Suphian Juma
Senior Member
- Apr 2, 2019
- 133
- 546
NIMEPOKEA UJUMBE WA WANAFUNZI WATANZANIA CHINA, SERIKALI IWATAFAKARI UPYA KABLA HATUJAWAPOTEZA WOTE 400!
Na: Suphian Juma
Pamoja na kwamba Serikali ya Tanzania, kupitia Waziri Mkuu, Majaliwa leo Januari 30, 2020 Bungeni kutoa wito kwamba wanafunzi wanaosoma China walio likizoni kutorudi China kutokana na tafrani ya virusi vya Corona, mimi Suphian Juma nimetaarifiwa na Wanafunzi Watanzania kadhaa kuhusu hali tete wanaoyopitia huko mjini Wuhan.
Kwa kauli ya Waziri Mkuu, Majaliwa nadhani Serikali ya Magufuli imejikita zaidi kuwaokoa wanafunzi walio likizo na imeweka umakini kiasi kwa wanafunzi na Watanzania waishio China hususan katika mji wa Wuhan, na kutoweka umakini wa kutosha kwa Watanzania kiasi cha wao kuhisi kutengwa, na kuona uhai wao kuwa hatarini zaidi ukizingatia huduma za muhimu nako hawazipati ipasavyo kwa mujibu wa ujumbe walionitumia.
Aidha wanasema si kweli China haiwapi ruhusa ya kutoka mjini Wuhan kurudi Tanzania, China wameukubalia Ubalozi wa Tanzania China na Balozi za nchi zingine, kufanya mpango waondoke ila ubalozi wetu umekuwa mzito kuwaruhusu licha ya wao kuwa tayari kujigharamia nauli ya kurudi nyumbani ilmradi waokoe maisha yao.
Kiufupi wanasema wamebaki wanaishi ndani mithili ya wafungwa, wakisongwa na mawazo, wakikosa uhuru wa kutoka nje ya vyuo na makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa na virusi hivo hatari vinavyouua kwa muda mchache tu wakikushambulia.
Ufuatao ni ujumbe wa moja ya wanafunzi walionitumia.
Hello kaka Suphian hope mko poa, katika kuwapigania Watanzania.
Nakutaarifu juu ya hali ya Watanzania zaidi ya 400 waishio ndani ya mji wa Wuhan, mji ambao virus vya korona vilianzia.
Hali inatisha na huduma za msingi zinazidi kuzolota, nchi zinazojitambua zinazidi kuwaondoa raia wake huku serikali yetu ikiendelea kuleta siasa tu bila kuchukua hatua.
Siku mbili zilizopita Serikali yetu ilitoa press release kupitia ubalozi wake hapa China kuwa serikali ya China imegoma kutoa ruhusa kwa watu wa Wuhan kuondoka na kama wakitaka kutoka watawekwa kwenye quarantine kwa siku 14 ndo waruhusiwe kuondoka.
Jambo hilo ni uongo kama uongo mwingine wautoao, nchi zingine wakisha-organize usafiri wanatoa taarifa Serikalini ndege yao inaruhusiwa kutua Wuhan watu wanapanda nchi ndo inajua pa kwenda kuwachunguzia, I mean nchi yaweza kututoa huku ikatuweka hata pori la Burigi kwa siku 14 then tukaruhusiwa kwenda makwetu.
Huku vyuoni wanaendelea ku pressurize wanafunzi waombe Balozi zao ziwaondoe eneo la hatari wao wanaendelea kusisitiza Serikali ya China ndo kikwazo.

Mwisho wa nukuu.
Binafsi kama Mtanzania ninayejua thamani ya uhai wa kila Mtanzania, na wajibu wangu na haki yangu ya Kikatiba ya kuwasemea na kulinda uhai na UTU wa Watanzania wenzetu popote waliopo, NAITAKA Serikali ya Tanzania chini ya Rais Magufuli IWATAFAKARI UPYA Watanzania wenzetu hawa, ichukue hatua za dharura ikiwemo kuwahamisha Watanzania hawa kutoka kutoka mji athirika na Corona na kuwapeleka pahali salama.
Tiba ni bora zaidi ya Kinga, tusisubiri wafe, tuanze kusema ni mipango ya Mungu wakati ni uzembe wetu.
NB: Nimeambatanisha na email na nakala za barua walizonitumia wanafunzi walizotumiwa kutoka moja ya Chuo wanachosoma China na pia barua kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Suphian Juma,
Afisa Habari, ACT Wazalendo, Tanzania.
Januari 30, 2020.
Sent using Jamii Forums mobile app