Tuwe makini tunaposafiri na mabasi

Korogwe au Mombo au Tanga au Dar sio maudhui yaliyolengwa.

Kwa hali hii hata ingekuwa USA River kwenda Mbamba Bay bado angewamwaga.

Mitungi haipimwi kwa kijasho chembamba, si jukumu wala uwezo wa abiria kuchunguza na kujua hali ya dereva.

Serikali inatakiwa iwe na drug and alcohol program kwa madereva wote wa vyombo vya biashara.
 
Hapo kwenye chupa kubwa ya maji ndipo mmeachwa solemba, inaonesha alimaanisha ndani ya chupa ile ya maji kulikuwa na maji yaliyowekwa kilevi na ndio sababu ya dereva kushindwa kulimudu gari na kusababisha ajali, hivyo anawata abiria wawe wanaoona dereva na chupa la maji yenye kilevi wawe huru kusema hapana, kwamba, hawawezi kuendelea na safari hiyo hata kama wametoa pesa.
 
Ni kweli unachosema kwa sababu always huwa sieleweki hata kwenye life style mkuu.. Soon nategemea kuwa kioo cha jamii hivyo ipo siku tutashare kichwa na wewe kufikia lengo, japo kwa sasa uwezo unao, ila hujaamua kwa sababu hujajua umuhimu wake.. Ntakuwa njia ya Watanzani.. Binafsi ni Nabii wa kwanza Mwaafrika.
umeanza vizuri lakini hapo mwishoni umeharibu!!!
 
Ni kweli unachosema kwa sababu always huwa sieleweki hata kwenye life style mkuu.. Soon nategemea kuwa kioo cha jamii hivyo ipo siku tutashare kichwa na wewe kufikia lengo, japo kwa sasa uwezo unao, ila hujaamua kwa sababu hujajua umuhimu wake.. Ntakuwa njia ya Watanzani.. Binafsi ni Nabii wa kwanza Mwaafrika.
Ha ha ha ha ha
 
Ni wachache sana wamekuelewa na ni wachache watakaokuelewa. Akili za wabongo wanataka watafuniwe kila kitu wao wameze then uwakumbushe kwenda chooni na ikiwezekana uwaoneshe hata choo kilipo na namna ya kukitumia.
 
Nilivyomuelewa mimi dereva kaenda kona karudi na chupa kubwa la maji huku kijasho chembamba kikimtoka ndani ya chupa ya maji kulikuwa na kilevi ndo hitimisho la yote
Hapa naanza kuelewa,kuna madereva wanaweka Konyagi kwenye chupa za maji ya Kilimanjaro,wewe unaona kama anakunywa maji kumbe Konyagi, Mostly madereva wa gari za mizigo wanaosafiri usiku. Kwa mng'ao wa maji ya Kilimanjaro na mng'ao wa Konyagi huwezi kutofautisha. Nadhani ndicho anachotaka kutuambia mtoa mada kuhusu huyo dereva aliyesababisha ajali.
 
Kooote huko haikuwa lazima kufika! Swali lakumuuliza mtoa mada ni je, anataka abiria a/wafanye nini wakiona dereva ana chupa ya maji na labda anatoka kijasho chembamba?

Ni ngumu kwa abiria kutambua kama dereva ametumia au anatumia kilevi kilichopo ndani ya chupa ya maji na wasingeweza kuchukua hatua yoyote kwa wakati ule. Lakini inapotokea abiria wachache wakakaemea uzembe wa wazi wa dereva mara nyingi hawapati ushirikiano wa abiria wote waliopo kwenye chombo hicho cha usafiri. Abiria wengine hawana uthubutu wa kukemea madereva wanapoendesha kizembe majanga yanatokea wau wanajuta kwa nini hawakuchukua hatua.
 
anamaanisha dereva kwenye chupa ya. Kilimanjaro alikua ameweka kilevi na sio maji, kwa nini atoke jasho jembamba na huku anakunywa maji.. atakuwa aliweka konyagi/ viroba
 
Ni ngumu kwa abiria kutambua kama dereva ametumia au anatumia kilevi kilichopo ndani ya chupa ya maji na wasingeweza kuchukua hatua yoyote kwa wakati ule. Lakini inapotokea abiria wachache wakakaemea uzembe wa wazi wa dereva mara nyingi hawapati ushirikiano wa abiria wote waliopo kwenye chombo hicho cha usafiri. Abiria wengine hawana uthubutu wa kukemea madereva wanapoendesha kizembe majanga yanatokea wau wanajuta kwa nini hawakuchukua hatua.

Wahusika wanaposhindwa wajibu kwao husingizia abiria. Hivi watu waliokutana kwenye basi mnataka wagombane na dereva ili iweje? Umewakabidhi wanao kwa mama wa kambo halafu akiwanyanyasa unawalaumu watoto?
 
Eti dereva katoka Dar vizuri kwenda Tanga, kafika Korogwe kwenye chakula, kawapa muda wa kula abiria dakika kumi.

Abiria wote wameenda na muda, kasoro Dereva. Mara katokea na chupa kubwa ya maji ya kilimanjaro.. Jasho jepesi usoni.. Halafu unakuta mtu unamuona na bado unakuwa na amani, kweli kabisa mtu na akili zako unatulia kabisa..

Matokeo yake kaua mwendesha baiskeli na basi kupinduka. Watu watatu hapo hapo.. Wawili hospitalini.. Jumla watano. Majeruhi ndio usiseme.. Duuh!! Kama kweli ni dereva, angemgonga mmoja akaokoa basi, ila bwana Dereva kaangusha basi na mwendesha baiskeli kamgonga.. Duuh Dereva..

N:B Tuwe makini tunapo safiri na mabasi, kuwa huru kwasababu umetoa pesa.. Pesa yako inaisha pindi ukifa tu.
Maelezo ya majeruhi wa ajali ya jana Tanga.
 
Back
Top Bottom