani mfumo ya bank. Hatutaweza kuendelea kama mfumo wa bank hausaidii biashara ndogondogo kukua. Sababu mojawapo ni kwamba mfumo wetu ni wa mtaji sasa kama mikopo haipatikani na ikipatikana ni 20% riba hatutaweza kushindana.

3. Tubadilishe mfumo wa Afya kutoka kuuguza na kutibu kwenda kwenye kupunguza magojwa na kuzuia magojwa. Mfano nchi yetu ni ya vijana na magojwa mengi yanayo gharimu yanatokana na kisukari na moyo. Haya magojwa yote yanaweza kupunguzwa kwa elimu kama kufanya mazoezi, vyakula na kupima afya. Badala ya kuwa na vituo vya afya pekee kungekuwepo na team za Dr, Nurse ambao wanazunguka vijijini kutoa huduma na elimu , chanjo n.k. Yaani siku hizi kuna mpaka CT za mobile, vipimo vya sukari vya betri au hata solar vipo. Vilevile serikali inatakiwa kuweka sheria wazi ili tuweze kusaidia nchi tuungane na universities mbalimbali duniani madoctor na kuwe na uwazi wa kodi ili tuweze kusaidia vifaa badala ya kuleta vitu halafu vipigwe minada.

4. Tuweke sera kila mtanzania awe na skill fulani badala ya kuwa na vijana wengi wababaishaji. Kama ilivyokuwa lazima kwenye JKT kwa mwaka iwe lazima kila mtu awe mtaalamu wa kitu fulani kwasababu kama mtu hachangii kwenye uchumi ina maana sisi ndiyo tunampa lishe

Wamechukuwa miaka 4 lakini naona sasa wanaanza kunielewa!
 
Back
Top Bottom