Tuwaorodheshe kwa majina wale wote wanaobeba CCM uchaguzi huu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuwaorodheshe kwa majina wale wote wanaobeba CCM uchaguzi huu...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ramos, Aug 23, 2010.

 1. R

  Ramos JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF najua mnalichukulia kwa uzito mkubwa suala la kutenda haki katika uchaguzi wa mwaka huu. Naamini kuwa kwa kiasi kikubwa utakuwa mchango mkubwa katika kuwezesha taifa letu kukombolewa mikononi mwa mafisadi.

  Naomba tuwaorodhesha wasimamizi, viongozi au hata askari wote watakaoonekana ama kwa maslahi yao, au kwa kumbeba mtu wanapindisha sheria za uchaguzi makusudi. Hii itasaidia kuwajulisha kuwa wananchi wamewafahamu, na kuwa wanastahili kulipa gharama kwa namna yeyote ile endapo matendo yao yatasababisha uvunjifu wa amani au watu kupokonywa haki zao...


  Kwa kuanza naomba mwenye jina la Msimamizi ambaye pia ni Mkurugenzi wa wilaya ya Handeni aliweke hapa. Huyu jamaa anaripotiwa na magazeti leo kuwa Anampendelea mgombea Abdalah Kigoda wa CCM, na pamoja na mambo mengine alimnyanyasa mgombea wa upinzani kwa kumuamuru atoke nje wakati wa urejeshaji wa form kumpisha Bw.Kigoda, ingawa mgombea huyo ndiye aliyewasili mwanzo na kuingia katika ofisi hiyo. Hili linaweza kuonekana kama tukio dogo, lakini mtu unaweza kupata picha ni nini kitatendeka baadae katika uchaguzi jimboni humo...

  Mwenye taarifa ya mwingine aliyeboronga aiweke hapa...
   
Loading...