Tuwasaidieje watoto hawa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Alia kwa watoto wake wawili walemavu kukosa masomo
Kaanaeli Kaale
HabariLeo; Thursday,November 29, 2007 @00:07

910c1396067a.bmp

Mwanahawa Juma (katikati) akiwa na watoto wake Asia na Ahmed.
“INGAWA elimu ni haki ya mtoto na msingi kwa kila mtoto, Asia Kawi na mdogo wake anaitwa Ahmed, wamekosa nafasi ya kujiunga na shule kutokana na hali yao ya ulemavu,” anasimulia mama yao Mwanahawa Juma.

Mwanahawa anasema watoto wake wamekosa nafasi ya kujiunga na shule ya viziwi, jambo linalosababisha wakose elimu ambayo ingewasaidia maishani.

Watoto hao wenye uchu wa elimu huamka saa 11.30 alfajiri na kuvaa sare za shule kisha kukaa sebuleni huku wakinyoosha vidole kuelekea mlango ili kuashiria kuwa wanataka kutoka nje.

Wanapofunguliwa milango, watoto hukaa barazani na kuwapungia watoto wenzao wanaopita eneo hilo kuelekea shuleni. Watoto hao wanaozungumza kwa lugha ya ishara kila mara wanamsihi mama yao awapeleke shule.

“Jambo hili huwa linaniumiza na ni pigo kubwa kwa watoto wangu….walizaliwa wakiwa wazima kisha wakaugua na kuteseka kipindi chote cha utoto wao…na sasa wanaendelea kuteseka kwa kukosa nafasi ya masomo,” Mwanahawa anaeleza akiwa anabubujikwa na machozi.

Hivi sasa Asia ana miaka 15 lakini ameshindwa kupata elimu sahihi kulingana na ulemavu wake, kwani mama yake amejitahidi kumtafutia shule ya elimu maalumu kwa viziwi bila mafanikio.

Mwanahawa anasema mtoto huyo alipotimiza umri wa kwenda shule alimpeleka katika Shule ya Msingi Viziwi Buguruni lakini hakufanikiwa kupata nafasi ya masomo.

“Nilikwenda kumwandikisha katika shule ya msingi Viziwi Buguruni akajumuishwa na watoto wengine kwa ajili ya usaili na baadaye uongozi wa shule ulinijulisha kuwa amekosa nafasi,” Mwanahawa anasema kwa huzuni.

Baada ya kubaini kuwa mtoto wake amekosa nafasi katika shule ya elimu maalumu kwa viziwi, aliamua kwenda kumuandikisha katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. Mwanahawa alikuwa akimpeleka mwanawe shuleni kila siku kwa kipindi cha miaka minne, lakini mtoto huyo hakuwa anaelewa kitu kwa sababu hakuwa anafundishwa kwa lugha ya ishara.

“Asia alichanganywa na watoto wenye taahira ya akili na mtindio wa ubongo na kuhudhuria masomo kwa miaka minne lakini alikuwa haelewi kitu chochote, hata hivyo nilibaini kuwa akifundishwa kwa lugha ya ishara anaelewa,” Mwanahawa anaeleza.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo anahitaji elimu maalumu kwa watoto viziwi, aliamua kutoendelea kumpeleka shule ya Uhuru Mchanganyiko kutokana na ukweli kuwa alikuwa akitembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma ambayo haipo.

Anasema alirudi tena katika shule ya viziwi Buguruni kuomba nafasi kwa ajili ya Asia lakini hakufanikiwa, jambo linalosababisha mtoto huyo kukaa nyumbani.

“Ahmed alipofikisha umri wa kwenda shule nilikwenda tena katika shule ya Msingi Viziwi Buguruni kuomba nafasi…walimwita kufanya usaili kisha wananiambia kuwa hakuna nafasi kwa kuwa shule hiyo inachukua wanafunzi wachache,” Mwanahawa anaeleza.

Anadai kuwa ameomba nafasi hiyo kwa miaka minne mfululizo lakini hakufanikiwa, jambo linalosababisha watoto wote wawili kukaa nyumbani baada ya kukosa nafasi katika shule ya elimu maalumu kwa viziwi.

