Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Kiburi kitawaponza hawa ndugu zetu wa CCM, waliungana kumkingia kifua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa DSM kama kwamba wao hawajui kipi ni kosa Kwa mujibu wa sheria na katiba, au kipi sio kosa.
Sasa wanaoneana haya wao Kwa wao na kila mmoja akikana aliyoyazungumza siku chache zilizopita na sasa wanasema 'Makonda hafai kuwa kiongozi' kwasababu tu kisu kimegusa mfupa. Labda niwaulize, na hili la kuvamia ofisi za Clouds media limepelekewa ...na vita dhidi ya dawa za kulevya??
Ndugu zetu wa CCM Kwa heshima nawaambia kwamba muwe mnatafakari mambo na sio kushikilia kiapo cha kuitetea CCM hata pale inapofanya maovu, au viongozi wake wanapofanya maovu na kukiuka misingi ya uongozi.
Kwa taarifa yenu, sisi sote ni watanzania, yote yanayotokea nchini sote twayaona na kuyashuhudia wazi wazi, hivyo; tukilisema jambo mkachukulia kwamba ni wapinzani wamesema, ilhali mmejitoa ufahamu lakini ukweli mwaujua, hamlisaidii taifa wala chama chenu, mnaibomoa nchi na kuicheleweshea maendeleo, pia mnakidumaza chama chenu.
Haiwezekani watu wanapopiga firimbi kwamba kuna kiongozi anainajisi Elimu yetu ambayo ndiyo mapigo ya moyo ya taifa letu na msingi wa maendeleo, Kwa kughushi vyeti, halafu wanaibuka watu wanasema hizo ni kelele za wapinzani, mara ni kwasababu Makonda ameongea kuhusu madawa ya kulevya.. Mbona tumekwisha kumpata Kamishina Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia madawa ya kulevya Kamanda [HASHTAG]#Sianga[/HASHTAG], whatta else do we need? Makonda anahusikaje tena kwenye hili la madawa ya kulevya? Mbona hamumshabikii kamishina mpya mnabaki na Makonda, who is he? Au mliamini kauli take kwamba akisimama yeye, amesimama mungu??? Whatta kind of stupidity my fellow Tanzanians you doing?
Leo mtamteteaje huyu kijana aliyekengeuka, aliyepotoka, aliyelewa madaraka, aliyesahau mipaka ya kazi yake hata kufanya uvamizi kwenye kituo cha habari kushinikiza habari yake ya kuokoteza inayokiuka misingi, taratibu na taaluma za wanahabari kurushwa Kwa maslahi yake binafsi huku akivitumia vyombo vya ulinzi na usalama kumsaidia kufanya uharamia huo??
Nimuulize kaka yangu Humphrey Polepole, hii ndiyo CCM mpya mnayoinadi kwamba imerudi katika misingi yake? Kwamba na sisi wananchi tukiyaishi maneno ya wahenga kuwa 'Samaki mmoja akioza wote wameoza' itakuwa ni sawa?
Nchi ilipofikia hata Hayati Mwl. Nyerere laiti angekuwepo Leo Nina mashaka angeweza kuililia nchi na wananchi ambao wanajikuta wanayaishi matatizo yanayosababishwa na viongozi wabovu na wasio zingatia maadili ya utumishi wa umma.
Kama hili pia litaruhusiwa kupita kama ilivyoada Kwa maovu mengine yanayotukia nchini na kuachwa kwasababu tu wakosaji ni makada watiifu wa CCM, taifa zima litakosa imani na serikali iliyopo madarakani, kwamba wakosaji Hawa hawakosei Kwa Bahati mbaya au Kwa makusudi yao binafsi, wali wanayatenda haya wakiwa wametumwa na wakubwa zao wanaowateua na kuwapa mamlaka.