Tuwaunge mkono wanaharakati wanaotetea haki za walemavu kwa kupiga kura hapa kabla ya Saa 6 Usiku

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
WanaJF,

Shirika la Under the Same Sun linalotetea haki za walemavu wa ngozi linawania tuzo inayodhaminiwa na taasisi ya kutetea haki za binadamu ya nchini Uholanzi,Human Rights Tulip.

Yapo mashirika 30 kutoka sehemu mbalimbali duniani yanayowania tuzo hiyo.Kutoka Tanzania ni shirika hili pekee lililoingia katika kinyang'anyiro hicho.Tulipigie kura kwa wingi shirika hili kwa muda mchache uliosalia

Mwisho wa kupiga kura ni kabla ya saa sita usiku wa leo

Kura yako ni Sehemu ya kuonyesha sapoti kwa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi.Tuwaunge mkono na kuwatia moyo kwa kupiga kura kwa wingi kupitia link hii hapa chini.Hebu tufanye hivi kwa ajili ya kupaza sauti zaidi kutetea ndugu zetu,tufanye hivi kwa ajili ya Tanzania

Under The Same Sun | Candidates and Voting | Human Rights Tulip
 
  • Thanks
Reactions: prs
mkuu naona umekuja kitaifa sasa mambo ya sakosi umeachana nayo sasa
 
Shukrani sana kwa wote mliopiga kura.Ni sehemu ya mchango wenu katika kutetea haki za ndugu zetu walemavu wa ngozi

Tatizo la upigaji kura nchi hii linahitaji a very serious intervention.Kupiga kura tu hata kwa njia ya mtandao ambayo haihitaji kupanga foleni au kutembea umbali fulani nalo ni tatizo.

Nadhani kuna tatizo lingine tofauti na ile dhana ya kuwa watu hawapigi kura kwa kuwa wanajua zitaibiwa.Sasa kwa hili inakuaje?

Ni uvivu au ni tabia ya kutochukulia upigaji kura kama suala serious?
 
Hao wahoranzi ni wajinga sana, kutambua mchango wa shirika hili kunahitaji kupigiwa kura kwa misingi ipi? Ni walemavu gani wengine maisha yao yamewekwa kwenye ubao wa machinjio kutokana na ulemavu wao kama hawa albino.

Any way kabla sijapiga kura.

Lengo la hiyo tuzo ni nini?
 
Back
Top Bottom