Tuwasaidie Vipi 60% ya Wazanzibari kutoka kwenye Muungano?

Mzee Mwanakijiji umenena vyema! Tatizo kubwa na viongozi wa Zanzibar ni unafiki maana wana taka sitaki! Kama hawaupendi Muungano kwa nini wanataka muungano wa mkataba? Yaani ili sisi tutumie resources zetu kuwalinda? Hilo hatulitaki! Kama hawataki kubaki kwenye muungano wajiondoe na wawe na mamlaka yao kamili badala ya kuwa nusu ndani nusu nje!
BYE BYE ZANZIBAR

970028_651978404817198_1811388342_n.jpg

Inaonekana kina Seif Sharrif na kina Karume hawataki hasa Zanzibar iwe dola huru ikiwa na "mamlaka yake". Kwa karibu miaka miwili sasa wameendelea "kudai" Zanzibar "huru" huku wakipuuzia njia zote rahisi za kuweza kufanya hivyo. Nimejaribu kwa kila namna kuwapa ushauri rahisi wa kuiondoa Zanzibar kwenye Muungano na ikawa nchi huru na tukakutana UN, SADC, na EA kama nchi huru majirani lakini ndugu zetu inaonekana hawataki kuchagua njia hata moja. Badala yake wameendelea na nina uhakika wataendelea kufanya mikutano mingine ya "kudai" Zanzibar huru.

Sasa najiuliza wanataka tuwasaidieje? Wanataka sisi tuwafukuze watoke ili waseme tumewafukuza? Suala la Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili liko mikononi mwa Wazanzibari peke yao.

1. Walipodai Bendera ya Zanzibar Tanzania bara hatukuulizwa; waliamua wakawa nayo
2. Walipotaka wimbo wa Taifa - Tanzania Bara hatukuulizwa; wakawa nao
3. Walipoamua kutangaza Zanzibar ni huru na kuainisha mipaka yake kupitia katiba yao walifanya hivyo bila Watu wa Bara kuulizwa.

Kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa linapokuja suala la Zanzibar kudai "uhuru" na alama za kuwa bado wao ni dola Zanzibar wana rekodi ya kufanya hivyo bila kuomba kibali kutoka Dodoma au kwa watu wa bara. Sasa kwanini kwenye "mamlaka kamili" ni kama vile "wanataka hawataki"? Kabla sijaamua kuwapa pendekezo jingine naomba Wazanzibar wale asilimia 60 ambao wanaamini kutokana na wingi wao wanawakilisha msimamo wa Wazanzibari wote wafanya mambo yafuatayo ili waharakishe kuitoa Zanzibar kwenye "ukoloni" wa watu wa bara na kuirejesha kuwa ile nchi nzuri, ya heri, ambapo watu wake wote walikuwa wanaishi kwa furaha na maridhiano tangu enzi na enzi.

1. Chama cha CUF na wale wa CCM upande wa Zanzibar ambao wanaamini Zanzibar inakaliwa na Bara kama koloni watangaze kutoutambua Muungano huu kwa vile siyo halali.

2. Wakishafanya hilo la kwanza CUF na CCM Zanzibar wawaambie wabunge wao walioko kwenye Bunge la Muungangano kujiuzulu mara moja ili warudi Zanzibar

3. Wazanzibar wamuambie Makamu wa Rais wa Muungano Dr. Ghaib Bilali pamoja na watumisho wengine wote walioko kwenye Utumishi wa Jamhuri ya Muungano ambao ni Wazanzibari waachie nafasi zao zote ili kutekeleza hilo la 1. Hii itauthibitishia ulimwengu na marafiki zao kuwa kweli wako serious katika kutaka uhuru - huwezi kudai uhuru wakati huo huo unatumikia serikali ile ile!

4. Ili kufanikisha hayo mambo matatu ya kwanza hapo juu na kuwa yasionekane yamefanywa kiholela basi Baraza la Wawakilishi ambao lina wasomi lifanye mambo mawili. Kwanza lilete hoja rasmi ya kuitaka serikali kuandaa mswada wa Sheria ya kusimamia kura ya maoni (referendum) ya jinsi Zanzibar itajitoa, ijitoe lini na vipi na kwa mfumo gani. Na pili ni kuileta sheria hiyo ili ipitishwe na Wawakilishi.

5. Kwa vile inawezekana basi katika sheria hiyo ya No 4 hapo itahitaji Bunge la Muungano liliridhie basi Baraza la Wawakilishi lipitishe sheria hiyo na iridhiwe na Rais wa Zanzibar na hoja ya sheria hiyo iletetwe na hao wabunge wa Zanzibar kwenye Bunge la Muungano (kabla hawajatoka) ili Bunge la Muungano liipitishe na kuruhusu Zanzibar kuanza mchakato wa kutoka kwenye Muungano na ili kwamba Bunge la Muungano nalo liweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa mali na haki za Watanganyika Zanzibar haziangukii mikononi mwa Nchi ya Zanzibar!

6. Wazanzibari waharakishe kuweka tarehe ya kutaka kutoka kwenye Muungano ili na sisi watu wa bara tuzidi kuwaombea ili matamanio yao na njozi zao za kuirudisha Zanzibar ambayo inatawaliwa na Tanganyika zitimie.

NB: Ikumbukwe kuwa watu wa bara hatutaki Muungano wa Mkataba. Tunataka Zanzibar watoke bila ya kufuatiwa na kitu kingine chochote zaidi ya mahusiano ya ujirani mwema wa nchi mbiili. Bila ya shaka kutokana na historia inawezekana katika mfumo ujao kutakuwa na makubalianao ya nchi mbili (bilateral agreements) ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa huru n.k nk

Sasa kama njia hizi zote hazichukuliwi; tuwasaidie vipi Wazanzibar hawa wanaotaka kutoka kufunga virago?

LET ZANZIBAR GO!!!

Maamuzi ya waz'br ni ya waz'br wenyewe,hakuna nyerere wala mwanakijiji mwenye uwezo wa kuwaamulia,mnaogopa nini kuileta tanganyika kwenye meza tukaujadili muungano huu?hii ndio njia rahisi kuliko zote.
Sasa waz'br mbona mnajikanyaga! Sisi tunasubiri ridhaa yenu kama hamtaki muungano tuko tayari! Sisi tukiamua kuuvunja muungano tutaonekana tunawanyanyasa kutokana na udogo wa nchi yenu.
 
Hivi Bara inaicolonize Zanzibar Kivipi?
​Hawa akina Seif na Moyo watu wa ajabu sana! Wamekuwa viongozi katika serikali hizi kwa muda mrefu lakini inaelekea hawajui namna serikali hizi zinavyoendeshwa!
 
Wazee wa fitina hawawezi kuuchukua ushauri wako hata robo.Zanzibar tutaitawala milele hata kwa bakora na mtutu wa bunduki wataka wasitake.Tukiwaacha hawa jamaa ni majanga na historia itakuja kutuhukumu.Na hizo pye pye zao hazina madhara yoyote wakivuka mipaka watakiona cha moto.Pambav kabisa.Tanzania haifi ng'o.
 
sioni faida ya muungano .. KURA YA HAPANA KWA MUUNGANO KWANGU IKO WAZI .. MAANA MIMI BINAFSI NIMECHOKA NA KELELE ZA UPANDE WA PILI... TUNABEMBELEZANA NINI JAMANI..? NDOA TAKATIFU ZINAVUNJWA SEMBUSE MUUNGANO WA KISIASA .. LINAPOKUJA SUALA MUUNGANO UKWELI NA KWAZIKA NAFSI YANGU SANA TENA SANA .. NI MOJA YA MAOMBI YANGU KUVUNJIKA MUUNGANO NAAMINI MUNGU WANGU ATANISIKILIZA... MAANA KWA SASA SIONI SABABU YA UWEPO HUU MUUNGANO..
LET ZANZIBAR GO!!!
L
 
​Hawa akina Seif na Moyo watu wa ajabu sana! Wamekuwa viongozi katika serikali hizi kwa muda mrefu lakini inaelekea hawajui namna serikali hizi zinavyoendeshwa!

