Tuwashauri Waalimu na Wastaafu East Africa warudishe Kadi za CCM

akilimtindi

JF-Expert Member
Jun 30, 2008
421
83
Nimerudi tena baada ya kutoka kwa muda waungwana wa jumuiya hii. Naombeni kuja na hoja yangu ambayo nadhani kwa mawazo yangu mtindi inaweza kuleta mabadiliko makubwa ama inaweza kuwatia hamasa viongozi.

Kwa muda sasa kumekuwa na mabishano makubwa na kutokuelewana kwa sehemu kubwa kati ya Serikali ya CCM na Wastaafu wa Afrika Mashariki na pia kwa sehemu nyingine Serikali ya CCM na Waalimu wa Shule za Msingi/Sekondari. Wastaafu hawa na Waajiriwa hawa wamekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda mrefu kwa kile kinachoonekana kuwa ni Serikali kuona wao hawana meno ya kuing'ata serikali wala sauti za kuibweka walau kuitishia kama sio kuwatia kabisa meno viongozi wanaowanyanyasa. Sina haja ya kuongea mengi sana maana mengi yameonekana kwenye vituo vingi vya televisheni na kusikika kwenye vituo vingi vya redio.

Mifano hai ni kama ile ya JK kwenda kushabikia mimba za mashuleni huko Tanga kwa siku 9 kuwakimbia wazee waliopiga kambi ikulu kudai haki zao zilokwisha kuleta faida kubwa kwa mafisadi ambao hata kurudisha walau sehemu ya riba ni utata. Hata walioachwa na JK kuongea na hao wazee ilikuwa taabu, wote walikimbia na kuwaona wastaafu kama ombaomba wanaotakiwa kuondolewa na polisi pale Ikulu ya mafisadi. Je, ni kweli wazee wetu ni Ombaomba?

Mfano mwingine ni pale Serikali ilipoamrishwa kulipa madai ya waalimu kwa siku kadhaa kulingana na makubaliano vinginevyo wangegoma, hapa mimi waalimu kidogo walinipa moyo maana "immediately" kesho yake serikali ilitii amri utadhani walishtuliwa usingizini. Serikali ya CCM bwana, utadhani saa iliyokwisha betri, hadi uigonge gonge ndio iamke kufanya kazi. Nilitaka kutoa mfano mwingine lakini nikaona wakati wake bado, utakuja. Sasa vita bado inaendelea, bado madai hayajamaliziwa.

Mimi nina njia moja rahisi sana, na hii ikitumiwa ipasavyo hakutakuwa na haja ya kutumia nguvu wala kupiga kelele na fisadi yeyote yule maana ni lazima mawili kati ya haya yatekelezwe. Na huu ndio wakati muafaka wa kuyafanyia kazi maana uchaguzi unakuja... "WASTAAFU WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA WATOTO NA WAJUKUU WENU, RUDISHENI KADI ZA CCM (Chama cha Mafisadi), NDIO IMEKULA PESA ZENU TANGU ENZI WA UJANA WENU NA SASA WOTE MNAKUFA MASIKINI WENZENU WAKIENDELEA KUSHINDWA KUBEBA TUMBO ZAO". Hilo ni kwa Wastaafu.

Pili... "WAALIMU WOTE TENA WA NGAZI ZOTE, RUDISHENI KADI ZA CCM (Chama cha Mafisadi) MAANA NAULI ZENU ZITAISHIA NJIANI WAKATI WENZENU WAKIPELEKA MAHAWARA ZAO SOKONI KWA MASHANGINGI MAPYA KILA SIKU" Nitawaambia kwanii... Waalimu wa nchi hii ni wengi mno na nina hakika zaidi ya 30% ya kura wanazopata CCM ni kutoka kwa Waalimu, simply tuwanyanganye hizo 30% tuone.

Mawili kati ya Haya ni yapi?... Ni lazima aidha Serikali ya CCM (Mafisadi wawalipe pesa zenu maana hawatakubali kundi kubwa kiasi hicho liondoke CCM. Kuwashawishi kupitia viongozi naiona njia ngumu maana shida haziishi. Kama watakuwa wagumu kulipa, naiona njia ya CCM kuanza kuanguka wazi kabla ya 2010 maana walioathirika wote wataelewa wazi kwamba hii sio serikali tena bali ni majambazi walipania kutunyonya damu zetu kwa nguvu zao zote hata ikibidi kukaba wananchi, kuua na hatimaye kunyonya hiyo damu...!

FANYENI MAAMUZI MAANA NDIO WAKATI WAKE, UCHAGUZI UNAKUJA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom