Tuwe makini na urudishwaji wa pesa BOT jamani

BabaH,

Lakini hela tunazoambiwa zimerudishwa hazina uhusiana na EPA ni hela za program iliyokuwa inaitwa Commodity Import Suport (CIS) so nadhani hazina uhusiano na zile za EPA billion 133.

Kikubwa tunataka serikali iweke wazi who are those people waliopewa hizo hela. Na kama mfuko huo ulisimamishwa 1992 ni More than 10 and according to banking Tanzania regulation (BoT reguulation) mtu asipolipa deni lake kwa siku 90 ni defaulter na anapaswa kutangazwa hadhazani wakati recovery measure zinaandaliwa.

watuambie ni kina nani na kiasi gani walizochukua. Sio tuambiwe baaadhi ya watu wamerudisha bila kutuambia hali halisi as of today.
 
Hakuna pesa iliyorudishwa! sana sana hizi ni propaganda kupitia vyombo vya habari kujaribu kupoza hii ishu baada ya kuona moto wa Richmod ulivyowapukutisha wanasiasa.

Wengi wa wamiliki wa yale makampuni hewa ni "maboya" tu na pesa ilichukuliwa na wanasiasa ambao wasingependa kuanikwa hadharani.

Hii EPA siyo mara ya kwanza; ziliwahi kuliwa pesa kwa mtindo huu huu miaka ya '80 mwishoni katika kile kilichoitwa OGL na DCP na hakuna senti iliyorudishwa! La kushangaza, hawa mafisadi wa sasa hivi, baadhi yao ni walewale waliokula pesa za OGL na DCP na wamekuwa wafadhili wakubwa wa chama tawala.
 
Back
Top Bottom