Tuwaungeni Mkono Wazalendo Wachache Tulionao

John Mashaka

Member
Feb 6, 2013
40
91
Hakuna binadamu mkamilifu. Hata yesu alikuwa na mapungufu yake. Yawezekana huyu kiongozi akawa moja ya watu wenye udhaifu kwa namna moja au nyingine kama binadamu. Lakini pale kiongozi anapojitokeza kuonyesha uzalendo, uchungu kwa namna hii hadharani, lazima tumuunge mkono.Haya ni maneno hadimu sana kutoka kwa viongozi wetu. Ni ujumbe mzito sana na changamoto kwetu kama taifa kushirikiana kuzilinda rasilimali zetu. Swala la Faru na Tembo itatuathiri wote kama watanzania bila kujali itikadi na matabaka yetu.Licha ya madhaifu ya Kibinadamu, Balozi Kagasheki na Mh. Mwakyembe wanatupa changamoto kubwa sana kama vijana kutokana na uzalendo wao...

Sikiliza

Last edited by a moderator:
Dhamira ya kweli haipimwi kwa maneno
You're very right, dhamira ya kweli haipimwi kwa maneno! Lakini pamoja na yote hayo, nazani tunaweza kuanza kumjadili huyo Kagasheki hata kama si kwa kutumia video iliyowekwa na John Mashaka coz' Kagasheki sio mgeni katika siasa za Tanzania! Tuanzie hapo sasa; weka itikadi na mapenzi halafu nieleze unaweza kumuelezea vipi Kagasheki!
 
Last edited by a moderator:
Namjua kama mwanasiasa nguli watoka enzi na enzi japo mda wake mwingi kautumikia nje ya nchi kama balozi,na sasa ni waziri wa maliasili na toka ashike hyo nafasi sijaona mabadiliko yoyote kwenye hyo secta mkuu,na hili swala la tembo ni gumu sana kudeal nalo kwani wahusika wakuu ni maboss zake,sasa hapo utafanya nini kudhibiti wizi huu?
 
tabu tupu mkuu,kuna siku nilikuwa nachart na mzee mmoja msitaafu wa usalama wa Taifa<japo huwa hawasitafuu hawa> akasema nchi hii inatakiwa watu kama tundu lisu asiyetaka kupindisha sheria ndiyo tutanyoka otherwise hatuna kiongozi ndani ya serikali hii anaweza kuzingatia sheria za nchi hii,kwani sheria hizo ziko juu ya viongozi wote bila kujali huyu ni rais ama waziri......lakni kwa sasa,kiongozi anatuhumiwa kujihusisha na ujagili wa faru na tembo wetu na bado wanasiasa wanakuja kumtetea tena mbele ya watungaji wa sheria,hapo utasema nchi hii itasonga?

viongozi wote wamejipanga kudhibiti cdm tu na sio kushughulika matatizo ya wananchi moja kwa moja
 
wazalendo wako chadema tuuuuuuuu, kwingine wako mafisadi na majangili, kwehkweheeerrrrr,wachaga tangu lini wakawa wazalendo?????? wao ni fedha tuuu na ujambazi na sasa wameingilia siasa!! tunashuhudia ujambazi wa kisiasa. ALL IN ALL, THIS COUNTRY CAN NEVER BE LEFT TO DOGS, and the dogs of this country are well known. hata mwalimu nyerere aliwaona
 
Mlianza na udini, ukaekspaya. Mkaja na ukanda, nao pia hauna tija. Sasa mnashupalia ukabila. Upepo wa mabadiliko unavuma toka pande zote za nchi. Itawasaidia kidogo mkiacha uvivu na tamaa. Unamkumbuka Lyatonga? Sokoine je? Mkiwa na viongozi wa aina hii nchi itatulia. Angalia utendaji wa watu usiangalie makabila yao. Makabila mengine uchapakazi ndio utamaduni wao.
 
Namjua kama mwanasiasa nguli watoka enzi na enzi japo mda wake mwingi kautumikia nje ya nchi kama balozi,na sasa ni waziri wa maliasili na toka ashike hyo nafasi sijaona mabadiliko yoyote kwenye hyo secta mkuu,na hili swala la tembo ni gumu sana kudeal nalo kwani wahusika wakuu ni maboss zake,sasa hapo utafanya nini kudhibiti wizi huu?

Jamani kama alivyosema bwana mashaka. Balozi kagasheki ni jembe. Ni mwadilifu na mzalendo wa kweli. Siyo kama wakina Mulugo kwambwa na Muhongo ambao wanajiita profesa kumbe hovyo tu !
 
Kama kagasheki ni jembe,we wanna see huo ujembe wake hadharani na sio kwenye makaratasi tu,i do support him sana tu ila anahitajika zaidi ya kagasheki na mwenye moyo wa chuma anaweza mtia ndani mtu yoyote yule hata kama ana mapembe na hapo ujembe wake utaonekana kwa watu wengi na sio kwa kikundi cha watu fulani tu.