Ni hofu ya Kifo inawasumbua, haya mawazo walikuwa nayo toka wakiwa vijana wadogo lakini hawakuwa tayari kuyapigania kwa sababu walikuwa ni wafaidika wa mfumo uliopo sasa, now that umri unawalazimisha kuachia mirija, kwa namna ya kutokutaka wengine wafaidi kama wao wanataka kuwaaribia.
 
Looh haw watu wa Zenji wanatutegemea sana watu wa Bara.hata vitu vyao vyotee wananunua huku kuanzia kitunguu nyanya karot kila kitu ni bara wakijitoa tu watakufa na shida zao.kweli maisha ya ZNZ yapo juu sana kwa mahitaji ya nyumbani.Waacheni wanebde zao jamani.
 
Mwana kijiji una dhani baba yenu wa taifa alipo viunga nisha vyama vya ukombozi alifanya kwa kubahatisha faida yake ni hiyo ya viongozi wa Z'bar kukosa mamlaka na nguvu za kisiasa dhiti ya nch yao , rais jumbe kaishia wapi baada ya kuhoji muungano wanachofanya Wazanzibar kutaka hayo mamlaka wakiyapa watakuwa hawana haja ya muungano kandamizi na watauvunjia mbali
 
This NOISY is a well calculated move to influence RASMU YA KATIBA MPYA. Hao Wazanzibari wanafahamu karibu Warioba atatoa rasmu ya Katiba mpya. Hivyo wanajua kupiga kelele kama kawaida kutamuogopesha Warioba. Make no MISTAKE utaona Rasmu ya Katiba mpya atakayoitoa itakuwa na vipengele vingi vya kuipendelea Zanzibar. Hivyo Lengo lao litakuwa limetimia.

BTW, Kama wana UHAKIKA kwamba 60% ya Wazanzibari hawautaki MUUNGANO it is so SIMPLE. Solution iko kwenye ballot box. 2015 waipigie kura CUF, then CUF inaweza kuwaaondoa kwenye muungano. Hayo yote uliyopendekeza hayawezi kufanyika chini ya CCM. Huyo Karume Jnr Mwenyewe alikuwa na kila UWEZO wa kuitoa ZNZ kwenye Muungano wakati huo akiwa RAIS wa SMZ. Lakini hakufanya hivyo, hadi hii leo he is almost powerless ndiyo anapayuka kama debe tupu.

ZNZ huru haiwezi kupatikana under CCM because viongozi wa CCM Zanzibar they are HYPOCRISY.

Ballot box? My foot what Ballot box? Its an open secret CUF imeshinda chaguzi zote tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi.
 
Mzee Mwanakijij,

Tarehe 30/5/2013 Wazanzibar kadhaa wamefungua kesi (Petition) Mahakama Kuu ya Zanzibar wakiomba Mahakama hiyo itangaze kuwa Muungano ni batili. Kesi hii imeshafikishwa mahakamani ingawa bado haijapangiwa kusikilizwa. Huenda na hizi ndiyo muendelezo wa siasa za Zanzibar na hatua mahususi ya ama kuvuruga mchakato wa Katiba au kuvuruga Muungano huu ambao ni dhahiri wenzetu wameuchoka kabisa. Ngoja tuendelee kufuatilia kesi hiyo.
 
2. Wakishafanya hilo la kwanza CUF na CCM Zanzibar wawaambie wabunge wao walioko kwenye Bunge la Muungangano kujiuzulu mara moja ili warudi Zanzibar

3. Wazanzibar wamuambie Makamu wa Rais wa Muungano Dr. Ghaib Bilali pamoja na watumisho wengine wote walioko kwenye Utumishi wa Jamhuri ya Muungano ambao ni Wazanzibari waachie nafasi zao zote ili kutekeleza hilo la 1. Hii itauthibitishia ulimwengu na marafiki zao kuwa kweli wako serious katika kutaka uhuru - huwezi kudai uhuru wakati huo huo unatumikia serikali ile ile!

LET ZANZIBAR GO!!!

