Tuwe makini na mitandao ya kijamii

SueIsmael

JF-Expert Member
Dec 11, 2013
932
1,282
Ndugu zangu,

Leo naona niilete hii hoja tena hata Kama ilishazungumziwa kabla.

Hii mitandao ya kijamii inabidi tuitumie kwa umakini mkubwa sana. Kila wakati kuna mtandao mpya unaanzishwa Na watu hukimbilia kuitumia kabla ya kujiuliza kama wanaihitaji au la. Don't get me wrong, mitandao ya kijamii inamanufaa yake ila tusisahau iko kama kisu kwani huweza kutumika kudhuru pia.

Kubwa zaidi, ni watoto wetu. Je tunawafundisha matumizi sahihi ya hii mitandao? Kwanza tumewafundisha matumizi sahihi ya simu za mkononi? Ukimnyima bila kumfundisha bado hujamsaidia Na ukimpa bila kumwelekeza matumizi sahihi unaweza ukamhatarisha pia.

Jamani dunia ya sasa imeharibika sana. Uhalifu wa kwenye mitandao unaongezeka kwa kasi. Tujifunze kuzungumza wenyewe kwa wenyewe na watoto wetu pia.

Hata magaidi wanatumia mitandao ya kijamii kutafuta wafuasi. Wezi hutumia taarifa zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii kufahamu undani wako. Sasa hivi kuna apps na networks kama periscope, snap chat, Inke, Ustream, nk. ambazo zinampa mtumiaji uwezo wakutuma picha na video wakati mwingine moja kwa moja. Tunajifanyia surveillance wenyewe.

Tukiendelea kuishi kwa kufumba macho na kutotambua madhara ya hivi vitu tutakuja kujuta Sana baadae.
 
Sikio la kufa...! Mitandao kama ukimwi haiepukiki sababu ya utandawazi km vile ukimwi na mahali ulipokaa...!
 
Back
Top Bottom