Tuwatambue Vijana Wetu na Kuwazawadia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwatambue Vijana Wetu na Kuwazawadia

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sabi Sanda, Dec 23, 2009.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wana JF,

  Kila mwaka matokeo ya Mitihani ya Kitaifa katika ngazi mbalimbali yanapotoka huwa tunapata fursa ya kujua vijana wetu walioongoza nchi nzima katika ngazi ya darasa la saba, O Level na A Level. Kama sehemu ya jamii ya Watanzania, napendekeza tuanzishe utaratibu wa kuwazawadia vijana wetu hawa kwa kufanya vizuri katika masomo yao. Katika kila ngazi ya elimu inapendekezwa tumzawadie kijana aliyekuwa wa kwanza nchi nzima. Tujadiliane kuhusu zawadi zipi wanastahili kupewa bila kusahau kitu kama ngao ya JF na Cheti toka JF.

  Iwapo wazo hili la kuwazawadia vijana wetu litakubalika, MUNGU akipenda kila robo mwaka nitajitahidi kuchangia shilingi elfu 50 kuanzia mwaka ujao (2010) kwa ajili ya kutimiza azma hii. Hapa tunaweza kuanzisha Mfuko wa Elimu wa JF ambao tutakubaliana uitwe kwa jina gani.

  Siku njema kwenu wote.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  jf inavyochukiwa!.......mmh
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,427
  Likes Received: 3,789
  Trophy Points: 280
  inachukiwa kivipi mkuuu...........?????
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hao vijana watafuatiliwa na kusakamwa sana, na huenda wakaathiriwa hadi mbele ya safari wakiwa vyuoni, maana JF ni mwiba!..Labda kiwe ni kitendo cha siri!..
   
 5. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  PakaJimmy na Geoff,

  Naamini JF inalisaidia sana taifa letu katika kutoa mbadala wa mawazo toka kwa watu mbalimbali na nini kifanyike katika kuindeleza nchi yetu. Binafsi kwa sasa siamini kama watawala wetu wanaichukia JF. Naamini ni kinyume chake.
   
Loading...