Anadai baada ya kwenda katika shule hiyo mara kwa mara walimshauri ampeleke Ahmed katika shule ya Msingi Mugabe ambako kuna kitengo cha elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza.

Hata hivyo, Mwanahawa anasema ameshindwa kumpeleka mtoto huyo katika shule iliyopo Sinza kwa kuwa kuu mbili. Kwanza hana kipato kitakachomwezesha kugharamia nauli ya kumpeleka shule kila siku, pili ana mtoto mwingine mlemavu ambaye naye anahitaji uangalizi maalumu.

“Nimetamani sana watoto wangu wasome Buguruni kwa sababu ni kama dakika saba tu kufika shuleni…ninaweza kuwashika mkono na kuwapeleka…nasikitika kwa kuwa shule ya msingi Buguruni Viziwi haipo mbali na ninakoishi, lakini watoto wangu hawakupata bahati ya kuifaidi,” Mwanahawa anasema kwa huzuni.

Anaendelea kusema, “wakati mwingine nahisi kuwa umasikini wangu ndio unaosababisha watoto wangu wakose nafasi ya masomo. Kama ningekuwa na uwezo wa kifedha au cheo fulani wanangu wangepewa kipaumbele kwa kuwa ni wakazi wa Buguruni, lakini wote wawili wamekosa shule…nasikitika sana.”

Mwanamke huyo mjane, asiyekuwa na uhakika kwa kupata mlo wa siku anawaomba wasamaria wema na taasisi mbalimbali zijitokeze na kusaidia kugharamia masomo ya watoto wake ili waweze kupata elimu itakayowasaidia maishani.

“Bila elimu watoto hao hawataweza kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii na badala yake watakuwa mzigo…wataishi katika hali ya ufukara kwa sababu mimi mwenyewe sina uwezo wa kuwajengea msingi imara kwa maisha yao ya baadaye,” anaeleza.

Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania, Matilda Ngonyani anasema uongozi wa shule hiyo utakuwa mstari wa mbele kujiunga na taasisi na wasamaria wema watakaojitokeza kutoa msaada kwa watoto hao.

“Tumepokea kwa mshtuko taarifa kuhusu watoto hao…sisi tutawasaidia kwa kuwa kila mtoto ana haki ya kusoma kulingana na mahitaji ya ubongo wake…ikiwa kweli watafaa katika darasa la viziwi tutawapokea ingawa nafasi ni finyu,” anaema Ngonyani.

Anafahamisha kuwa shule hiyo inayosimamiwa na Chama cha Viziwi Tanzania, haibagui watoto viziwi lakini inakabiliwa na changamoto kubwa kwa sababu haiwezi kuchukua wanafunzi zaidi ya 30 kwa mwaka.

“Kila mwaka tunachukua wanafunzi 20 kwa darasa la kwanza na 10 wa shule ya awali…wanafunzi hao wanatoka sehemu mbalimbali nchini na tunawagharamia kila kitu…wazazi wao hawalipii chochote,” Ngonyani anasema.

Hata hivyo, anasema ufinyu wa nafasi katika shule hiyo siyo sababu ya kutowapatia Asia na Ahmed nafasi ya kusoma katika shule hiyo na ameahidi kufuatilia ili kubaini tatizo.

“Huenda walikosa nafasi kwa sababu wana tatizo zaidi ya moja, mfano taahiri ya akili na mtindio wa ubongo, kutokuona au ulemavu mwingine ambao unasababisha wasiendane na kundi la viziwi,” Ngonyani anaeleza.

Ngonyani, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi inayomiliki shule hiyo, anaeleza kuwa shule hiyo inafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaopata nafasi katika shule hiyo ni kundi la viziwi pekee ili kuepuka vikwazo vinavyosababishwa na watoto wenye ulemavu zaidi ya mmoja.

“Mfano tukichukua mtoto mwenye ulemavu wa taahira ya akili na mtindio wa ubongo au mwenye otizim atakuwa anafanya mambo tofauti na wenzake hivyo watoto wengine wataacha kuzingatia masomo na kuanza kudadisi mwenendo wa mwenzao anayefanya mambo tofauti…, jambo hilo linatufanya tuwe makini sana wakati wa kuchukua wanafunzi viziwi,” Ngonyani anaeleza.

