#COVID19 Tuwaruhusu na kuwahamasisha waumini wetu kupokea chanjo ya COVID-19

mjarrab

Senior Member
Nov 13, 2015
108
55
ZINDUKA CHANJO YA COVID 19
-------------------------------------------
Kumekuwepo na wasiwasi juu ya Matumizi ya chanjo ya covid 19.
Wengine Wana wasiwasi juu wa kupata Madhara ya baadae kutokana na chanjo hizo.

Wengine wanaona ni Kama mtego wa kuwaangamiza baadhi ya watu fulani.
Wale wenye imani za dini(siyo wote) Wanaamini Kukubali kuchanjwa ni sawa na kudharau nguvu za Maombi!

Wakati dunia ilipo kumbwa na janga hili kulikuwa hakuna namna ya kufanya zaidi ya kila mtu kutafuta namna ya kujikinga au kujitibu kwa wale walio patwa na ugonjwa huo.

Serekali Yetu ya awamu iliyopita ilihamasisha Matumizi ya dawa za asili ikiwemo kujifukiza katika juhudi za kupambana na janga hilo!
Pia maombi kupitia imani za dini mbalimbali yalifanyika katika kumuomba Mungu aiepushe na janga hili!.

Ukweli ni kwamba Mambo hayo yalisaidia Sana! kuondosha wingu la hofu lililo kuwa limetanda!,Ijapo kuwa Kuna watu wengi walipoteza Maisha katika kipindi hicho,.

Kwa bahati Dunia imeweza kugundua baadhi ya chanjo za kupambana na ugonjwa huo, Lakini imekuwa ni kazi ngumu kuwashawishi watu kuitumia chanjo hiyo!

VIKWAZO KWA IMANI ZA KIDINI.
Zipo baadhi ya dini ambazo zinapinga matumizi ya chanjo hiyo kwa msingi wa kiimani! wao waliamini wimbi la kwanza na la pili liliondoshwa kwa Maombi!,hivyo hata wimbi hili la tatu Wanaamini litaondoshwa kwa njia ya Maombi vile vile!.
Sasa Naomba kuongea na watu hawa kwa sababu ni kundi kubwa katika jamii.

Mwenyezi Mungu kwa Mujibu wa imani kuu mbili hapa Tanzania alimuumba Mwanaadamu na kumpa Mamlaka ya kuviendesha(kuvisimamia) vitu vyote duniani!.

Lakini hakumpa mamlaka bila kumpa nyezo na uwezo wakuweza kuvisimamia!
Hivyo alimuumba kwa sifa zote zinazo hitajika kuwa msimamizi!, kupitia neema ya akili alimuongoza kujua kanuni za vitu,ufumbuzi na utatuzi wa Mambo!

Kupitia neema hiyo ya Uumbaji, binaadamu ameweza kumudu kuvumbua vitu vingi, Binaadamu kupitia neema hiyo ya akili amejifunza madhara na faida ya kila kitu!
amajua nini kitatokea kwa kuharibu Mazingira,amegundua nini kinacho sababisha kuleta magonjwa, anaegundua kwa neema hiyo ya akili namna ya kujikinga na Madhara! amegundua dawa za kujitibu kwa neema ya akili aliyo pewa na Mungu.

Binaadamu bado ana safari ndefu! bado Kuna Mambo mengi ambayo hajayapatia ufumbuzi,!

kwa Yale alio fanikiwa kuyagundua na kuyatumia hana budi kurejesha Shukrani kwa Muumba kwa sababu ya neema ya akili aliyo pewa ambayo imemsaidia kutatua moja ya changamoto!.

kwa hivyo kutumia akili kwa Jambo ambalo linaleta ustawi katika jamii ni kuitumia neema hiyo kwa kazi ambayo ndiyo Lengo la kuumbwa kwake!.
Kwa hivyo dawa zote unazo ziona ambazo zinatibu zimetokana na akili iliyo undwa na Mungu kufanya kazi hiyo.

Kwa hivyo dawa yenye kutibu ni kazi ya Mungu! hivyo mtu anatakiwa atumie dawa huku akimshukuru Mungu kwa neema ya ugunduzi wa dawa iliyofanywa na akili iliyo undwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kazi hiyo!

Ikiwa Chanjo au dawa haipo kwa wakati huo ina maana kwamba Bado binaadamu hajafikia uwezo wa kugundua kwa wakati huo! Na kwa kuwa tiba ni hitajio kwa wakati huo! Basi binaadamu hana budi kurejea kwa Muumba wake kwa Maombi,Sala,na Dua! kwa sababu hana namna yoyote kwa wakati huo.!

Na Mwenyezi Mungu atatoa msaada kwa sababu aliyepewa mamlaka ya usimamizi Kuna kitu cha dharura anahitajia kwa wakati huo. Ama Kama chanjo au Dawa imepatikana basi Binaadamu hana budi isipokuwa kumshukuru Mungu kwa neema ya akili iliyo gundua chanjo au tiba!.

Mwenyezi Mungu anaombwa kwa Yale yasiyowezekana kwa Mwanaadamu, Na anashukuriwa kwa Yale ambayo binaadamu ameweza kuyamudu!
Kumshukuru Mungu kwa kile ulicho weza kukimudu kunaongeza baraka za Mungu kwa sababu umetambua nguvu inayo endesha Mambo yote.

Sasa Kumuomba Mungu kinga au tiba,wakati chanjo au Dawa zipo ni sawa na kumuomba Mungu chakula wakati mkate upo mbele yako!.
DHANA YA CHANJO KUWA SUMU KWA WATU WA IMANI.

Kama kweli muumini anaimani thabit hawezi kuogopa chanjo au Dawa eti kwa kisingizio zimewekewa madhara!
Mwenyezi Mungu huyo huyo ambae mnamuomba awalinde na kuwatibu na ugonjwa wa Corona anaweza pia kuwakinga na Madhara yanayoweza kuwemo kwenye dawa!

Hivyo basi tuwaruhusu na kuwahamasisha waumini wetu kupokea chanjo ya ugonjwa huu,huku maombi ya kiwa ni kumuomba Mungu kukinga Madhara yanayo weza kuletwa na Dawa hizo.
 
Asee...

Huyu covid naona anawapa watu shida sana.

Ngoja niwe mtazamaji na msikilizaji kwanza, maana tulipofika siku 100 tulikuwa na mbwembwe za kufa mtu za ANAUPIGA MWINGI.

So hata kwa huyu ndg covid pia nampa muda twende taratibu kwanza, kabla ya kuchukua uamuzi usio umiza.
 
Tunachanja kwa hiari, Wengi hatutaki kuchanja, nyie wachache mnaotaka kuchanja kazi kwenu, mbona mnatia nguvu sana kutuhimiza, kama mnaona tuna enjoy basi msichanje 😃😃

Chanjeni nyie kwanza muwe viumbe vya majaribio kama wale panya wa kwenye maabara, tukiona bado mko fresh baada ya miaka 30 hivi ndo tutashawishika kuchanja.

Ila kwa sasa bado tunawashukuru kwa ujasiri wenu, maana msipochanja sijui tutapata viumbe vya majaribio wapi
 
Aliyeamini maombi na ambaye anaamini kwamba corona ilipungua kwa kuwa tulichukua tahadhari, hao wote kwangu hawana tofauti.
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Kiongozi wa dini:🗣waumini eeee
Waumini:🗣eeeh babaa!!
Kiongozi wa dini:🗣tuchanje mbuga!!
Waumini:🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
Takwimu za vifo kwa watu wenye magonjwa kama hayo ikoje?
 
Kwanini msijibu hoja za Gwajima kwanza?

1.) Hiyo chanjo si ya majaribio kwani? Anasema uongo?
2.) Kwanini mnaiita chanjo wakati haizuii maambuki, haikingi usiambukize wengine na haizuii kuumwa na kufariki kwa Corona? Why?

3.) Kama Mungu ametupa akili kama usemavyo, ni kwanini unataka tusizitumie wakati tunaona kabisa hatari iliyopo mbele yetu kwenye hizo chanjo za majaribio? Huoni kuzikataa ndio kutumia hizo akili?
 
Tunachanja kwa hiari, Wengi hatutaki kuchanja, nyie wachache mnaotaka kuchanja kazi kwenu, mbona mnatia nguvu sana kutuhimiza, kama mnaona tuna enjoy basi msichanje 😃😃

Chanjeni nyie kwanza muwe viumbe vya majaribio kama wale panya wa kwenye maabara, tukiona bado mko fresh baada ya miaka 30 hivi ndo tutashawishika kuchanja.

Ila kwa sasa bado tunawashukuru kwa ujasiri wenu, maana msipochanja sijui tutapata viumbe vya majaribio wapi
Wewe wale wamechanja vitamin tu zile, hivi Rais wa nchi ni mtu wa kumfanyia majaribio ya Johnson and Johnson yenye uwezekano wa kugandisha damu? We inakuingia akilini hiyo?!
 
Kwanini msijibu hoja za Gwajima kwanza?

1.) Hiyo chanjo si ya majaribio kwani? Anasema uongo?
2.) Kwanini mnaiita chanjo wakati haizuii maambuki, haikingi usiambukize wengine na haizuii kuumwa na kufariki kwa Corona? Why?

3.) Kama Mungu ametupa akili kama usemavyo, ni kwanini unataka tusizitumie wakati tunaona kabisa hatari iliyopo mbele yetu kwenye hizo chanjo za majaribio? Huoni kuzikataa ndio kutumia hizo akili?
Waweza kuta wew ndiye Gwajiboy mwenyewe, kila kitu unamuwaza Gwajiboy tu, au unasali kwake??
 
wagonjwa wa kisukari, ukimwi, saratani, moyo, presha na hata TB wanapuputika sana ktk wimbi hili la 3 la Corona/delta
Takwimu za vifo vya hao watu wenye hayo magonjwa ndio lingekuwa jambo zuri sana, kwa sababu tungeweza kujua ongezeko la vifo vya hao watu. Maana kuna issue nyengine ya kufa kutokana na covid na kufa ukiwa na covid.
 
Back
Top Bottom