Tuwe makini na uwekezaji wa "Warehousing and Storage" kwenye mafuta

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,596
8,738
Watanzania ni lazima tuwe makini sana na uwekezaji kwenye uhifadhi wa mafuta. Kwa historia ya Tanzania ni lazima tuelewe ufisadi mkubwa sana kwenye hii nchi unafanyika kwenye sehemu kuu tatu (1) Bandarini na miradi yake (2) Umeme na mambo yote yanayohusu Tanesco (3) Mafuta

Nitaongelea Mafuta. Mafuta ni sehemu ambayo kuna harufu ya rushwa na serikali iwe makini sana maana hii ni sehemu ambayo wafanyabiashara na viongozi wachache serikalini wanashirikiana kuiba.

Sababu mojawapo ya mkurugenzi wa bandari ya Dar-es-salaam kufukuzwa ni kuanzisha mradi wa kuhifadhi mafuta wa kujenga tanks bila kuwa na sababu ya msingi hasa kwa kuzingatia kuna kampuni inaitwa Puma Energy ambayo serikali ina ubia na tank zao zilikuwa na nafasi. Sasa ukijiuliza ni sababu gani hasa bandari ilijiingiza kwenye mradi huu utagundua ni ufisadi mtupu. Kuna makampuni binafsi ambayo yatari yanafanya kazi hii badala ya kutumia pesa kukuza na kurekebisha mambo ya msingi bandarini wakurugenzi wetu walikuwa wanatafuta miradi ya kifisadi hasa kwa kupitia mafuta.

Kwenye safari ya Raisi Samia ya Dubai nimeshtuka kidogo kusikia waziri Makamba akisema kuna kampuni zinakuja kuwekeza kwenye kuhifadhi mafuta. Lakini serikali kwa kupitia Makamba wanajisahaulisha kama vile hakuna kampuni ya Puma Energy ambayo inayo uwezo wa kuongeza uwekezaji. Ukweli ni kwamba miradi mipya inakuja na michongo ya rushwa. Hapa si semi kwamba Makamba amechukuwa rushwa lakini napata wasiwasi pale ambapo hawaongelei kabisa Puma energy. lakini vilevile tujiulize ni nani alitoa pesa kwa bandari kutaka kujenga bila kuhusisha serikali matank ya kuhifadhi mafuta. Mpaka leo hatujui wale watu waliokuwa wanaiba mafuta kwenye ile pipeline bandarini kesi yao imefika wapi. Inaelekea uhalifu wowote wakishaona wamiliki wa nyumba au wezi ni watu wa serikalini kesi inapotea. Wale wezi wa mafuta kesi yao imeenda kichini chini pamoja na ukweli kwamba wamehatarisha maisha ya watu, wamekwepa kodi na kuiba mafuta kwa miaka mingi. Hizi dili si kweli kwamba watu walikuwa hawajui.

Wizara ya nishati inatakiwa iangaliwe kwa ukaribu sana maana ufisadi mkubwa Tanzania kwa historia unatokea kwenye sehemu hii. Msikilize makamba kwenye clip hapo chini


 
Usisahau genge la kuficha sukari ikaadimika, bei ikapanda halafu genge likaanza kuwapiga wanyonge
 
Hayo mafuta mnayoweka mnayapata wapi. Mnauwezo wa kuhifadhi mafuta ninyi. Acha kuumiza kichwa tulia tu.
Na kwasasa mafuta hayatawezekana kuhifadhiwa mlishachelewa saivi. Subiri mpaka vita itakapokwisha. 😃😃😃😃😃😃😃🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Hakika tunachanja mbuga, acheni ngano na magugu vikuwe pamoja ili siku ikifika tutajua nani alikuwa chuya na nani alikuwa mbegu ya kuliwa.


Ahahhaaa 😄 🇹🇿 Tanzania great country with full of dark acting!.
 
Nini kimetokea pale TIPER, bila Shaka kuna matanks mengi tu na makubwa, na pale makambako?
 
Back
Top Bottom