Anafafanua baadhi ya watoto wenye taahira ya akili na mtindio wa ubongo au wenye otizim wana tabia ya kukaa kimya au kukaidi wanapoitwa, jambo linalosababisha wazazi waamini kuwa wana ulemavu unaosababisha washindwe kusikia na kuzungumza.

Ili kubaini tatizo hilo watoto wanaopelekwa katika shule hiyo hufanyiwa uchunguzi wa masikio ili kupima uwezo wao wa kusikia. Pia hufanyiwa majaribio mengine kama vile kuchagua rangi, kupanga vitu mbalimbali kwa kufuata ukubwa na kuchora mstari.

Kwa kuwa watoto hao ni wadogo tunawapa majaribio mepesi ili kutambua matatizo yao. Mfano wataalamu wanapanga herufi au maumbo yenye rangi mbalimbali ambapo mtoto anapaswa kuigizia akichagua herufi tofauti au rangi tofauti na wataalamu wanatambua ana matatizo ya macho au tatizo jingine mbali na kutosikia.

“Unaweza kuchora mstari na kumuambia mtoto achore anachokiona…badala ya kuchora mstari anaandika nukta nukta au anaambiwa aweke maumbo kwenye mashimo kulingana na ukubwa anachukua umbo kubwa analazimisha liingie kwenye shimo dogo….hapo wataalamu wanabaini kuwa watoto hawa sio viziwi ila wana matatizo ya ubongo ambayo yanawakosesha mawasiliano,” Ngonyani anafafanua.

Hata hivyo, anasisitiza hivi sasa Tanzania ina vitengo mbalimbali vya elimu maalumu wa watoto wenye ulemavu hivyo Asia na Ahmed hawana sababu ya kukosa elimu.

“Kwa kuwa hakuna binadamu aliye kamili inawezekana hata sisi tulipitiwa…tumelichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa …ikiwa ni viziwi tutawapatia nafasi…Asia anaweza kujiunga na shule ya ufundi na Ahmed akaingia shule ya msingi…hata wakiwa na tatizo lingine tutamshauri mama yao na kumwelekeza pa kuwapeleka,” Ngonyani anasema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Viziwi Buguruni, Said Mkude anasema, anaomba Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza vitengo vya elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki ya kusoma.

Mkude anafahamisha kuwa amewasilisha maombi yake kwa Ofisa Elimu wilaya ya Ilala na kumfahamisha kuwa ipo haja ya kuongeza vitengo vya watoto viziwi katika shule za kawaida kwa kuwa shule yake haiwezi kuchukua watoto wote wanaomba nafasi za masomo.

Akitoa mfano Mkude anasema kwa mwaka huu, watoto 78 waliombewa nafasi ya kujiunga na darasa la kwanza, kati yao wavulana 47 na wasichana 31. Waliohudhuria usaili ni 53 kati yao wavulala 33 na wasichana 20.

“Kati ya wavulana 33 waliochaguliwa ni 9 na kati ya wasichana 20 waliochaguliwa ni 11 hivyo kukamilisha idadi ya wanafunzi 20 wa darasa la kwanza lenye michipuo miwili….pia tumechukua wavulana sita na wasichana wanne wa darasa la awali. Hivyo watoto zaidi ya 23 waliofanya usaili wamekosa nafasi,” Mkude anaeleza.

Anaendelea kusema,"Tukijumlisha na watoto ambao hawakufika kwenye usaili ni dhahiri kuwa wastani wa watoto viziwi 45 wanakosa nafasi za masomo baada ya wazazi wao kuonyesha nia ya kuwasomesa……hivyo Serikali na wadau wa elimu wanapaswa kulipa uzito jambo hili na kulitafutia ufumbuzi ili watoto wenye ulemavu waweze kupata elimu.”

Ikiwa Serikali ina dhamira ya kweli ya kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanasoma, inapaswa kufuata ushauri uliotolewa na shule vya Viziwi Bunguruni na kuongeza vitengo vya elimu maalum kwa watoto wenye ulemavu nchini.

