Tuwashauri wazee wetu kuchangamsha viungo ni muhimu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Hawa wazee wetu wengi wao wakistaafu basi anakuwa amerelax kabisa. Umejitahidi kuwaboreshea wazee makazi, unawawekea vijana wa kuwasaidia shughuli na wao wanaona maisha ndiyo haya.

Asubuhi wanaamshwa wafungue kinywa kila kitu kiko mezani. Baada ya hapo wanaangalia TV,mchana wanaitwa chakula tayari na jioni hivyo. Huu ndiyo mwanzo wa matatizo. Si muda mrefu mtaanza kupelekana hospitali kwa matatizo ya moyo, miguu, kisukari etc.

Washauri wachangamshe viungo kila asubuhi. Hata kuwahi msikitini au kanisani kila siku ni faida ya roho na mwili.

Kustaafu ichukuliwe kama kufanya mambo kwa muda wako lakini si kuwa umeacha kabisa kuishi kila kitu ufanyiwe.
 
Washauri wachangamshe viungo kila asubuhi. Hata kuwahi msikitini au kanisani kila siku ni faida ya roho na mwili.
Hiyo umenena mkuu, ndio maana wale wamama na madingi wa dini sana huwa hawazeeki siku zote wako vilevile...hii pia nimeiona kwa walimu...unakuta kuna mzee anakuambia ''huyo ni mwalimu wangu kanifundisha'' na ukimuona yule mwalimu unaona ni kijana kuliko yule anayesema kafundishwa.....
 
Nimegombana sana na bimkubwa kuhusu hiki kitu unakisema hapa, nilimuomba sana ajiunge na yale mavyama ya watu wazima pale kanisani moyo mtakatifu wa yesu, sijui wawata, na vingne vipo vingi humu kanisani kwetu (katoliki) ili tu apate hizo movement hakutaka kabisa hadi leo hataki na hyo ilikua 2017 alipostaafu, yeye alichopenda akae tu nyumbani kwa kuwa tayari ashachakalika sana akiwa kazini, leo miguu mara magoti yanawka moto mara ooh mbona sina hamu ya chakula,.....ndo basi tena kutafuta neuroton na joint support kumtumia.🤦‍♂️
 
Rafiki yangu mama yake alikuwa mchuuzi wa mboga na matunda, aliifanya biashara hii baada ya dingi kupata mchepuko kwenye mid life crisis na kugundua kuwa mchepuko anatema yai kuliko mkewe.

To cut a story short, dada mkubwa alimaliza shule akaolewa na mume mwenye pesa zake. Walimjengea mama nyumba na kumuwekea kila kitu cha muhimu ndani.

Mama akawa akitoka chumbani anashinda kwenye makochi, jioni anakwenda chumbani. Sasa hivi hata kwenda chooni anakwenda kwa shida. Miguu, mifupa, circulation.
Wenyewe wanasema kheri wangemshauri aendelee na uchuuzi wa mboga na matunda.
 
Nimegombana sana na bimkubwa kuhusu hiki kitu unakisema hapa, nilimuomba sana ajiunge na yale mavyama ya watu wazima pale kanisani moyo mtakatifu wa yesu, sijui wawata, na vingne vipo vingi humu kanisani kwetu (katoliki) ili tu apate hizo movement hakutaka kabisa hadi leo hataki na hyo ilikua 2017 alipostaafu, yeye alichopenda akae tu nyumbani kwa kuwa tayari ashachakalika sana akiwa kazini, leo miguu mara magoti yanawka moto mara ooh mbona sina hamu ya chakula,.....ndo basi tena kutafuta neuroton na joint support kumtumia.🤦‍♂️
Hata kuwahi misa asubuhi tu inasaidia sana.
 
kustaafu si kupumzika kabisa, mwili ulishazoea kufanya mazoezi miaka mingi iliyopita.
kujishughulisha(mazoezi) ni afya(kinga) ya mwili.
 
