DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
Hizi show rooms nazipatia mashaka sana, watu wengi wanaoibiwa magari hapa Dar ni wale walionunua magari yao kwenye show rooms za maeneo hayo. Na uchunguzi wangu mdogo niliofanya magari mengi kwenye show rooms hizi ni yale magari yaliyotembea kwa muda hapa TZ, kwahiyo yanakuwa ni magari ya watu fulani ambao wameomba wawekewe kwenye hizo show rooms ili wauziwe, na hata utakapokuja kulinunua hutapata nafasi ya kuonana na mtu mwenye hilo gari. Baada ya muda hilo gari utaibiwa katika mazingira ya kutatanisha, ni kana kwamba mtu alikuwa na copy ya ufunguo wa hilo gari. wengi wanaoibiwa hayo magari ni wale wanaoishi maeneo hayohayo, wataibiwa maeneo ya sinza, mwenge, pale mlimani city ndio usiseme, maeneo ya udsm, changanyikeni, mbezi etc.
Kwahiyo tuweni makini sana tunaponunua magari kwenye show rooms hizi. Maana ni jinsi gani inavyouma kuibiwa gari ambalo umelipata baada ya kujinyima mambo mengi na kulinunua halafu mtu anakuja kulichukua kama vile la kwake.