Wanaotaka kuwasaidia Asia na Ahmed wawasiliane na mama yao kwa simu namba 0754 364 085.

My take:

- Nimeguswa na habari ya watoto hawa na ninataka kuwasaidia kwa namna fulani ili mwaka mpya wa masomo unapoanza waweze kupata nafasi ya kwenda shule.

- Nataka nifanye kitu cha kusaidia wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka; kama zawadi ya Krismasi na Mwaka mpya.

- Kama kuna watu wanataka tushirikiane kuwasaidia wao au kusaidia shule ya Viziwi kwa ujumla yake naomba tuwasiliane na mawazo yanakaribishwa.

- Endapo kutakuwa na watu wako tayari ninaweza kushikirikiana na gazeti la Daily News kuhakikisha kuwa watoto hawa wanapata msaada unaohitajika. Ninachotaka kujua tu ni kama naweza kuungwa mkono na watu kadhaa ili nilifuatilie. Vinginevyo, tusubiri wazungu waje kuwasaidia.
- Tunaweza kuwapa samaki wakala kwa siku moja au tukatengeneza bwawa wakala na wengine au tukawafundisha kuvua!
 
Nimeguswa na habari nzima kuhusu watoto hawa na kilio cha mama yao tell it all.

Kuna darasa la sanaa ambalo lipo mahala fulani ammbapo wanaweza kupata refresher ya kuwaongezea ujuzi na warm life. kama wakianza shule au wakishindwa kuanza shule haitawazuia kujifunza sanaa kwa stadi yao inavyowezekana.

Niko tayari kuorganize darasa maalum kwao hata kama ni nyumbani once a week ambapo mwalimu atakua anakwenda kuwafundisha na kuangalia posibility ya kupata vifaa vya sanaa.

Nilishawahi pata nafasi ya kufundisha viziwi shughuli fulani ya sanaa ambapo waliweza kufanya presentation nzuri ya kushangaza.

Sin fedha ila nina ujuzi wa kuwapatia
 
Hivi darisalama nzima kuna skuli moja tu ya watu wenye ulemavu wa ukiziwi? Hawa ni watoto wawili ambao mama lao kaamua kusema je ni wangapi huko Gezaulole ambao wanakosa elimu bila sababu za maana!?

Mtanganyika, hapa pia unasemaje? je si wajibu wa serikali kuhakikisha yakuwa kwamba wananchi wake wanapata huduma muhimu regardless ya deficit zao za kimaumbile?

Well, mie nakuunga mkono MKJJ. Kama ni $$ nitajipiga hapa na pale kwani tax returns zinakaribia!!!. Hakuna kitu muhimu kama kuwa na Elimu, mtu asiwe nayo kwa uzembe wake na sio kuwa denied.
Msanii, wazo lako la kuwafunza sanaa ni zuri.....lakini hiyo mie naona iwe kama nyongeza juu ya elimu ya kawaida tuliyopata sisi sote tena kwa bei ya dezo.

Natoa pole zangu kwa familia, nipo moved na ujasiri wa mama kuliweka hili hadharani, poleni sana. Inshallah, pamoja tunaweza kufanya kitu positive hapa zaidi ya kupiga soga la madini na kambi ya wanyamwezi.
 
Nafikiri kwa mara nyingine tunaweza kufanya ushirikiano kati ya Jambo Forums na Daily News au mchango utoke na kuwa wa Jambo Forums kwenda familia hiyo. Kama tukipata mawazo ya watu wachache kuunga mkono nitawasiliana aidha na Daily News au gazeti jingine ili liwe go between kati yetu na familia hiyo. Hata hivyo najua wakati huu wengi mna majukumu mengi zaidi hivyo sitaona ubaya kujibana mimi mwenyewe na shemeji yenu mkubwa.
 
Mkjj pokea tano kwa kutuletea habari hizi za kusikitisha.

Inauma zaidi ukifikiria kuwa hawa watoto na mama yao ambaye ni mjane wanaishi Dar es salaam, ambako ndo kumeendelea kuliko sehemu ingine yeyote Tanzania. Je watoto kama hawa ambao wanaishi vijijini wapo kwenye mazingira gani?

