Tuwe Makini na Watu Tunaowasaidia, Itatugharimu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwe Makini na Watu Tunaowasaidia, Itatugharimu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Wabogojo, Sep 18, 2012.

 1. Wabogojo

  Wabogojo JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  FYI
  Nimetumiwa na rafiki yangu leo hii.

  Mzee Mbene  JUMAPILI ILIYOPITA MJOMBA WANGU ALIKUWA KWENYE DALADALA AKITOKEA UBUNGO KWENDA TEGETA.BASI LILIPOFIKA MWENGE ABIRIA WALIONGEZEKA NA WENGINE WAKAWA WAMESIMAMA, KATI YA WALIOSIMAMA ALIKUWAPO MZEE MMOJA ALIYEKUWA NA HAND BAG KAMA TUNAZOBEBEA LAPTOP HIVI, YULE MZEE ALIMUOMBA MJOMBA WANGU AMSAIDIE KUMSHIKIA BAG LAKE KWAKUWA YEYE ALIKOSA SITI, BILA YA KUSITA AKAAMUA KUMSAIDIA KALE KA BAG"BAADA YA VITUO VIWILI YULE JAMAA MWENYE KA BAG; ALITEREMKA BILA MJOMBA WANGU KUMUONA NA YEYE HAKUWA NA WASIWASI KWA KUWA ALIJUA MWENYE MZIGO AKITAKA KUSHUKA ATAUCHUKUA TU MZIGO WAKE.

  KABLA GARI HAIJAFIKA KITUO CHA TATU ILISIMAMISHWA NA WATU WALIOJITAMBULISHA KWAMBA WAO NI ASKARI POLISI WAPELELEZI KWAMBA KUNA KITU WANAPELELEZA,WAKAWAAMURU ABIRIA WOTE WATEREMKE KWENYE GARI,WALIFANYA HIVYO NA MMOJA WA WALE POLISI, ALIMFUATA MJOMBA WANGU NA KUMUULIZA 'NA WEWE KWENYE BAG LAKO KUNA NINI? AKAWAJIBU BAGI SIYO LANGU KWA HIYO SIWEZI JUA NDANI KUNA NINI!! WAKAMUULIZA TENA, MWENYEWE YUKO WAPI TUONESHE" AKAANGALIA KATI YA WALEA BIRIA WENZAKE HAKUMUONA.


  WAKASEMA FUNGUA TUONE KUNA NINI NDANI, WALIPOFUNGUA WAKAKUTA KUNA SILAHA AINA YA PISTO.ALIPOJARIBU KUJITETEA WAKAMWAMBIA TWENDE KITUONI UTAENDA KUJIELEZA HUKO. BASI LIKARUHUSIWA NA YEYE WAKAMPELEKA POLISI, WAKIWA NJIANI WAKAMWAMBIA KAMA ANATAKA WAMWACHIE ATOE LAKI NANE 800,000/= VINGINEVYO WATAMUUNGANISHAKATIKA KESI YA WIZI WA KUTUMIA SILAHA,AKAWAAMBIA SINA HIZO PESA NA SIWEZI KUTOA .MPAKA SASA BADO YUPO NDANI.HII INATUKUMBUSHA KWAMBA NI KWELI TUNAPENDA KUWASAIDIA WATU ILA TUWE MAKINI NA MISAADA TUNAYOITOA.


  MZEE ALIKUWA NA NIA NJEMA KABISA YA KUTOA MSAADA ILA MSAADA UMEMGHARIMU MAISHA.

  My Take: Napenda kuwatahadharisha watu wote tuwe makini na watu tusiowajua, itatugharimu ndugu zangu.
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 969
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni kweli ni tahadhari nzuri.
   
 3. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 7,814
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Asante kwa tahadhari hiyo ya ukweli ndugu ila umenichosa sana kwa kutumia herufi kubwa. Kwa nini herufi kubwa?
   
