Tuwe makini na vinywaji kama soda na bia kwenye chupa

kifuruko

Member
Sep 27, 2011
20
2
hivi karibuni nilitaka kunywa soda aina ya bitter lemon inayotengenezwa na bonite bottlers ltd, kampuni tanzu ya ipp. wakati nataka fungua niliona mdudu mkubwa tena ameanza kuoza! sasa nawauliza wan jf. katika karne ya sayansi na teknolojia, viwanda havina umakini wa kufanyia usafi vyombo kama chupa? huo ni uchafu unaoonekana, je uchafu mdogo! be aware......
 
Ulichukua hatua gani? Au ndo walewale tusiowapenda?ukiulizwa neno SOURCE utakuwa na utetezi wowote?
 
Hujaenda mahakamani bado kuishitaki hiyo kampuni ya bonite na TBS? Umeweka wapi hiyo soda mkuu? Tafadhari tuwasiliane unipe hiyo soda, pengine naweza kupunguza umasikini kupitia hii soda.
 
Tumia kanuni ya kwenye kesi ya Donoghue v. Stevenson kufungua madai ya negligence, na fidia.
 
Soda zote huwa chafu sio bitter lemon pekee.
Hiyo ni kama almasi siku ikiipata fanya party ya kuuaga umaskini
OTIS
 
Ukishafungua tu soda au bia ukikuta ina uchafu ndani huwezi kudai chochote kwasababu iko wazi wanasema unaweza kuwa wewe ndio umeweka huo uchafu!labda ugundue huo uchafu kabla hujafungua chupa.
BTW nyingine ni hujuma tu kutoka kwa washindani
 
bora huyo aliyekuta mdudu mie nilifungua fanta ile nakunywa hivi nikakuta viwembe viwili chini ya chupa ndo hapo sasa ujiulize. Sikuwa na muda nlikuwa busy sana siku hiyo so niikaona hata nikishtaki itakula kwangu tu.
 
kuna mmoja aliwahi leta habari kama hii akasema yeye alikuta kondomu iliyofunguliwa kwenye chupa ya soda. Tuwe makini na hivi vinywaji vya kwenye chupa.
 
Hujaenda mahakamani bado kuishitaki hiyo kampuni ya bonite na TBS? Umeweka wapi hiyo soda mkuu? Tafadhari tuwasiliane unipe hiyo soda, pengine naweza kupunguza umasikini kupitia hii soda.

Hii hapa waliacha kuisafisha kisoda kilikuwa ndani tufanye biashara tafadhali nitafute dili kali!
 

Attachments

  • IMG-20120212-00171.jpg
    IMG-20120212-00171.jpg
    107.6 KB · Views: 70

Similar Discussions

Back
Top Bottom