Pili hii inatokea ati baada ya miaka 46 ya uhuru!!!, Je Uhuru wa nchi yetu umewasaidia vipi hawa watanzaia mwenzetu?

Je, iweje mtoto kiziwi achanganywe kwenye darasa na watoto mataahira?-hii ni kashfa nzito. Kama huyo mzazi alivyosema, labda umaskini wa huyu mama ndiyo unaochangia serikali kutowaona hao watoto!
 
Mkjj

Nami naunga mkono, A am ready to suport if utaoganise namna ya kushiriki.
 
Alia kwa watoto wake wawili walemavu kukosa masomo
Kaanaeli Kaale
HabariLeo; Thursday,November 29, 2007 @00:07

910c1396067a.bmp

Mwanahawa Juma (katikati) akiwa na watoto wake Asia na Ahmed.
“INGAWA elimu ni haki ya mtoto na msingi kwa kila mtoto, Asia Kawi na mdogo wake anaitwa Ahmed, wamekosa nafasi ya kujiunga na shule kutokana na hali yao ya ulemavu,” anasimulia mama yao Mwanahawa Juma.

Mwanahawa anasema watoto wake wamekosa nafasi ya kujiunga na shule ya viziwi, jambo linalosababisha wakose elimu ambayo ingewasaidia maishani.

Watoto hao wenye uchu wa elimu huamka saa 11.30 alfajiri na kuvaa sare za shule kisha kukaa sebuleni huku wakinyoosha vidole kuelekea mlango ili kuashiria kuwa wanataka kutoka nje.

Wanapofunguliwa milango, watoto hukaa barazani na kuwapungia watoto wenzao wanaopita eneo hilo kuelekea shuleni. Watoto hao wanaozungumza kwa lugha ya ishara kila mara wanamsihi mama yao awapeleke shule.

“Jambo hili huwa linaniumiza na ni pigo kubwa kwa watoto wangu….walizaliwa wakiwa wazima kisha wakaugua na kuteseka kipindi chote cha utoto wao…na sasa wanaendelea kuteseka kwa kukosa nafasi ya masomo,” Mwanahawa anaeleza akiwa anabubujikwa na machozi.

Hivi sasa Asia ana miaka 15 lakini ameshindwa kupata elimu sahihi kulingana na ulemavu wake, kwani mama yake amejitahidi kumtafutia shule ya elimu maalumu kwa viziwi bila mafanikio.

Mwanahawa anasema mtoto huyo alipotimiza umri wa kwenda shule alimpeleka katika Shule ya Msingi Viziwi Buguruni lakini hakufanikiwa kupata nafasi ya masomo.

“Nilikwenda kumwandikisha katika shule ya msingi Viziwi Buguruni akajumuishwa na watoto wengine kwa ajili ya usaili na baadaye uongozi wa shule ulinijulisha kuwa amekosa nafasi,” Mwanahawa anasema kwa huzuni.

Baada ya kubaini kuwa mtoto wake amekosa nafasi katika shule ya elimu maalumu kwa viziwi, aliamua kwenda kumuandikisha katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. Mwanahawa alikuwa akimpeleka mwanawe shuleni kila siku kwa kipindi cha miaka minne, lakini mtoto huyo hakuwa anaelewa kitu kwa sababu hakuwa anafundishwa kwa lugha ya ishara.

“Asia alichanganywa na watoto wenye taahira ya akili na mtindio wa ubongo na kuhudhuria masomo kwa miaka minne lakini alikuwa haelewi kitu chochote, hata hivyo nilibaini kuwa akifundishwa kwa lugha ya ishara anaelewa,” Mwanahawa anaeleza.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo anahitaji elimu maalumu kwa watoto viziwi, aliamua kutoendelea kumpeleka shule ya Uhuru Mchanganyiko kutokana na ukweli kuwa alikuwa akitembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma ambayo haipo.

Anasema alirudi tena katika shule ya viziwi Buguruni kuomba nafasi kwa ajili ya Asia lakini hakufanikiwa, jambo linalosababisha mtoto huyo kukaa nyumbani.