Kiongozi mmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, "Mwalimu mwema, nifanye nini ili niweze kuupata uzima wa milele?" Yesu akamwambia, "Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. Unazijua amri: Usizini; usiue; usiibe; usitoe ushahidi wa uongo; waheshimu baba yako na mama yako." Yeye akasema, "Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu." Yesu aliposikia hayo akamwambia, "Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: uza kila ulicho nacho, wagawie maskini, na hivyo utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate." http://biblehub.com/luke/18-23.htm Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana
 
Wazee wa fitina hawawezi kuuchukua ushauri wako hata robo.Zanzibar tutaitawala milele hata kwa bakora na mtutu wa bunduki wataka wasitake.Tukiwaacha hawa jamaa ni majanga na historia itakuja kutuhukumu.Na hizo pye pye zao hazina madhara yoyote wakivuka mipaka watakiona cha moto.Pambav kabisa.Tanzania haifi ng'o.

Unaonaje nguvu hizo ukazielekeza kuwazuia wale wachina wanaochimba dhahabu?
 
Ballot box? My foot what Ballot box? Its an open secret CUF imeshinda chaguzi zote tangu kuanzishwa siasa za vyama vingi.

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa mara zote CUF inashinda, lakini mbona wamekuwa wanachezewa akili na wanasiasa wao huku wakiwa wanajua kabisa na hawawachukulii hatua zozote? Kama wanauwezo wakuwamwagia Tindikali viongozi wa serikali, kuua viongozi wa dini na kuchoma nyumba za ibada kwanini wasianze kuwawajibisha wanasiasa wao wanafiki kwa kuwafanyia hayo wanayowafanyia wengine?

Wachome nyumba ya seif,Karume etc kuonyesha kukerwa kwao na viongozi wao kuwa vigeugeu tuone kuwa ni kweli wapo serious. Kwanini wamekuwa na mipasho tu kama taarabu halafu hakuna hatua thabiti inayochukuliwa na wananchi? Mimi kwakweli wamenichosha sana hawa watu, japokuwa kuna babu zangu huko (Nilisikia babu zangu wakinyamwezi walikuwa wakipelekwa huko kipindi cha utumwa na vizazi vyao vimejaa unguja mpaka leo) lakini kiukweli nimeshachoshwa na kelele zao.
 
Kwa namna hali ya kisiasa ilivyo nchini kwa sasa, ni ngumu kwa Zanzibar kujitenga na Muungano..
 
BYE BYE ZANZIBAR

970028_651978404817198_1811388342_n.jpg

Inaonekana kina Seif Sharrif na kina Karume hawataki hasa Zanzibar iwe dola huru ikiwa na "mamlaka yake". Kwa karibu miaka miwili sasa wameendelea "kudai" Zanzibar "huru" huku wakipuuzia njia zote rahisi za kuweza kufanya hivyo. Nimejaribu kwa kila namna kuwapa ushauri rahisi wa kuiondoa Zanzibar kwenye Muungano na ikawa nchi huru na tukakutana UN, SADC, na EA kama nchi huru majirani lakini ndugu zetu inaonekana hawataki kuchagua njia hata moja. Badala yake wameendelea na nina uhakika wataendelea kufanya mikutano mingine ya "kudai" Zanzibar huru.

Sasa najiuliza wanataka tuwasaidieje? Wanataka sisi tuwafukuze watoke ili waseme tumewafukuza? Suala la Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili liko mikononi mwa Wazanzibari peke yao.

1. Walipodai Bendera ya Zanzibar Tanzania bara hatukuulizwa; waliamua wakawa nayo
2. Walipotaka wimbo wa Taifa - Tanzania Bara hatukuulizwa; wakawa nao
3. Walipoamua kutangaza Zanzibar ni huru na kuainisha mipaka yake kupitia katiba yao walifanya hivyo bila Watu wa Bara kuulizwa.

Kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa linapokuja suala la Zanzibar kudai "uhuru" na alama za kuwa bado wao ni dola Zanzibar wana rekodi ya kufanya hivyo bila kuomba kibali kutoka Dodoma au kwa watu wa bara. Sasa kwanini kwenye "mamlaka kamili" ni kama vile "wanataka hawataki"? Kabla sijaamua kuwapa pendekezo jingine naomba Wazanzibar wale asilimia 60 ambao wanaamini kutokana na wingi wao wanawakilisha msimamo wa Wazanzibari wote wafanya mambo yafuatayo ili waharakishe kuitoa Zanzibar kwenye "ukoloni" wa watu wa bara na kuirejesha kuwa ile nchi nzuri, ya heri, ambapo watu wake wote walikuwa wanaishi kwa furaha na maridhiano tangu enzi na enzi.

