Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,399
- 39,548
Alia kwa watoto wake wawili walemavu kukosa masomo
Kaanaeli Kaale
HabariLeo; Thursday,November 29, 2007 @00:07
Mwanahawa Juma (katikati) akiwa na watoto wake Asia na Ahmed.
INGAWA elimu ni haki ya mtoto na msingi kwa kila mtoto, Asia Kawi na mdogo wake anaitwa Ahmed, wamekosa nafasi ya kujiunga na shule kutokana na hali yao ya ulemavu, anasimulia mama yao Mwanahawa Juma.
Mwanahawa anasema watoto wake wamekosa nafasi ya kujiunga na shule ya viziwi, jambo linalosababisha wakose elimu ambayo ingewasaidia maishani.
Watoto hao wenye uchu wa elimu huamka saa 11.30 alfajiri na kuvaa sare za shule kisha kukaa sebuleni huku wakinyoosha vidole kuelekea mlango ili kuashiria kuwa wanataka kutoka nje.
Wanapofunguliwa milango, watoto hukaa barazani na kuwapungia watoto wenzao wanaopita eneo hilo kuelekea shuleni. Watoto hao wanaozungumza kwa lugha ya ishara kila mara wanamsihi mama yao awapeleke shule.
Jambo hili huwa linaniumiza na ni pigo kubwa kwa watoto wangu .walizaliwa wakiwa wazima kisha wakaugua na kuteseka kipindi chote cha utoto wao na sasa wanaendelea kuteseka kwa kukosa nafasi ya masomo, Mwanahawa anaeleza akiwa anabubujikwa na machozi.
Hivi sasa Asia ana miaka 15 lakini ameshindwa kupata elimu sahihi kulingana na ulemavu wake, kwani mama yake amejitahidi kumtafutia shule ya elimu maalumu kwa viziwi bila mafanikio.
Mwanahawa anasema mtoto huyo alipotimiza umri wa kwenda shule alimpeleka katika Shule ya Msingi Viziwi Buguruni lakini hakufanikiwa kupata nafasi ya masomo.
Nilikwenda kumwandikisha katika shule ya msingi Viziwi Buguruni akajumuishwa na watoto wengine kwa ajili ya usaili na baadaye uongozi wa shule ulinijulisha kuwa amekosa nafasi, Mwanahawa anasema kwa huzuni.
Baada ya kubaini kuwa mtoto wake amekosa nafasi katika shule ya elimu maalumu kwa viziwi, aliamua kwenda kumuandikisha katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. Mwanahawa alikuwa akimpeleka mwanawe shuleni kila siku kwa kipindi cha miaka minne, lakini mtoto huyo hakuwa anaelewa kitu kwa sababu hakuwa anafundishwa kwa lugha ya ishara.
Asia alichanganywa na watoto wenye taahira ya akili na mtindio wa ubongo na kuhudhuria masomo kwa miaka minne lakini alikuwa haelewi kitu chochote, hata hivyo nilibaini kuwa akifundishwa kwa lugha ya ishara anaelewa, Mwanahawa anaeleza.
Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo anahitaji elimu maalumu kwa watoto viziwi, aliamua kutoendelea kumpeleka shule ya Uhuru Mchanganyiko kutokana na ukweli kuwa alikuwa akitembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma ambayo haipo.
Anasema alirudi tena katika shule ya viziwi Buguruni kuomba nafasi kwa ajili ya Asia lakini hakufanikiwa, jambo linalosababisha mtoto huyo kukaa nyumbani.
Ahmed alipofikisha umri wa kwenda shule nilikwenda tena katika shule ya Msingi Viziwi Buguruni kuomba nafasi walimwita kufanya usaili kisha wananiambia kuwa hakuna nafasi kwa kuwa shule hiyo inachukua wanafunzi wachache, Mwanahawa anaeleza.
Anadai kuwa ameomba nafasi hiyo kwa miaka minne mfululizo lakini hakufanikiwa, jambo linalosababisha watoto wote wawili kukaa nyumbani baada ya kukosa nafasi katika shule ya elimu maalumu kwa viziwi.
Anadai baada ya kwenda katika shule hiyo mara kwa mara walimshauri ampeleke Ahmed katika shule ya Msingi Mugabe ambako kuna kitengo cha elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuzungumza.
Hata hivyo, Mwanahawa anasema ameshindwa kumpeleka mtoto huyo katika shule iliyopo Sinza kwa kuwa kuu mbili. Kwanza hana kipato kitakachomwezesha kugharamia nauli ya kumpeleka shule kila siku, pili ana mtoto mwingine mlemavu ambaye naye anahitaji uangalizi maalumu.