“Ahmed alipofikisha umri wa kwenda shule nilikwenda tena katika shule ya Msingi Viziwi Buguruni kuomba nafasi…walimwita kufanya usaili kisha wananiambia kuwa hakuna nafasi kwa kuwa shule hiyo inachukua wanafunzi wachache,” Mwanahawa anaeleza.

Anadai kuwa ameomba nafasi hiyo kwa miaka minne mfululizo lakini hakufanikiwa, jambo linalosababisha watoto wote wawili kukaa nyumbani baada ya kukosa nafasi katika shule ya elimu maalumu kwa viziwi.

Anadai baada ya kwenda katika shule hiyo mara kwa mara walimshauri ampeleke Ahmed katika shule ya Msingi Mugabe ambako kuna kitengo cha elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza.

Hata hivyo, Mwanahawa anasema ameshindwa kumpeleka mtoto huyo katika shule iliyopo Sinza kwa kuwa kuu mbili. Kwanza hana kipato kitakachomwezesha kugharamia nauli ya kumpeleka shule kila siku, pili ana mtoto mwingine mlemavu ambaye naye anahitaji uangalizi maalumu.

“Nimetamani sana watoto wangu wasome Buguruni kwa sababu ni kama dakika saba tu kufika shuleni…ninaweza kuwashika mkono na kuwapeleka…nasikitika kwa kuwa shule ya msingi Buguruni Viziwi haipo mbali na ninakoishi, lakini watoto wangu hawakupata bahati ya kuifaidi,” Mwanahawa anasema kwa huzuni.

Anaendelea kusema, “wakati mwingine nahisi kuwa umasikini wangu ndio unaosababisha watoto wangu wakose nafasi ya masomo. Kama ningekuwa na uwezo wa kifedha au cheo fulani wanangu wangepewa kipaumbele kwa kuwa ni wakazi wa Buguruni, lakini wote wawili wamekosa shule…nasikitika sana.”

Mwanamke huyo mjane, asiyekuwa na uhakika kwa kupata mlo wa siku anawaomba wasamaria wema na taasisi mbalimbali zijitokeze na kusaidia kugharamia masomo ya watoto wake ili waweze kupata elimu itakayowasaidia maishani.

“Bila elimu watoto hao hawataweza kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii na badala yake watakuwa mzigo…wataishi katika hali ya ufukara kwa sababu mimi mwenyewe sina uwezo wa kuwajengea msingi imara kwa maisha yao ya baadaye,” anaeleza.

Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania, Matilda Ngonyani anasema uongozi wa shule hiyo utakuwa mstari wa mbele kujiunga na taasisi na wasamaria wema watakaojitokeza kutoa msaada kwa watoto hao.

“Tumepokea kwa mshtuko taarifa kuhusu watoto hao…sisi tutawasaidia kwa kuwa kila mtoto ana haki ya kusoma kulingana na mahitaji ya ubongo wake…ikiwa kweli watafaa katika darasa la viziwi tutawapokea ingawa nafasi ni finyu,” anaema Ngonyani.

Anafahamisha kuwa shule hiyo inayosimamiwa na Chama cha Viziwi Tanzania, haibagui watoto viziwi lakini inakabiliwa na changamoto kubwa kwa sababu haiwezi kuchukua wanafunzi zaidi ya 30 kwa mwaka.

“Kila mwaka tunachukua wanafunzi 20 kwa darasa la kwanza na 10 wa shule ya awali…wanafunzi hao wanatoka sehemu mbalimbali nchini na tunawagharamia kila kitu…wazazi wao hawalipii chochote,” Ngonyani anasema.

Hata hivyo, anasema ufinyu wa nafasi katika shule hiyo siyo sababu ya kutowapatia Asia na Ahmed nafasi ya kusoma katika shule hiyo na ameahidi kufuatilia ili kubaini tatizo.

“Huenda walikosa nafasi kwa sababu wana tatizo zaidi ya moja, mfano taahiri ya akili na mtindio wa ubongo, kutokuona au ulemavu mwingine ambao unasababisha wasiendane na kundi la viziwi,” Ngonyani anaeleza.

Ngonyani, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi inayomiliki shule hiyo, anaeleza kuwa shule hiyo inafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaopata nafasi katika shule hiyo ni kundi la viziwi pekee ili kuepuka vikwazo vinavyosababishwa na watoto wenye ulemavu zaidi ya mmoja.

“Mfano tukichukua mtoto mwenye ulemavu wa taahira ya akili na mtindio wa ubongo au mwenye otizim atakuwa anafanya mambo tofauti na wenzake hivyo watoto wengine wataacha kuzingatia masomo na kuanza kudadisi mwenendo wa mwenzao anayefanya mambo tofauti…, jambo hilo linatufanya tuwe makini sana wakati wa kuchukua wanafunzi viziwi,” Ngonyani anaeleza.

Anafafanua baadhi ya watoto wenye taahira ya akili na mtindio wa ubongo au wenye otizim wana tabia ya kukaa kimya au kukaidi wanapoitwa, jambo linalosababisha wazazi waamini kuwa wana ulemavu unaosababisha washindwe kusikia na kuzungumza.

Ili kubaini tatizo hilo watoto wanaopelekwa katika shule hiyo hufanyiwa uchunguzi wa masikio ili kupima uwezo wao wa kusikia. Pia hufanyiwa majaribio mengine kama vile kuchagua rangi, kupanga vitu mbalimbali kwa kufuata ukubwa na kuchora mstari.

Kwa kuwa watoto hao ni wadogo tunawapa majaribio mepesi ili kutambua matatizo yao. Mfano wataalamu wanapanga herufi au maumbo yenye rangi mbalimbali ambapo mtoto anapaswa kuigizia akichagua herufi tofauti au rangi tofauti na wataalamu wanatambua ana matatizo ya macho au tatizo jingine mbali na kutosikia.

“Unaweza kuchora mstari na kumuambia mtoto achore anachokiona…badala ya kuchora mstari anaandika nukta nukta au anaambiwa aweke maumbo kwenye mashimo kulingana na ukubwa anachukua umbo kubwa analazimisha liingie kwenye shimo dogo….hapo wataalamu wanabaini kuwa watoto hawa sio viziwi ila wana matatizo ya ubongo ambayo yanawakosesha mawasiliano,” Ngonyani anafafanua.

Hata hivyo, anasisitiza hivi sasa Tanzania ina vitengo mbalimbali vya elimu maalumu wa watoto wenye ulemavu hivyo Asia na Ahmed hawana sababu ya kukosa elimu.

“Kwa kuwa hakuna binadamu aliye kamili inawezekana hata sisi tulipitiwa…tumelichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa …ikiwa ni viziwi tutawapatia nafasi…Asia anaweza kujiunga na shule ya ufundi na Ahmed akaingia shule ya msingi…hata wakiwa na tatizo lingine tutamshauri mama yao na kumwelekeza pa kuwapeleka,” Ngonyani anasema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Viziwi Buguruni, Said Mkude anasema, anaomba Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza vitengo vya elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki ya kusoma.

Mkude anafahamisha kuwa amewasilisha maombi yake kwa Ofisa Elimu wilaya ya Ilala na kumfahamisha kuwa ipo haja ya kuongeza vitengo vya watoto viziwi katika shule za kawaida kwa kuwa shule yake haiwezi kuchukua watoto wote wanaomba nafasi za masomo.

Akitoa mfano Mkude anasema kwa mwaka huu, watoto 78 waliombewa nafasi ya kujiunga na darasa la kwanza, kati yao wavulana 47 na wasichana 31. Waliohudhuria usaili ni 53 kati yao wavulala 33 na wasichana 20.

“Kati ya wavulana 33 waliochaguliwa ni 9 na kati ya wasichana 20 waliochaguliwa ni 11 hivyo kukamilisha idadi ya wanafunzi 20 wa darasa la kwanza lenye michipuo miwili….pia tumechukua wavulana sita na wasichana wanne wa darasa la awali. Hivyo watoto zaidi ya 23 waliofanya usaili wamekosa nafasi,” Mkude anaeleza.

