Tuwape nafasi viongozi wetu wafanye kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwape nafasi viongozi wetu wafanye kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 7, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kamati ya bunge ya miundombinu katika taarifa yake bungeni ililalamikia uteuzi wa kaimu mkurugenzi mkuu wa ATCL kuwa haukufuata vigezo, sheria na kanuni. Waziri Mwakyembe baada ya kuingia ofisini alipaswa kutekeleza maagizo na maelekezo ya kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu. Mojawapo likiwa hilo la kurekebisha kasoro ya uteuzi wa kaimu mkurugenzi wa ATCL.

  Watanzania tumekuwa tukilalamika juu ya utendaji usioridhisha wa watendaji wengi wa serikali wakiwemo mawaziri. Sasa inapotokea wanajitokeza mawaziri wachapakazi kama Mwakyembe na Magufuri ni vema tuwatie moyo na kuwaunga mkono na sikuwakatisha tamaa.

  Kwamba nani kateuliwa ni sifa na vigezo ndiyo vinaamua bila kujali jina, dini, rangi na kabila. Majungu yameanza kuwa Mwakyembe kamteua mnyakyusa mwenzake, swali la kujiuliza mteule ana sifa na vigezo vya kushika nafasi aliyoteuliwa kuishika? Captain Lusajo ni rubani mzoefu na wa muda mrefu hakuna mdau wa usafiri wa anga asiyemjua.

  Nini tafsiri ya ukabila hapo, kumteua mnyakyusa mwenye sifa au kutomteua mnyakyusa mwenye sifa kwa sababu ya unyakyusa wake?
   
Loading...