 4. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Nikweli inabidi tuwe makini sasa pamoja na kuwa watanzania ni watu wanaopenda kusaidia. Imefika wakati mambo yamebadilika si kama zamani, imani na uaminifu kwishney kabisa. Huko tunakoelekea tutashauriana tusisaidie tusiyemjua.
   
 5. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,073
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 145
  kuna siku nakumbuka miaka 4 nyuma,ilikuwa stend pale posta mpya muda wa jioni watu kurudi nyumban,wakat,kuna kijana alikuwa anasubiri usafiri,mara akatokea mama mtu mzima,akamuomba simu aweke line awapigie ndugu zake,yule kijana akampatia simu yule mama akatoa line ya jamaa na kuweka yake,baada ya kuongea yule mama akajifanya kama anarudisha line ya jamaa kumbe akufanya hivo,bus la mwenge lilivyokuja wote wakaingia,mara yule mama akaanza kulalamika kaibiwa simu,basi watu fasta wakasema mama atoe namba ya simu wapige kabla mwiz ajaizima,watu kupiga namba ikaitia kwa simu ya jamaa,wabongo bila kupata habari kamili,wakampokonya simu na kumpa yule mama,na kuanza kumshushia kipigo,yule mama akateremka fasta akapotea,jamaa adi anajieleza yule mama alikuwa ameondoka na jaa ashapigwa
   
 6. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145

  dah mkuu hiyo kiboko, very sad. Ndio maana hata mtu akiwa na shida ya kweli hasaidiwi kisa wapumbavu wachache kama hao.
   
 7. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,081
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  dunia tunayoishi sasa sio ya urafiki na undugu ni kuwa makini na kila mnayemwona. hili ndio la msingi. siku hizi hata ombaomba unaogopa kuwasaidia maana wengine wanga wana chuma ulete yani duniani sio sehemu rafiki tena.
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,777
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kweli Mkuu.
  Manake siku hizi ni bora ukajiepusha na kusaidia kuliko kufanywa Mbuzi wa Kafara..
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,240
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Ndo maana nimeamua kuwa Bandidu sitoi lifti au msaada kwa nisiyemfahamu ata awe na matatizo gani!
  Kama msaada niatautoa kanisani au msikitini
  Kuna jamaa alimpa mtu lifti si jamaa akashuka na simu si unajua gari ya home vitu huwa shaghala bagala!
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,083
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mkuu usinikumbushe hii nilipoteza BB yangu mpya kisa kumpa jamaa lifti aise
  Mpaka leo sitamani kufanya hiyo kitu aise
   
 11. M

  Mr Mayunga JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  point taken,umetukumbusha swala la msingi sana.
   
 12. che wa Tz

  che wa Tz JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wambuzi forever........hakuna muda wa kuchekeana
   
 13. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 888
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Siku hizi hakuna kuplay role of a good samaritan,,watu hawaaminiki,ila hao waliosimamisha gari na kujiita polisi ukute fake hao wapigaji tu wa mjini
   
 14. ram

  ram JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 5,880
  Likes Received: 578
  Trophy Points: 280
  Dunia ya sasa ni yakujiamini wewe mwenyewe tu
   
 15. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,587
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Tunakoenda ni kugumu zaidi.
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo manake hilo dili lilisukwa na polisi na huyo kibabu
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,517
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sasa kwa njia hii mbona watu watakuwa hawatoi misaada.
  Na ile ya ombaomba wa salenda iliishiaje?
   
 18. Wabogojo

  Wabogojo JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haswaaaaaah, hiyo ndiyo maana yake!
   
 19. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,530
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hao Police nao Hawana jIPYA!! Asiwape Hata senti Tano!! Ila kama Hiyo Hadithi ni ya Ukweli basi hii nchi haina askari wapelelezi ila ina wala Rushwa tu!!
   
 20. nipeukweli

  nipeukweli JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 421
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  msisitizo wa ujumbe...
   
Loading...