Tuwasaidie wenye uhitaji,Tusiwapuuze

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,957
Jamii Forum ni kijiji cha watu wengi sana,chenye vitongoji,kata na wilaya za kutosha ambazo jambo moja linaweza tokea Jukwaa flani,mtu wa jukwaa Lingine akashindwa liona,tupo watu tofauti humu JF wenye uwezo/masikini,nk nk.

Sitaki kuandika thread ndefu maana sina point zaidi ya ombi 1 kwenu wote mtaoweza soma hii thread ambayo nitakua na i update kwa kuitia . (nukta) kila siku iitwayo leo (nitakayoingia JF).

Nimeshuhudia watu wakifariki JF ambao siwezi sema nilikua na uwezo wa kuwasaidia ila naweza kusema nilikua na uwezo wa kufanya chochote juu yao (hata kama kingekua kidogo) siwezi jua kidogo changu kingewasaidiaje au wangekichukuliaje.

kupitia kutochangia chochote kwa hawa watu naombeni msaada kuanzia leo Mtu yeyote atae ona member yeyote (yuko serious) anahitaji msaada/anaonyesha kuchoka/kukata tamaaa naombeni mni TAG hata kama huna uwezo wa kumwambia pole,hata kama thread yake inaonekana ya kitapeli naombeni mni TAG mimi nitajua kama ni tapeli au sio tapeli.

Point yangu ni kwamba sitaki kupitwa tena/kuwa sababu/kutofanya kitu kwa hawa waliokata tamaa,member mpauko kaniuma sana ki ukweli huyu ndugu kajimaliaza kwasababu ya upweke (hakua na mtu hata wa kumpa pole) sipo tyr hili litokee TENA kwa member yeyote alie JamiiForums.

kuna thread nyingi sana sizipati,ila naomba kuanzia leo yeyote ataekutana na thread ya muhitaji kama hawezi msaidia naomba kwenye comment a comment user name Langu CONTROLA nikiingia online nitakuta notification nitajua cha kufanya.

kwa sasa ninaemfahamu ambae sitokubali ajipeleke ni Mayala B huyu ndugu yangu naombeni msimpuuze na hata mkimpuuza mimi nimesema Mayala B siwezi kubali ukaondoka otherwise uwe tu una hamu ya kuondoka ila sio MAISHA yawe sababu.

Tag CONTROLA popote unapoona pana uhitaji,Tag ID yangu bila kukosea

SI(c) O(o) EN(n) TI(t) ARA(r) O(o) EL(l) EI(a) = CONTROLA

Popote utapoona wewe pamekugusa naomba namiimi usiache ni tag nifanye chochote kitu,JF ina thread nyingi sana sana sana na nyingi zinatupita wengine,naomba kuanzia Leo niwe KAKA wa kila mwenye kukata tamaa YES i am Na Mungu atanisaidia.
 
Niseme tu kuwa na moyo wa kusaidia ni zaid ya kutoa kwenye nyumba za ibada

nadhani kuna haja ya upande wa uongozi wa jf ukawa na namna ya kuwasiliana na mhitaji ili kufanya huu mwanya usitumike vibaya kwa wenye nia ovu

Ni mtazamo wangu
 
mkuu CONTROLA upo sahihi sana, inasikitisha unaingia jf unakuta matukio yakugusa kweli kweli yamekupita mpaka unataka kujilaumu..
binafsi kuna matukio mawili wakufa kufa yametoka umu lakin nimesikitika sijapata kusaidi ata kwa comment ya hayo yote
kuna ndugu mmoja id: folk na huyu Mpauko mikasa yao inahuzunisha mnoo, ukiangalia jinsi mtu anavofunguka na mpokeo wa members wengine unavokua, daah kama unamchozi ya karibu unaweza kulia...
jaman wandugu, niwaambie kama umeweza kua member wa jf kwa mwaka nzima, una comment una post, una share mambo tofaut na watu humu basi jua hii ni kama community tofauti na social media nyingne as insta au jf, so kuna u seriousness kidogo ukizungumzia jf,
jingine wadau, akiomba msaada humu, kusaidia ni jambo rahisi, usiweke mawazo yako kusiadia ni pesaa tu.. maneno na mawazo yako yanaweza kuwa na mchango mkubwa sana kwa mtu, kuliko maela na mali.
 