Nimetamani sana watoto wangu wasome Buguruni kwa sababu ni kama dakika saba tu kufika shuleni ninaweza kuwashika mkono na kuwapeleka nasikitika kwa kuwa shule ya msingi Buguruni Viziwi haipo mbali na ninakoishi, lakini watoto wangu hawakupata bahati ya kuifaidi, Mwanahawa anasema kwa huzuni.
Anaendelea kusema, wakati mwingine nahisi kuwa umasikini wangu ndio unaosababisha watoto wangu wakose nafasi ya masomo. Kama ningekuwa na uwezo wa kifedha au cheo fulani wanangu wangepewa kipaumbele kwa kuwa ni wakazi wa Buguruni, lakini wote wawili wamekosa shule nasikitika sana.
Mwanamke huyo mjane, asiyekuwa na uhakika kwa kupata mlo wa siku anawaomba wasamaria wema na taasisi mbalimbali zijitokeze na kusaidia kugharamia masomo ya watoto wake ili waweze kupata elimu itakayowasaidia maishani.
Bila elimu watoto hao hawataweza kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kijamii na badala yake watakuwa mzigo wataishi katika hali ya ufukara kwa sababu mimi mwenyewe sina uwezo wa kuwajengea msingi imara kwa maisha yao ya baadaye, anaeleza.
Katibu wa Chama cha Viziwi Tanzania, Matilda Ngonyani anasema uongozi wa shule hiyo utakuwa mstari wa mbele kujiunga na taasisi na wasamaria wema watakaojitokeza kutoa msaada kwa watoto hao.
Tumepokea kwa mshtuko taarifa kuhusu watoto hao sisi tutawasaidia kwa kuwa kila mtoto ana haki ya kusoma kulingana na mahitaji ya ubongo wake ikiwa kweli watafaa katika darasa la viziwi tutawapokea ingawa nafasi ni finyu, anaema Ngonyani.
Anafahamisha kuwa shule hiyo inayosimamiwa na Chama cha Viziwi Tanzania, haibagui watoto viziwi lakini inakabiliwa na changamoto kubwa kwa sababu haiwezi kuchukua wanafunzi zaidi ya 30 kwa mwaka.
Kila mwaka tunachukua wanafunzi 20 kwa darasa la kwanza na 10 wa shule ya awali wanafunzi hao wanatoka sehemu mbalimbali nchini na tunawagharamia kila kitu wazazi wao hawalipii chochote, Ngonyani anasema.
Hata hivyo, anasema ufinyu wa nafasi katika shule hiyo siyo sababu ya kutowapatia Asia na Ahmed nafasi ya kusoma katika shule hiyo na ameahidi kufuatilia ili kubaini tatizo.
Huenda walikosa nafasi kwa sababu wana tatizo zaidi ya moja, mfano taahiri ya akili na mtindio wa ubongo, kutokuona au ulemavu mwingine ambao unasababisha wasiendane na kundi la viziwi, Ngonyani anaeleza.
Ngonyani, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi inayomiliki shule hiyo, anaeleza kuwa shule hiyo inafanya uchunguzi wa kina kuhakikisha wanaopata nafasi katika shule hiyo ni kundi la viziwi pekee ili kuepuka vikwazo vinavyosababishwa na watoto wenye ulemavu zaidi ya mmoja.
Mfano tukichukua mtoto mwenye ulemavu wa taahira ya akili na mtindio wa ubongo au mwenye otizim atakuwa anafanya mambo tofauti na wenzake hivyo watoto wengine wataacha kuzingatia masomo na kuanza kudadisi mwenendo wa mwenzao anayefanya mambo tofauti , jambo hilo linatufanya tuwe makini sana wakati wa kuchukua wanafunzi viziwi, Ngonyani anaeleza.
Anafafanua baadhi ya watoto wenye taahira ya akili na mtindio wa ubongo au wenye otizim wana tabia ya kukaa kimya au kukaidi wanapoitwa, jambo linalosababisha wazazi waamini kuwa wana ulemavu unaosababisha washindwe kusikia na kuzungumza.
Ili kubaini tatizo hilo watoto wanaopelekwa katika shule hiyo hufanyiwa uchunguzi wa masikio ili kupima uwezo wao wa kusikia. Pia hufanyiwa majaribio mengine kama vile kuchagua rangi, kupanga vitu mbalimbali kwa kufuata ukubwa na kuchora mstari.
