Tuwaonee huruma waandishi wetu nchini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,289
12,582
Waandishi wa habari Ni mhimili muhimu sana katika utawala bora na uibuaji wa kero za watu na makundi mbalimbali, lakini Waandishi wetu huwa wamekumbwa na kadhia ya kushindwa kuripoti kile wanachotaka kuripoti na kile wanachopaswa kuripoti kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kukosa weledi, woga, kuvizia kuteuliwa, nk.

Msiache kuwaombea watanzania wenzetu hawa kila mnapopata fursa ya kufanya hivyo.
 
Acha waisome namba!

Walisema hawataandika kihusu bashite lkn wakaanza kuandika bila kutujuza.

Tunaiombea JF na member wake tu. Wengine gongweni tyu!
Nikiwafananisha na waandishi wa kainchi kadogo Al-jazeera, Ulaya na Marekani nashindindwa kusoma magazeti, kusikiliza redio na kuangalia TV maana naona makapi ya taarifa mbalimbali. Hadi huruma
 
Mbali na sababu ulizotaja, uanahabari Tanzania ni kazi ngumu kutokana na Sheria zinazowazuia kuandika mawazo yao, bali matakwa ya dola. Haruhusiwi kuandika habari yoyote hasi bila idhini ya mhusika. Invesgative journalism Tanzania ni marufuku. Kifupi wamezibwa midomo, wamenyang'anywa kalamu.
 
Nyongeza ya hayo,unajuwa kuwa waandishi wa habari,huwa hawalipwi?
 
Mbali na sababu ulizotaja, uanahabari Tanzania ni kazi ngumu kutokana na Sheria zinazowazuia kuandika mawazo yao, bali matakwa ya dola. Haruhusiwi kuandika habari yoyote hasi bila idhini ya mhusika. Invesgative journalism Tanzania ni marufuku. Kifupi wamezibwa midomo, wamenyang'anywa kalamu.
Mtu anayetunga sheria anaanzia kwa kuzisoma tabia za wanaotungiwa hiyo sheria, je, wengi Wana elimu gani, je Wana umoja kiasi gani, je, Wana njaa kiasi gani, je, wako violent kiasi gani, je wanalipuka kiasi gani, na je watafanya Nini kabla ya kuitunga hiyo sheria.
 
Juzi walijazana Mwanza kuandika habari za MV. Magufuli sijui. Aibu sana hii
Ni sawa kuandika habari za mv maana pia Ni habari, lakini mwandishi wa habari anatakiwa kushabikia zaidi zile habari ambazo zina tija kwa taifa lote. Mfano, mtu wa Nanjilinji habari ya MV Mwanza ataiona sio habari kwake, hivyo haifai kukaa kwenye front page ya chombo Cha habari, sio cross cutting issue.
 
Yaani kuna gazeti moja hilo wiki nzima linaichambua hiyo meli.
Very shit!
Nahisi wameishiwa propaganda
 
Wadau msisahau njaa, pamoja na tasnia hii kukumbwa na janga la sheria kandamizi ila njaa inakuwa kali sana.

Ukimuona mwandishi please mpe tip asee, siyo lazima kuwepo na story, kingine hawa jamaa zangu msiwatenge kwenye interviews zenu au conference report unapofika muda wa kusign😁!.
 
Mtu anayetunga sheria anaanzia kwa kuzisoma tabia za wanaotungiwa hiyo sheria, je, wengi Wana elimu gani, je Wana umoja kiasi gani, je, Wana njaa kiasi gani, je, wako violent kiasi gani, je wanalipuka kiasi gani, na je watafanya Nini kabla ya kuitunga hiyo sheria.
Umemaliza kila kitu. Ukiona mtu kakudharau jua we mwenyewe ndio uliompa huo mwanya
 
Nimeondoka na somo..japo wengi mnatutukana lakin hamjui ugumu wa kazi yetu...

Ukitaka kujua kazi yetu tunaijua hebu angalia makala tunazoandoka za kuisifia nchi au kumsifia jamba moja...
Hayo mengine ni sawa tu na kazi za polis na mahakama..msimu kaz zote hazifanywi kwa weledi..
Binafs nimeacha kuandika wala kwenda kwenye mikutano ya upinzan..pamoja na yote mi ni binadam mwenye mahitaj yangu..

Kajitoa muhanga azory sembuse mie? Tuachen
 
Yaani kuna gazeti moja hilo wiki nzima linaichambua hiyo meli.
Very shit!
Nahisi wameishiwa propaganda
Mtu wa Korogwe hiyo meli sio habari kwake usijisumbue kuiandika, haiwezi kumbadilisha chochote, yeye anataka kusikia mabomba ya maji yatatandazwa lini mtaani kwake.
 
Wadau msisahau njaa, pamoja na tasnia hii kukumbwa na janga la sheria kandamizi ila njaa inakuwa kali sana.

Ukimuona mwandishi please mpe tip asee, siyo lazima kuwepo na story, kingine hawa jamaa zangu msiwatenge kwenye interviews zenu au conference report unapofika muda wa kusign😁!.
Mwandishi wa habari anaekaa mkao wa kuteuliwateuliwa kwenye siasa hawezi kufanya kazi za mhimili wa nne (4) wa dola. Mwandishi habari wa Kenya Ni zaidi Sana ya mwandishi wetu.

Pascal Mayalla na kipindi chache Cha kiti Moto ndio aina ya waandishi wa habari wenye viwango vya kimataifa, sijui nae alibanwa wapi.
 
Mambo ya hovyo sana. Kila mtu anasaka kuteuliwa. Nchi hii naishi kwakuwa tu wazazi wangu walizaliwa Bongo

Back
Top Bottom