Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,398
- 39,547
Kwa vile suala hili la "tunguri" na "sayansi mamboleo" linaweza kuabisha bunge, kudhalilisha "waheshimiwa" na kulifanya Taifa letu lionekane miongoni mwa mataifa yanayoamini sana "nguvu za giza" nimeonelea kuwa sisi JF kwa vile mara nyingi tumekuwa wakosoaji na tunalaumiwa kuwa hatutoi mapendekezo ya kutatua matatizo "solutions" basi huu ndio wakati muafaka.
Hivyo ili tusiache Bunge letu lidharirike na jambo hili tulimalize kifamilia basi naomba kuwaalika kutoa mapendekezo ya nini "uchunguzi" useme ili jambo hili limalizwe "kiutuzima". Kwa maneno mengine naomba tuwarushie CCM, na Bunge kamba ya kutokea katika shimo walilolichimba wenyewe wakatumbukia; kwa maneno mengine tuwapatie "gia" ya kutokea kwenye tope walilolikwamisha gari lao wenyewe.
Hivyo tutoe mapendekezo Bunge na Uchunguzi useme nini ili turidhike. Mapendekezo hayo naomba yazingatie mambo makubwa yafuatayo.
a. Yawe ya kuaminika
b. Yaelezee kilichotokea (kwa sababu ushahidi wa tepu upo, hivyo kukana "haikutokea" haiwezekani.
c. Yamlinde Bwana Chenge na kumfanya aonekane "ameonewa, kusingiziwa, au kugeuzwa Bangusilo".
d. Yalinde heshima ya Bunge kuwa wabunge wetu hawaamini mambo ya kishirikina.
e. Wakielezwa wananchi lazima washangilie kuwa serikali hatimaye imemsafisha Chenge na Bunge.
f. Yahakikishe kuwa lolote litakalomkuta Bunge yeyote aliyehusika na mojawapo ya Kamati au kuvalia njuga "issue" fulani hapatwi na "shinikizo, ajali ya ajabu ajabu n.k) kabla ya uchaguzi ujao. Hili najua litakuwa gumu lakini sidhani kama kuna mtu yeyote atakayeelewa kilichotokea endapo yeyote kati yao atadhurika.
Mimi nitatoa mapendekezo yangu Jumatano. Naomba tuwasaidie Bunge, CCM n.k wapate "cha kutokea nacho" na wakwepe aibu. Tuache itikadi za chama na tuoneshe mshikamano, umoja na upendo wetu wa Kitaifa kwani wakiadhirika basi sote tumeadhirika. Tuwahifadhi CCM.