Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kuna jambo nimejiuliza kuhusu Ubaguzi ambao tunaulalamika sana kila siku hasa kuhusu Wazungu wanaoufanya dhidi ya wageni wanaohamia huko kwao, nimejaribu kulifikiria sana nikaona kama Wazungu wanaonewa sana na karibia kila mtu na kulaumiwa kwa mambo ambayo sisi tunaolalamika tusingeyakubali kwenye nchi zetu!
Nitatoa mfano kuna miji mingi ya Wazungu Ulaya au Marekani leo hii wageni ni wengi sawa au klk wenyeji, chukulia kwa mfano London nasikia kuna sehemu kuona Mzungu asilia siyo rahisi, sasa fikiria kwa mfano leo hii labda wewe ni mkazi wa Sinza, Mbagala au Keko kesho wanahamia watu ktk India au China na wanakuwa wengi klk nyie yaani fikiria nyumba zote za Sinza ziwe na Wachina au Wahindi wengi klk sisi WatanZania halafu ukienda Shule kama Mapambano kuwe na Wanafunzi wa Kichina wengi klk wetu sisi watu wetu waishio haya maeneo watalipokeaje hili swala?
Au chukulia kwa mfano kinachotokea sasa hivi Ulaya na Marekani wahamiaji ktk Uarabuni, kwetu Afrika na sehemu nyingine kwa wingi wao wanakuja na kuanza kujenga Misikiti au Matempo kama kwao, Je Wazungu wanaweza kwenda Uarabuni au India na kuanza kujenga Makanisa? Je hizo jamii za huko zitakubali?
Hivyo nafikiri Dunia kwa hili la Ubaguzi inawaonea Wazungu, kwani kwangu mimi Wazungu wamekubali kufungua milango yao na maisha yao kwa kila mtu ambapo wengi wetu hatuwezi kukubali huku kwetu, fikiria TanZania watu wanalia na kulalalmika kwamba Wakenya wamejaa TanZania, au Wahindi na Wapakistani na hiyo ni Dar, Je kama siku ikija vijiji vyetu kuvamiwa na wageni kama vile tunavyovamia vijiji vya Wazungu hali itakuwaje? Kumbuka hawa wageni tunaolia wamejaa kwetu wala hawafikii asilimia 5% ya Watz, sasa kwa Wazungu kuna maeneo wageni wanafikia 80%!
Kwa maana huko Ulaya na Marekani mpaka vijijini wageni wamevamia na wamekuja na tamaduni zao wanajenga sehemu za kuambudu n.k!
Tumeona AK walichoma moto wageni!
Ukiangalia hili la Wakimbizi Ulaya leo wamechukuwa Wakimbizi ktk Syria, Afghanistan kwetu Afrika mpaka zaidi ya milioni mbili, Je ni nchi gani ingeweza kukubali kufanya hivi? Ni kwa nini Mkimbizi atoke Syria au Nigeria avuke nchi kibao aende Ulaya?
Je sisi tungekubali?