Niseme tu kuwa na moyo wa kusaidia ni zaid ya kutoa kwenye nyumba za ibada

nadhani kuna haja ya upande wa uongozi wa jf ukawa na namna ya kuwasiliana na mhitaji ili kufanya huu mwanya usitumike vibaya kwa wenye nia ovu

Ni mtazamo wangu
Uko sahihi Mndali,ila acha nikwambie kitu kimoja hata akitokea Tapeli ila moyo wako umekusukuma kumsaidia MSAIDIE,nikwambie kitu mndali Hata hawa matapeli wengi wao wanafanya utapeli kwasababu tu ya ugumu wa maisha na vikwazo vyake.

ila tu niseme kitu unapomsaidia msaidie kwa sharti moja (lazima muongee) wakati mnaongea mueleze Ukweli kwann unamsaidia,mueleze si kwamba wewe ni tajiri ila unafanya kwa ajili yake,nakuhakikishia kupitia maneno utakayompa yawezekana "wewe" ukawa wa mwisho kutapeliwa nae.

kupitia yale maneno yakamfanya kuacha utapeli,don't just help and stay quite,these huys needs WORDS very special words usiache ongea nao,naamini hata hawa matapeli tutawaokoa na wengine wanaweza kuacha.

sitoumia nikimsaidia mtu kisha nikaja kugundua ni tapeli ila Nitaumia sana kama nisipomsaidia mtu halafu kumbe hakua ni Tapeli (itaniumiza mno).
 
kuna ndugu mmoja id: folk na huyu Mpauko mikasa yao inahuzunisha mnoo, ukiangalia jinsi mtu anavofunguka na mpokeo wa members wengine unavokua, daah kama unamchozi ya karibu unaweza kulia...
Nimeshindwa vumilia mwenzako,imenibidi niruke baadhi ya comment

kwenye nyuzi za Mpauko mpk thread zake zenyewe ndio kabisa mwisho

nikajisemea (hebu nitoke huku) kama kutokea imeshatokea ila sasa lazima

nihakikishe siumii hivi tena,maana maumivu mengine kama usipochukua hatua

inakua kama ulijitakia na siwezi ruhusu hilo litokee.Mungu anisaidie.
 
Uko sahihi Mndali,ila acha nikwambie kitu kimoja hata akitokea Tapeli ila moyo wako umekusukuma kumsaidia MSAIDIE,nikwambie kitu mndali Hata hawa matapeli wengi wao wanafanya utapeli kwasababu tu ya ugumu wa maisha na vikwazo vyake.

ila tu niseme kitu unapomsaidia msaidie kwa sharti moja (lazima muongee) wakati mnaongea mueleze Ukweli kwann unamsaidia,mueleze si kwamba wewe ni tajiri ila unafanya kwa ajili yake,nakuhakikishia kupitia maneno utakayompa yawezekana "wewe" ukawa wa mwisho kutapeliwa nae.

kupitia yale maneno yakamfanya kuacha utapeli,don't just help and stay quite,these huys needs WORDS very special words usiache ongea nao,naamini hata hawa matapeli tutawaokoa na wengine wanaweza kuacha.

sitoumia nikimsaidia mtu kisha nikaja kugundua ni tapeli ila Nitaumia sana kama nisipomsaidia mtu halafu kumbe hakua ni Tapeli (itaniumiza mno).
Mkuu mimi kuongea na mtu siwezi nikitumwa na na nafsi yangu

ila ngoja leo niseme tu kuwa kila mwenye uhitaji nitamsaidia kulingana na nilicho nacho
 
Kuna wakati ni vigumu sana kumjua yupi anahitaji msaada na yupi ni tapeli.

Mfano mimi mwezi huu february 2020 na february 2019, nimeishia kutapeliwa tu kwa huruma.

Unapomsaidia mtu halafu kumbe lengo lake ni kukudhulumu/ kukudanganya au kukutapeli inauma sana, kwa sababu amechukua advantage ya moyo wako wa huruma na kusaidia.

Hii inasababisha kumpa msaada mtu ambae hakufaa kusaidiwa na kusababisha aliyehitaji msaada sahihi kuukosa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
January and February Ni miezi migumu sana, usichoke kusaidia, ukitapeliwa na kuumia Mungu anakubariki zaidi na kukunyooshea njia zako bila wewe kujua, Mungu ni mwema kwetu na mwenye Haki ataishi kwa Imani

Back
Top Bottom