Tuwe makini. Humu ukumbini wameingia watu "virus" ambao nia yao ni kuona Chadema wanafarakana. Wapo watu wanaoshabikia na kusambaza sumu, kwa mfano kutabiri Zitto kutaka kugombea uongozi wa upinzani bungeni, wengine wanasema Zitto kasaliti Chama...na mambo kama hayo. Tuwapuuze hawa watu kwani mambo ya Chama yanashughulikiwa na vikao vya Chama na sio ushabiki. Nina uhakika Viongozi wa Chadema na wanachama wake ni Makini na watafanya maamuzi MAKINI kukiweka tayari Chama kwa 2015.
Tuwashukuru wote walioleta changamoto ya kisiasa nchini, Bila hawa akina Mbowe, Slaa, Zitto na wengine tusingekuwa hapa tulipo. Tuwape moyo badala ya kuwakatisha tamaa mana saa ya mabadiliko inakaribia.
Kutokana na uchaguzi wa mwaka huu, Japo CCM wameshinda lakini nchi na uongozi hautakuwa kama ulivyokuwa kabla ya 2010.
CCM watapandikiza watu humu JF ili kuvuruga wapenzi wa Chadema mana wamegundua JF ina nguvu kuleta mabadiliko. TUwe MAKINI SANA!