Kweli kabisa, kustaafu kazi haimaanishi kuustafisha mwili kufanya kazi. Nenda ibada za asubuhi sana, fanya kazi za nyumbani hata kama unawasaidizi. Waweza pia fanya kazi (kuajiriwa) ambayo ulikuwa unaifanya kabla ya kustaafu, hasa wafanyakazi waliokuwa serikalini.
 
Hata kuamka na kwenda kuchukua maji ya kunywa ni faida kwa mwili kuliko kumuita mjukuu akuletee maji.

Kama kuna birika ajitengezee chai, kama hakuna birika maji ya moto kwenye chupa yanamfaa kujitengenezea chai.
 
Sasa mimi nimefanya kinyume. Najuta. Mama yangu alipostaafu akiendelea na mambo yake, mara forever living,mara ana kiofisi,kiduka kifupi bado alikuwa akiamka asubuhi ana pa kwenda.

Miaka hii michache changamoto za kiuchumi hivyo vishughuli vyake vikawa vinayumba,haviingizi hela hapo sasa kodi ya ofisi ikabidi tumlipie mimi na mdogo wangu. Mwisho tukamwambia aache tu akae home tumpe allowance yake kila mwezi. Alikubali kwa shingo upande sana.

Aisee baada ya muda mfupi tu alianza kuumwa magonjwa yote ya uzee. Ile kukaa idle,mawazo hakuwa na raha. Aliumwa sana, mpaka siku moja nikamwambia mdogo wangu sababu ya haya yote ni sisi kumuachisha misele yake.

Mungu mkubwa akapata nafuu na rafiki yake akaanza kumchukua wanaenda kwenye mambo yao. Siku hizi akinipigia utasikia tunaenda semina ya ujasiriamali inabidi nimsapoti tu aende na abaendelea vizuri
 
Nimegombana sana na bimkubwa kuhusu hiki kitu unakisema hapa, nilimuomba sana ajiunge na yale mavyama ya watu wazima pale kanisani moyo mtakatifu wa yesu, sijui wawata, na vingne vipo vingi humu kanisani kwetu (katoliki) ili tu apate hizo movement hakutaka kabisa hadi leo hataki na hyo ilikua 2017 alipostaafu, yeye alichopenda akae tu nyumbani kwa kuwa tayari ashachakalika sana akiwa kazini, leo miguu mara magoti yanawka moto mara ooh mbona sina hamu ya chakula,.....ndo basi tena kutafuta neuroton na joint support kumtumia.🤦‍♂️
Mkuu hata mimi hili ninalo taabika nalo mkienda hospitaL DK anasema mama yako mzima huyu anatakiwa mazoezi tu ukimwambia hivyo tu atakuwa mkali mpaka nyumba uiogope.
 
Huko kanisani wanaweza kwenda na usafiri,

Ungenyohosha maelezo tu, kwamba wafanye mazoez ya mwili .

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi mazoez ni sehem yangu ya maisha, kama kula au kwenda toilet..

Sitegemei kuacha, nimesahau nimeumwa lini seriously illness

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pia wanawake baada ya kuolewa mna relax sana yaani maisha mnaona ndio haya, hamjishughulishi tena umefunguliwa biashara una vijana wa kukusaidia kazi, nyumbani pia unamsaidizi yaani upo upo tu muda sio mrefu performance 6 kwa 6 upo chini ya kiwango full kunenepa, vyakula vizuri vyote unazuia na madkatari maisha hayana furaha tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hata mimi hili ninalo taabika nalo mkienda hospitaL DK anasema mama yako mzima huyu anatakiwa mazoezi tu ukimwambia hivyo tu atakuwa mkali mpaka nyumba uiogope.
Daaah hatuna jinsi mkuu ndo washazeeka hawa, na ni wakwetu lazima tuwalee....Yaan hapo hapo ukitaka akubali zoezi ni kufanya nae, kutembea nae, kila kitu ni kujifanya kama mnafanya wote ndio atakubali tena kwa tabu kitu ambacho angekuwa na mazoea ya kufanya mwenyewe angekua mzima zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom