Tuwasaidie viongozi wetu kutuongoza

Status
Not open for further replies.

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,819
35,809
Mabibi na mabwana kutofautiana kimawazo hakujawahi kuwa dhambi. Kutofautiana kwa mawazo ndiyo uthibitisho rasmi wa kuwa tu binadamu hai na timamu.

Kutofautiana kimawazo ni muhimu mno kwa mustakabala wa ustawi wa jamii na hata taifa lolote.

Siyo siri tena kuwa tuna gonjwa baya katikati yetu. Amekiri mh. Rais Magufuli kuwa kuna Corona mbaya zaidi imeingia nchini. Imeingia vipi, ni ngeni ni ile ile nk, hakuna ajuaye kwani hatukuwa na mkakati thabiti wa ufutiliaji.

Pamoja na yote mengine sasa yanabakia kuwa historia. Kama wenye busara suala lilopo kinakufa ni kuganga yaliyopo na yajayo. Vinginevyo tumeshatumbukia shimoni na tunaendelea kulichimba zaidi.

JJ Rawlings Rais kipenzi wa Ghana kazikwa jana akiwa mhanga wa Corona.

Haitusaidii kuuficha ukweli. Kwa mwendo huu wa Tanzia baada ya tanzia tufike mahali tushike brake sasa na kwa kudhamiria haswa. Hatuko salama.

Tanzia huku, tanzia kule. Kwa kigogo huyu kwa kigogo yule. Achilia mbali kwetu sisi kina yakhe.

Tuna haki ya kuishi kama hawa wanao na walio tangulia ghafla ghafla hivi. Leo wao kesho itakuwa sisi na wapendwa wetu.

Tunao uwezo wa kuyasimamisha madhila haya kama binadamu. Ya Mungu tumwachie yeye nasi tuna sehemu yetu. Maisha hayawezi kuendelea kama kawaida.

Ni heri kuishi tukiwa maskini kuliko kufa matajiri. Ni heri tukifa tukipambana ili kuishi kuliko kusubiria lolote kuwa liwe.

Maisha ya watu wetu kwanza bandugu.

Ninawasilisha.
 
Hapa palikuwa na moja ya wito kwa mh. Rais wakati mashule yakiwa yamefungwa mwaka jana.

Wito huo ungali unaishi leo:

 
JJ Rawlings rais kipenzi wa Ghana kazikwa jana akiwa mhanga wa corona.
Huyu ni nani?
Bahati mbaya Magufuli hataki kusaidiwa, hamsikilizi mtu. Afadhal Idd Amin alikuwa anamsikiliza Isaac Maliyamungu ( msaidizi na kipenzi cha Idd Amin aliyekuwa katili kuliko Idd Amin mwenyewe)
 
Huyu ni nani?
Bahati mbaya Magufuli hataki kusaidiwa, hamsikilizi mtu. Afadhal Idd Amin alikuwa anamsikiliza Isaac Maliyamungu ( msaidizi na kipenzi cha Idd Amin aliyekuwa katili kuliko Idd Amin mwenyewe)

"Uongozi wa nchi si sawa na uongozi wa shamba la mtu binafsi," alisema hayati Baba wa taifa (rip).

Uongozi wa nchi si suala la kutaka au kukataa kushauriwa kama nafsi ya mtu anavyoweza kujisikia kwenye mambo binfsi. Uongozi wa nchi hauwezi kuwa suala binafsi.

Uongozi wa nchi ni pamoja na kupewa options zote mezani. Si tu zile azitakazo mtu. Bali hata zile asiyetaka kujisikia.

Hata kuwa impeached ikibidi nayo ni option.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom