Tuwasaidie wana-igunga kama kweli ni wapenda maendeleo na siyo Madaraka?

Topical

JF-Expert Member
Dec 3, 2010
5,173
935
CCM wangetumia 30% ya hela walizotumia ili kupata mbunge moja wangeweza kujenga zahanati katika kila kata Igunga

CDM wangetumia 30% ya hela walizotumia ili kupata mbunge (japo wamemkosa) wangeweza kukarabati shule zote za msingi Igunga

CUF wangetumia 30% ya hela walizotumia ili kupata kura 2000 wangeweza kujenga barabara za kata zote za igunga...

Tunatumia pesa nyingi kutafuta madaraka kuliko pesa tunazotumia kuleta maendeleo????...

Je CDM, CCM na CUF wako tayari kufanya harakati kama hizo katika jimbo lolote (hata la mfano tu) ili kuleta maendeleo kwa wananchi?

Regia anaandika aliyoyakuta igunga..je yuko tayari kuwashawishi viongozi wa chama chake watumie 30% ya hela walizotumia kusaidia wana igunga au ni kugombea madaraka tu..
 
heshima yako mkuu leu umetumia kichwa kufikir asante sana naunga mkono hoja but with an exption aanze kafumu kuonyesha njia acje akawa kama YA RA
 
Kwanini aanze kafumu? njia inaweza kuonyeshwa na mtu yeyote yule?

Hivi vyama si vinasema vinataka kuleta maendeleo? kwanini wasianze hata na jimbo moja hivi (la mfano)

Wa mobilize fund kwa ajili tu ya maendeleo ya jimbo fulani...

Naona vyama vyote wana strategies kali sana ili kupata madaraka lakini ikija kuhamasisha maendeleo lazima aenze kafumu why?
 
Ikiwa Ndesamburo alishanyimwa kujenga soko jimboni kwake kwa kile kilichohofiwa na ccm kuwa ni kujiongezea umaarufu;itakuwaje siku wapinzani wakiamua kujenga jimbo moja la mfano?
Na wakianza harakati za kujenga jimbo moja ni nini itakuwa mikakati ya wabunge wao kuhakikisha majimbo yao hayabaki nyuma?
Ni jukumu la kikatiba la serikali iliyopo madarakani kuwaletea watu wake maendeleo.
Chama kinachojenga jimbo moja(hata kama si lake) bila kuwa na mikakati ya kuking'oa chama kilichopo madarakani kinaweza kutafutiwa jina lingine KATU SI CHAMA CHA SIASA.
 
Kwa hiyo vyama vinaogopa propaganda za kupewa majina wakiamua kupanga strategies za kuwasaidia watu kimaendeleo...

Lakini wako tayari kupinga kwa gharama kubwa propaganda ili wapewe madaraka?
 
Back
Top Bottom