1. Chama cha CUF na wale wa CCM upande wa Zanzibar ambao wanaamini Zanzibar inakaliwa na Bara kama koloni watangaze kutoutambua Muungano huu kwa vile siyo halali.

2. Wakishafanya hilo la kwanza CUF na CCM Zanzibar wawaambie wabunge wao walioko kwenye Bunge la Muungangano kujiuzulu mara moja ili warudi Zanzibar

3. Wazanzibar wamuambie Makamu wa Rais wa Muungano Dr. Ghaib Bilali pamoja na watumisho wengine wote walioko kwenye Utumishi wa Jamhuri ya Muungano ambao ni Wazanzibari waachie nafasi zao zote ili kutekeleza hilo la 1. Hii itauthibitishia ulimwengu na marafiki zao kuwa kweli wako serious katika kutaka uhuru - huwezi kudai uhuru wakati huo huo unatumikia serikali ile ile!

4. Ili kufanikisha hayo mambo matatu ya kwanza hapo juu na kuwa yasionekane yamefanywa kiholela basi Baraza la Wawakilishi ambao lina wasomi lifanye mambo mawili. Kwanza lilete hoja rasmi ya kuitaka serikali kuandaa mswada wa Sheria ya kusimamia kura ya maoni (referendum) ya jinsi Zanzibar itajitoa, ijitoe lini na vipi na kwa mfumo gani. Na pili ni kuileta sheria hiyo ili ipitishwe na Wawakilishi.

5. Kwa vile inawezekana basi katika sheria hiyo ya No 4 hapo itahitaji Bunge la Muungano liliridhie basi Baraza la Wawakilishi lipitishe sheria hiyo na iridhiwe na Rais wa Zanzibar na hoja ya sheria hiyo iletetwe na hao wabunge wa Zanzibar kwenye Bunge la Muungano (kabla hawajatoka) ili Bunge la Muungano liipitishe na kuruhusu Zanzibar kuanza mchakato wa kutoka kwenye Muungano na ili kwamba Bunge la Muungano nalo liweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa mali na haki za Watanganyika Zanzibar haziangukii mikononi mwa Nchi ya Zanzibar!

6. Wazanzibari waharakishe kuweka tarehe ya kutaka kutoka kwenye Muungano ili na sisi watu wa bara tuzidi kuwaombea ili matamanio yao na njozi zao za kuirudisha Zanzibar ambayo inatawaliwa na Tanganyika zitimie.

NB: Ikumbukwe kuwa watu wa bara hatutaki Muungano wa Mkataba. Tunataka Zanzibar watoke bila ya kufuatiwa na kitu kingine chochote zaidi ya mahusiano ya ujirani mwema wa nchi mbiili. Bila ya shaka kutokana na historia inawezekana katika mfumo ujao kutakuwa na makubalianao ya nchi mbili (bilateral agreements) ili kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa huru n.k nk

Sasa kama njia hizi zote hazichukuliwi; tuwasaidie vipi Wazanzibar hawa wanaotaka kutoka kufunga virago?

LET ZANZIBAR GO!!!

Mkuu MKJJ mbona rahisi sana!
Kwanza ni wakubaliane kususia muungano kwa kujiuzuru nafasi zote kuanzia Umakamu wa rais na wabunge wote toka Znz kujitoa Bungeni, hasa wakati huu.
Pili Zanzibar ni nchi , na wazanzibari wote walioko Tanganyika kurudi nchinini kwao.
Kutnganisha chama cha mapinduzi ndiyo rahisi kabisa, si kila mtu ana kwao?!!
 
Tanganyika Tanganyika nakupenda kwa moyo wote.

Last edited by a moderator:
Mie nafikiri watanganyika km kawaida yetu ni wakarimu na upendo tele,hawa wazanzibar ni ndugu zetu,ukiangalia vizuri historia yetu karibia nusu ya wakazi wa zanzibar asili yao ni bara,sasa awo wanaoleta chokochoko ya kutaka kuvunja muungano,ni wakuja tu hawo km wakina uhamsho.
 
Back
Top Bottom