Tuwe makini sana na watu wanaojiita 'Motivational Speakers' hasa wanapojinasibu kuzungumzia masuala ya ujasiliamali na kujiajiri

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Hawa wazungumzaji /motivational speakers huwa wanawapotosha sana vijana wetu , hasa graduates toka vyuo mbali mbali.

Unakuta wanawakusanya vijana wetu pengine wanawachangisha mpaka viingilio halafu wanaenda kuwamezesha 'nondo' walizodownload kwenye mitandao, bila wao wenyewe kuwa na uhalisia ama utekelezaji wa wanachokizungumzia.

Hawanaga mifano halisi ya wao wenyewe kama wamepractise hicho wanachokiongelea. Hawanaga mifano halisi.

Unakuta wamepiga pamba utafikiri wana projects au wamejiajiri. Hewa kabisa.

Wanazungumzia vitu kwa nadharia tu.

Tuwateme. Hovyo sana.
 
Sasa kwa faida ya vijana ungewataja..huu uzi bila majina ni mchuzi usio na nyama.
 
Mfano halisi ni yeye uwezo wake wa kukusanya ao vijana na kuwalipisha kingilio na yeye kujiongezea kipato. Kwan kaiba?
 
Hahaha mbona wanasiasa wanafanya hayohayo, waache vijana wafundishwe ujasiliamali.
 
Motivatinal Speakers waache wafanye kazi yao, kwanini?
Ndugu zangu kuongea mbele ya watu hadi wakakusikiliza na kukupigia makofi nacho ni kipaji..sio kila mtu anaweza..Hao motivational speakers wapo ulimwengu mzima wala sio tz peke yake..ngoja niishie hapo.
 
Hawa wazungumzaji /motivational speakers huwa wanawapotosha sana vijana wetu , hasa graduates toka vyuo mbali mbali.

Unakuta wanawakusanya vijana wetu pengine wanawachangisha mpaka viingilio halafu wanaenda kuwamezesha 'nondo' walizodownload kwenye mitandao, bila wao wenyewe kuwa na uhalisia ama utekelezaji wa wanachokizungumzia.

Hawanaga mifano halisi ya wao wenyewe kama wamepractise hicho wanachokiongelea. Hawanaga mifano halisi.

Unakuta wamepiga pamba utafikiri wana projects au wamejiajiri. Hewa kabisa.

Wanazungumzia vitu kwa nadharia tu.

Tuwateme. Hovyo sana.
mungu ndo anatoa riziki sio hao.mimi mtu akiniambia nikupe siri ya kufanikiwa sijui na kitabu jinsi ya kufanikiwa.sijui namuonaje.akili yangu ndio uwezo wangu wakupambana na riziki toka kwa mwenyezi mungu
 
Unachoshindwa kuelewa ni kuwa

Hao motivation speaker wamejiajiri kwa kutumia midomo yao

Au umekariri kujiajiri mpaka ufungue genge la kuuza nyanya?
 
Ukiona unaitiwa fursa jua wewe Ndiyo fursa
Acha waliwe tuu
Kesh kuna wajinga nimewaita niwafundishe ufugaji wa kuku na samaki lakin mimi sina vyote hivo
Kiingilio tsh 8000 tuu
Wamejiandikisha 113 nimewapanga kwenye section tatu masaa Mawil Mawil nakusanya vyangu nalipia eneo nasepa mjini ni akili tuu
Jion naingia You tube na download video za kesho nasoma bas wanasema huyo Ndiyo mtaalam sasa kumbe najua mwenyewe
Halafu wananikubali kinoma
 
Mimi naona hao motivational speakers hasa hawa tulionao katika haya mazingira ya nchi zetu masikini ni kuwachukulia kama walimu wa shule za msingi ambao siku zote watawahimiza wanafunzi wao wasome kwa bidii ili wafike mbali japo wao hawakufika huko wanakowahimiza wanafunzi wao wafike. Wanafunzi wao wakiwasikiliza kweli watafika mbali. Ukweli ni kwamba hao motivational speakers wana nafasi kubwa na muhimu sana katika kuwa shape wanajamii ili kubadilika na kuhamasika kuboresha maisha yao. Hivyo tusijikite sana kwenye kuwabeza kila siku.
 
Hahahaha kam kuba moja juzi kati nilikutananaye maeneo ya stend kavaa ndala na nguo zmechookaaa ..kumcheki kwa makini nikakumbuka miaka mbili nyuma niliwah mwona maeneo ya New Arusha Hotel akiwa nadhifu na suti kali akimotivate vijana kuhusu forever living ..

Mzeee, ilikuwa bado kidogo nijiunge na izo maforever maana jamaa alikuwa anongea kiasi kwamba mtu ukisikia utatamani ujiunge muda huo huo.

Nakumbuka vijana weng sana waliingia sa cjui saiv wako na hali gani uko. Na kama mim ningekuwa na cash siku ile ile ningeshajiunga. Nashukuru Mungu skuwa na cash.

Ila hawa Motivational speakers huwa waongo kweli kweli...itabidi wawe wanachnguzwa kwanza kabla ya kutoa izo motivesheni zaoo...
 
Aisee kweli jamaa Ni wasanii Kuna MMOJA aliwahi TOA semina ya ifugsni wa sungura akaninasibu wee,Sasa ilikuonesha yet kafanikiwa kutokana na masungura akaanza kuuliza Nani anasungura Nina hitaji Mia 2,3,-5 nikanyoosha mkono na kusema ninao 250 hybrid tukapeana namba za simu Ila baada ya semina namba hazipatikani Hadi leo hiii
 
Unapoambiwa mambo ya fursa fursa kuwa millionaire kwa mtaji wa laki 1 basi jua wewe ndiyo fursa yenyewe
Ndio hivyo mjini mnazidiana ujanja kidogo, ukipiga unafurahi ukipigwa unatafuta wakumpiga life inaenda, sasa mkiwaharibia hao nao watakosa ajira, maana wao ni wajasiliamali pia. mlitakiwa muwa support nao wa survive.
 
Back
Top Bottom