Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
inna lillahi wa inna ilayhi rajiiun, mola ampuzishe kwa amani
Kada muhimu wa CUF Mara afariki
Na Mashaka Baltazar, Musoma
MWANASIASA machachari ambaye pia alikuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa tiketi ya CUF, Bw. Julius Masaka (49), amefariki dunia katika hospitali ya mkoa wa Mara, mjini hapa.
Taarifa iliyotolewa jana na mtoto wa marehemu, Bw. Frank Masaka, zilisema Bw. Masaka alifariki dunia juzi muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji katika chumba cha upasuaji cha hospitali hiyo.
"Baba alipelekwa katika chumba cha upasuaji akiwa anazungumza vizuri na hata jana (juzi) usiku tulizungumza vizuri na hatukuwa na matarajio kuwa angefariki dunia, baada ya kutoka huko alirudi akiwa amenyamaza na ndipo tukashituka kuona hazungumzi," alisema Frank huku akitokwa machozi.
Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini Bw. Masaka alitoa maelezo, kwamba alikunywa bia ambayo ilimpa utata katika baa moja mashuhuri ya mjini hapa (jina linahifadhiwa) na kabla ya hapo, alipigiwa simu aliyodai kuwa mpigaji alikuwa akimhitaji hapo, ili wapate kinywaji na kudai huenda iliwekwa sumu.
Ilidaiwa na Frank, kwamba mara baada ya baba yake kuinywa bia hiyo, alianza kusikia tumbo likimuuma na kuomba msaada wa kupelekwa kujisaidia.
Baada ya kutoka kujisaidia, alilala katika baa hiyo kabla ya mkewe kuitwa na kumpeleka hospitalini Oktoba 12 mwaka huu.
Aidha, habari kutoka familia ya marehemu Masaka, zilisema kabla ya mazishi mwili wa marehemu utafanyiwa uchunguzi wa kina, ili kubaini chanzo cha kifo chake. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Musoma, Bw. Valentino Bhangi, hakupatikana kuzungumzia kifo hicho.
Marehemu Masaka alizaliwa katika kata ya Bweri mjini hapa na kuhitimu elimu ya msingi shule ya msingi Azimio mwaka 1972, na kuanza siasa na kuwa Katibu wa CCM tawi la Nyasho, ambalo lilikuwa limeunganisha kata tatu za Bweri, Nyakato na Nyasho na baada ya hapo, alikwenda kusoma katika Chuo cha Siasa cha Murutunguru, Ukerewe, Mwanza.
Mwaka 1992 alijiunga na NCCR-Mageuzi, akiwa na wadhifa wa Katibu Kata wa kata ya Nyakato na mwaka 1993 alipandishwa cheo na kuwa Katibu wa NCCR-Mageuzi wa Wilaya ya Musoma Mjini wadhifa alioendelea nao hadi mwaka 1999 alipohamia TLP.
Aliteuliwa kuwa Katibu wa TLP wa Mkoa wa Mara tangu wakati huo hadi mwaka 2003 alipojiengua TLP na kujiunga na CUF na kuteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Tendaji ya Wilaya ya Musoma Mjini.
Marehemu Masaka aliteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2004 akiwa Msimamizi Mkuu katika kikao cha CUF kilichofanyika Julai 2004.
source majira