Kwa kuwa watoto hao ni wadogo tunawapa majaribio mepesi ili kutambua matatizo yao. Mfano wataalamu wanapanga herufi au maumbo yenye rangi mbalimbali ambapo mtoto anapaswa kuigizia akichagua herufi tofauti au rangi tofauti na wataalamu wanatambua ana matatizo ya macho au tatizo jingine mbali na kutosikia.
Unaweza kuchora mstari na kumuambia mtoto achore anachokiona badala ya kuchora mstari anaandika nukta nukta au anaambiwa aweke maumbo kwenye mashimo kulingana na ukubwa anachukua umbo kubwa analazimisha liingie kwenye shimo dogo .hapo wataalamu wanabaini kuwa watoto hawa sio viziwi ila wana matatizo ya ubongo ambayo yanawakosesha mawasiliano, Ngonyani anafafanua.
Hata hivyo, anasisitiza hivi sasa Tanzania ina vitengo mbalimbali vya elimu maalumu wa watoto wenye ulemavu hivyo Asia na Ahmed hawana sababu ya kukosa elimu.
Kwa kuwa hakuna binadamu aliye kamili inawezekana hata sisi tulipitiwa tumelichukulia suala hilo kwa uzito mkubwa ikiwa ni viziwi tutawapatia nafasi Asia anaweza kujiunga na shule ya ufundi na Ahmed akaingia shule ya msingi hata wakiwa na tatizo lingine tutamshauri mama yao na kumwelekeza pa kuwapeleka, Ngonyani anasema.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Viziwi Buguruni, Said Mkude anasema, anaomba Serikali iangalie uwezekano wa kuongeza vitengo vya elimu maalumu kwa watoto wenye ulemavu ili kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata haki ya kusoma.
Mkude anafahamisha kuwa amewasilisha maombi yake kwa Ofisa Elimu wilaya ya Ilala na kumfahamisha kuwa ipo haja ya kuongeza vitengo vya watoto viziwi katika shule za kawaida kwa kuwa shule yake haiwezi kuchukua watoto wote wanaomba nafasi za masomo.
Akitoa mfano Mkude anasema kwa mwaka huu, watoto 78 waliombewa nafasi ya kujiunga na darasa la kwanza, kati yao wavulana 47 na wasichana 31. Waliohudhuria usaili ni 53 kati yao wavulala 33 na wasichana 20.
Kati ya wavulana 33 waliochaguliwa ni 9 na kati ya wasichana 20 waliochaguliwa ni 11 hivyo kukamilisha idadi ya wanafunzi 20 wa darasa la kwanza lenye michipuo miwili .pia tumechukua wavulana sita na wasichana wanne wa darasa la awali. Hivyo watoto zaidi ya 23 waliofanya usaili wamekosa nafasi, Mkude anaeleza.
Anaendelea kusema,"Tukijumlisha na watoto ambao hawakufika kwenye usaili ni dhahiri kuwa wastani wa watoto viziwi 45 wanakosa nafasi za masomo baada ya wazazi wao kuonyesha nia ya kuwasomesa hivyo Serikali na wadau wa elimu wanapaswa kulipa uzito jambo hili na kulitafutia ufumbuzi ili watoto wenye ulemavu waweze kupata elimu.
Ikiwa Serikali ina dhamira ya kweli ya kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanasoma, inapaswa kufuata ushauri uliotolewa na shule vya Viziwi Bunguruni na kuongeza vitengo vya elimu maalum kwa watoto wenye ulemavu nchini.
Wanaotaka kuwasaidia Asia na Ahmed wawasiliane na mama yao kwa simu namba 0754 364 085.
My take:
- Nimeguswa na habari ya watoto hawa na ninataka kuwasaidia kwa namna fulani ili mwaka mpya wa masomo unapoanza waweze kupata nafasi ya kwenda shule.
- Nataka nifanye kitu cha kusaidia wakati huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka; kama zawadi ya Krismasi na Mwaka mpya.
- Kama kuna watu wanataka tushirikiane kuwasaidia wao au kusaidia shule ya Viziwi kwa ujumla yake naomba tuwasiliane na mawazo yanakaribishwa.
- Endapo kutakuwa na watu wako tayari ninaweza kushikirikiana na gazeti la Daily News kuhakikisha kuwa watoto hawa wanapata msaada unaohitajika. Ninachotaka kujua tu ni kama naweza kuungwa mkono na watu kadhaa ili nilifuatilie. Vinginevyo, tusubiri wazungu waje kuwasaidia. - Tunaweza kuwapa samaki wakala kwa siku moja au tukatengeneza bwawa wakala na wengine au tukawafundisha kuvua!