"kuisafisha wizara yake ni simple sana,aanze na hao wasaidizi wake wanaomiliki vitaru na makampuni ya tours na maafisa wanyamapoli wote apige chini hapo tutaongea,otherwise ni kelele tu kama tulizozizoea" business as usual
 
tabu tupu mkuu,kuna siku nilikuwa nachart na mzee mmoja msitaafu wa usalama wa Taifa<japo huwa hawasitafuu hawa> akasema nchi hii inatakiwa watu kama tundu lisu asiyetaka kupindisha sheria ndiyo tutanyoka otherwise hatuna kiongozi ndani ya serikali hii anaweza kuzingatia sheria za nchi hii,kwani sheria hizo ziko juu ya viongozi wote bila kujali huyu ni rais ama waziri......lakni kwa sasa,kiongozi anatuhumiwa kujihusisha na ujagili wa faru na tembo wetu na bado wanasiasa wanakuja kumtetea tena mbele ya watungaji wa sheria,hapo utasema nchi hii itasonga?

viongozi wote wamejipanga kudhibiti cdm tu na sio kushughulika matatizo ya wananchi moja kwa moja

Mkuu umemaliza, Katika viongozi wetu hawa hata pale wanaposema tushirikiane binafsi naona kama wanatutania ili tuone wamejirudi. Ni mangapi yanawekwa wazi na wapenda maendeleo, halafu hao hao wanaoomba tushirikiane wanaanza kutungo'oa meno na kucha, Tena wanasimama kifua mbele kuwatetea hao hao majangili?.
Juzi tu hapa Kagasheki anatetea jamaa wa loliondo aendelee kuumiza wananchi tena aongezewe na eneo, leo anaomba tumsaidie. Kwa nini anaota mchana hivi?.
Likikuja suala la ufisadi wakaomba wasaidiwe, Wafisadi wakawekwa wazi na leo tunashuhudia serikali ndio imekuwa ya kwanza kuwaficha na kuwatetea mafisadi.
Likikuja suala la Mauaji ya walemavu wa ngozi, viongozi wakaja juu lakin mwisho wake Hata kesi hatuoni zinaishia wapi.
Imekuja utendaji mbovu wa Jeshi letu la polisi, wakaja na ulinzi shirikishi na wananchi wakajirudi matokeo yake wanaowekwa wazi ni wachache sana wanachukuliwa hatua tena wale wadogo wadogo huku mapapa wakipandishwa vyeo na kurutubishwa na kodi zetu.
Watanzania tunatakiwa kuwasikiliza kwa umakini na kuwaelewa vizuri viongozi wetu, Ni kwa nini kila siku wanakuja na maneno mazuri wanapoona maji ya shingo hata hivyo bado wamekuwa ni wagumu wa kuyafanyia kazi yale wanaoyataka wasaidiwe. JAMANI HATA NYUMBA UIPENDAYO IKICHOKA UNAIBOMOA NA KUJENGA NYINGINE HATA KAMA KIWANJA NI KILE KILE.
 
This is a blasphemy. Jesus is God. He is omnipotent, omnipresent and omniscient. He can never err. He is the Alpha and the Omega. You must repent this sin.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Jamani kama alivyosema bwana mashaka. Balozi kagasheki ni jembe. Ni mwadilifu na mzalendo wa kweli. Siyo kama wakina Mulugo kwambwa na Muhongo ambao wanajiita profesa kumbe hovyo tu !

Mulugo professor? God forbid.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
jamani kama alivyosema bwana mashaka. Balozi kagasheki ni jembe. Ni mwadilifu na mzalendo wa kweli. Siyo kama wakina mulugo kwambwa na muhongo ambao wanajiita profesa kumbe hovyo tu !
e mbaya.
umenichefua na hiyo signature yako ile mbaya.
 
Mkuu ebu shushia na ile video ya mch Msigwa ili siku yako iende vizuri maana umegusa panapo husika kabisa na matatizo yanayotuzunguka........'Matatizo ya nchi hii hayawezi kutatuliwa na watu hao hao waliyoyaanzisha"
 
Kama anaongea tu, hawezi kumkamata bosi wake wa chama (Kinana) kwa uchunguzi ambaye ametajwa sana kuhusika na ujangili wa tembo, tutamuelewaje. Anybody can speak
 
Kwani kipi anachosema zaidi ya kulalamika kama bosi zake tu. Kwa CCM ilivyo, ili kujua wanachomaanisha wewe tafsiri opposite ya kila anachosema. Anadai wawepo watu wazalendo wakti watu kama Tundu Lissu, Mnyika, Msigwa ambao ukiwasoma kisaikolojia mioyo yao inaumia kwa kutetea Utanzania lakini CCM wanawaona wabaya wao. Unaweza kukufuru kuwaombea CCM wote wafe mambo yaanze upya, wanaudhi sana hawa watu jamani
 
Back
Top Bottom