Tuwe makini na marafiki tunaowaamini na kuwaona ndio kila kitu.

Ornate

Member
Jul 13, 2021
26
33
Si vyema kuishi bila rafiki lakini je, unamuamini rafiki yako kiasi gani na mangapi kukuhusu wewe anayafahamu.
Kuna baadhi ya marafiki zetu, tunaowaona kuwa watu wa karibu wamekuwa na tabia za panya, yaan wanang'ata huku wanapuliza.
Unaweza kupata shida fulani katika maisha mfano ya kifedha na unapomwambia anakuwa sio msiri na kuanza kutangaza kwa wengine.
Haitoshi wapo baadhi yao ambao tuna waamini sana inafikia hatua tunawatambulisha kwa wapenzi wetu, lakini kwa tamaa zao wanaanza kuwalisha maneno ya ajabu kusudi tu watu waachane na watimize haja zao.
Lazima tuwe na mipaka katika mahusiano na marafiki zetu ili kuepukana na madhara yake.
Kwani hili mwisho wake huwa ni ugomvi na hata kugharimu maisha ya mtu pamoja. Kuaminiana ni jambo jema lakini liwe na hatua.
 
Rafiki yangu jamaa angu alinipeperushia ndege wangu kipenzi hadi leo sina hamu nae japo tunaogea.Rafiki yako ndie ajuae madhaifu yako na ndo atakaye kuangusha. Siri yoyote ikivuja ni marafiki zako ulowashirikisha
Rafiki wa kweli ni pesa tu kamwe haitokuangusha tafuta pesa na si marafiki,
 
Mpaka tukiumizwa nao ndio tunapata funzo,. kuna mtu saa hii anamwambia rafiki yake jinsi ameongezewa mshahara, kapata mchumba,kapandishwa cheo kazini,ni mjamzito,anaanza ujenzi mwingine,ananunua gari,kapata sponsor anamuhonga balaa n.k woiii ni hatariii
 
Fact
 
Rafiki yangu jamaa angu alinipeperushia ndege wangu kipenzi hadi leo sina hamu nae japo tunaogea.Rafiki yako ndie ajuae madhaifu yako na ndo atakaye kuangusha. Siri yoyote ikivuja ni marafiki zako ulowashirikisha
Rafiki wa kweli ni pesa tu kamwe haitokuangusha tafuta pesa na si marafiki,
Ooh pole
 
Siri za mke wangu nitabaki nazo ndani ya nafsi yangu mpaka naiaga Dunia. Kamwe haitotokea hata sekunde moja nimwambie the so called rafiki siri zangu za chumbani kwangu na mke wangu. Haya ni mafundisho aliyonipa babu yangu kabla hajatangulia mbele za haki
 
daaaaah kuna mpuuzi mmoja tunafahamiana toka primary school, tulikutana chuo, akawa ananinyea kwa watu waliokua wananikubali sana.Alaaniwe popote alipo
 
Back
Top Bottom