Anaendelea kusema,"Tukijumlisha na watoto ambao hawakufika kwenye usaili ni dhahiri kuwa wastani wa watoto viziwi 45 wanakosa nafasi za masomo baada ya wazazi wao kuonyesha nia ya kuwasomesa……hivyo Serikali na wadau wa elimu wanapaswa kulipa uzito jambo hili na kulitafutia ufumbuzi ili watoto wenye ulemavu waweze kupata elimu.”

Ikiwa Serikali ina dhamira ya kweli ya kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanasoma, inapaswa kufuata ushauri uliotolewa na shule vya Viziwi Bunguruni na kuongeza vitengo vya elimu maalum kwa watoto wenye ulemavu nchini.

Wanaotaka kuwasaidia Asia na Ahmed wawasiliane na mama yao kwa simu namba 0754 364 085.

My take:

- Nimeguswa na habari ya watoto hawa na ninataka kuwasaidia kwa namna fulani ili mwaka mpya wa masomo unapoanza waweze kupata nafasi ya kwenda shule.

- Nataka nifanye kitu cha kusaidia wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka; kama zawadi ya Krismasi na Mwaka mpya.

- Kama kuna watu wanataka tushirikiane kuwasaidia wao au kusaidia shule ya Viziwi kwa ujumla yake naomba tuwasiliane na mawazo yanakaribishwa.

- Endapo kutakuwa na watu wako tayari ninaweza kushikirikiana na gazeti la Daily News kuhakikisha kuwa watoto hawa wanapata msaada unaohitajika. Ninachotaka kujua tu ni kama naweza kuungwa mkono na watu kadhaa ili nilifuatilie. Vinginevyo, tusubiri wazungu waje kuwasaidia.
- Tunaweza kuwapa samaki wakala kwa siku moja au tukatengeneza bwawa wakala na wengine au tukawafundisha kuvua!

kuna uwezekano wa kupata contact za hawa watu au hiyo shule ya viziwi?, kwani kuna watu naweza nikawapa hii habari na nina imani wanaweza wakakubali kusaidia ila tatizo lao wanakuwa hawataki mtu wa kati na pia wana imani ya kwamba msaada hutolewa kwa siri. kama inawezekana basi naomba ,hata kama ukini PM. tnx in advance
 
Washauri wa set account number na CRDB, i think majority of us we can make difference on this case. However we need check and balance in order to make sure the fund is utilize wise and as recommended by majority of us.

So tell them to set CRDB tanzanite account which will be easy for most of us who are in abroad. I believe we need to take care this now.
Thanks
 
That's wasup! good idea, since each and everyone of us will remain anony...plus no need of doin' this thru MKJJ.
 
YNIM, you don't have to do it through me. Nilitaka kutengeneza hiyo mechanism ya watu kusaidia moja kwa moja kwa familia. Kama mtu anaweza kufanya hivyo yeye mwenyewe well and good; lakini watu wakitaka kukusanya nguvu is even better but in whatever case hamu yangu ya kuona familia hii inasaidiwa itakuwa imetimizwa. So, friends go ahead and help the family and these kids now that is whats up!!
 
Mkjj,
trust me bro, nilikuwa na-joke tu kidogo......issue ni kusaidia hao watoto na mama lao, whatever works.!!! Sometimes you are too serious, utajapata HTN bure........eazy kaka, have a nice weekend na unafanyakazi nzuri!!!.Kudos.
 
Nimekupata mzee.. yeah.. I need to relax; sorry my wheelchair had some issues now i need a new one.. daymn.. the snow!
 
Washauri wa set account number na CRDB, i think majority of us we can make difference on this case. However we need check and balance in order to make sure the fund is utilize wise and as recommended by majority of us.

So tell them to set CRDB tanzanite account which will be easy for most of us who are in abroad. I believe we need to take care this now.
Thanks

True Mtanganyika, let's have Bank Account Details.
Nina uhakika watu watachangia. Ninafahamu wako wengi wanao-face the same challenge lakini hawa wamejitokeza hadharani kuomba msaada. Hivyo tunawajibu wa kuwasadia kama Watanzania na binadamu wenzetu . Wakati huo huo tuiombe Serikali ifanye juhudi za makusudi ku-invest kwenye shule za watu ambao ni Physically challenged.

Thanks MKjj for bringing forward the issue.
 
Back
Top Bottom