Tuwasemee na wale wengine wanaoozea mahabusu kwa 'ugaidi wa michongo'

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Mimi ni katika watu waliosikitishwa sana na kesi ya ugadi aliyobambikiwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Hii inaonesha suala la haki za raia lina mushkili sana. Fikiria kama inaweza kufanyika hivi kwa mtu mkubwa kama Mbowe, vipi hali zetu sisi wa kawaida?

Hata hivyo, wakati tukishinikiza Mbowe aachiwe, nawaomba ndugu zangu tuwakumbuke na wale wengine ambao wapo mahabusu kwa kesi ya ugaidi kwa hadi miaka hadi 10 sasa bila hata kesi kusikilizwa!

Yaani ni kama washahukumiwa kabisa. Afadhali ingeandikwa tu kwenye sheria ya ugaidi kuwa ukikamatwa na tuhuma hizo ndio tayari ushakutwa na makosa, tujue moja.

 
Kesi ziko nyingi...uchaguzi uliopita uliwatundika msalabani wapinzani kama vile kushirki uchaguzi ni Dhambi. Wengi wako magerezani, family zao znateseka sana!!Kifupi wote walitakiwa Rais atangaze waachiliwe warudi wajenge nchi yao, Kwani si mlioshinda si mnakula mema ya nchi kwanin muendelee kuwaweka kizuizn? Hofu ninii? Fingulieni wote nchi yetu sote si ya kundi la watu.
 
This Life is not for every one!
bila shaka watawala wetu pia wanaamini hili, kwamba wao tu ndio wanastahili kuwa hapo walipo, ukigusa maslahi yao unaozea ndani.
Ha ha ha binadamu hatujifunzi.
 
Back
Top Bottom