‘Tuwanyonge viongozi wa umma’

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
MIAKA miwili iliyopita, serikali ilikuwa na programu ya kupambana na majambazi. Baadaye ikadhihirika kwamba baadhi ya majambazi wakuu ndio walikuwa wafadhili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Baadhi yao wakaanza kuvujisha hata taarifa za michango yao kwa CCM wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Bila shaka hii ilikuwa njama yao ya kujitetea wasiguswe. Na kweli, hawakuguswa.

Tumeishia kuona askari wetu wakihatarisha maisha yao kwenye misako ya majambazi kwa kutumia pikipiki, hasa jijini Dar es Salaam! Wanakimbizana na wakwapuzi, wezi wakubwa wanatesa!

Tangu majambazi hao walipotamba kuiumbua CCM kwa kutaja viwango vya michango yao, na kina nani walipokea – wengine wana vivuli na vishina vya hundi za benki – serikali ilinywea.

Haraka haraka, yakatokea mambo mawili. Kwanza, Rais Jakaya Kikwete akatamka hadharani kwamba ‘sasa umefika, ni vema chama kitafute njia mbadala za kupata pesa safi kwa ajili ya uchaguzi.’

Hili lilikuwa ungamo la wazi – labda bila kujua – kwamba CCM imekuwa inaneemeka kwa pesa chafu. Na kwa kuwa tulikuwa tumetoka tu kwenye uchaguzi uliompa yeye ushindi, bila shaka alikuwa anazungumzia pesa chafu iliyoongeza nguvu katika ushindi wake wa kishindo.

Kwa wengine, alikuwa anazungumzia kilichokuwa kinajadiliwa mitaani juu ya majambazi mashuhuri waliokuwa mstari wa mbele kuchangia CCM na kuhamasisha ushindi wake, huku baadhi yao pia wakishiriki kampeni zake moja kwa moja.

Wengi tulisubiri kuona kama rais mpya ana ubavu wa kuwagusa majambazi wazito au naye atakimbizana na vibaka na wakwapuzi wa ‘vijisenti’ vinavyoporwa benki.

Pili, Rais Kikwete alitoa kauli kwamba anawafahamu majambazi na wala rushwa; na kwamba anawapa muda wajirekebishe. Mwenendo wa mambo sasa unaonyesha kwamba wezi hawa waliopewa ruksa ya muda usiofahamika, wameitumia vizuri.

Wametumia muda huo kuiba kwa kasi mpya (maana hawajui muda waliopewa utaisha lini); na wametumia muda huo huo kujijenga na kuizidi nguvu serikali. Wameimarisha mtandao kitaifa na kimataifa.

Na kwa kuwa sasa ni mwaka wa tatu tangu walipopewa ruksa kumalizia hata hicho kilichokuwapo, si makosa kusema kwamba nusu ya utawala wa serikali ya awamu ya nne imetumika kuwaneemesha wezi.

Ndiyo maana wapo watu wanaodiriki kuuita utawala wa sasa kuwa ni wa wezi. Yawezekana wanawatuhumu baadhi ya walio madarakani au wasaidizi wao au maswahiba wao. Lakini ujumbe wa kijumla ni kwamba sifa kuu ya awamu ya nne ni ufisadi.

Hii ndiyo ‘legasi’ (au urithi) ambayo Rais Kikwete ameijenga – makusudi au kwa uzembe na woga tu – katika miaka miwili na ushee aliyokaa madarakani.

Imekomazwa na kauli zake hizo mbili nilizotaja hapo juu, lakini zaidi hiyo ya pili, na uzito wa rais kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi serikalini mwake.

Tukizipima katika mizani ya kiakili, kauli hii ya pili ina kasoro kubwa. Ile ya kwanza inaonyesha nia ya rais kujiondoa katika madaraka yaliyojengwa kwenye nguvu ya ujambazi.

Hii ya pili inaibua maswali leo kama ilivyokuwa wakati anaitamka mwaka 2006. Rais aliwajuaje majambazi? Aliwajua lini? Ni wa mbali au ni watu wake wa karibu? Aliletewa taarifa za kishushushu? Au alitoa kauli kisiasa kuwatisha tu? Je, kauli kama hiyo ina madhara gani iwapo hatimaye majambazi hao wataonekana washindi?

Na je, kama yeye amefikia mahali pa kuwajua, polisi hawana habari nao? Wamewafanyaje? Taasisi ya kupambana na rushwa na vyombo vingine vya dola havina taarifa hizo? Au haviwezi kuwachukulia hatua hadi viruhusiwe na rais?

Na hii tabia ya viongozi kuwapa majambazi muda wa kujirekebisha imeanza lini? Je, vibaka na wezi wa mifukoni watapewa fursa hiyo? Je, katika muda huo jamii itakuwa salama? Au hii ndiyo kasi mpya tuliyoambiwa? Kauli hii haiibui udhaifu wa kiuongozi? Haiibui uswahiba na majambazi?

Tuliulizana sana wakati huo, na sasa bado tunaulizana maswali mengi, hasa baada ya fukuto la ufisadi unaoihusisha serikali yenyewe, wakubwa na watu wao wa karibu.

Miaka miwili baada ya kauli ya rais, watawala wanadhani tumesahau. Majambazi wanaendelea kutesa. Au bado wanafaidi kipindi walichopewa na rais?

Lililo wazi ni kwamba miaka mitatu haikutumiwa na majambazi tu. Hata sisi Watanzania tumeitumia kuwagundua na kuwatambua majambazi halisi. Tumejua ukweli zaidi.

Ujuzi huu umeongeza hata ujasiri wa wananchi kusema bila woga kwamba wengi wa majambazi wakubwa wamo serikalini. Wamo na wastaafu. Wengine ni washauri wa kutegemewa na watawala.

Kwa sababu hiyo, sasa – baada ya miaka miwili - tunapata tafsiri halisi ya kauli hiyo ya pili ya rais, kwani pole pole, hatusikii lolote kuhusu kasi mpya, bali kauli na matendo yanayoonyesha kwamba huruma yake kwao imezidi hasira zake za awali.

Mkubwa amekwama, na nchi nzima inakwama naye. Ndicho kilio cha Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya, anapoifananisha Tanzania na mdudu aitwaye Tengaruzi, ambaye “ana tabia ya kuzunguka kwa kasi kubwa ndani ya maji yasiyotembea kwa kasi, lakini hawezi kwenda mbele.” Anaongeza: “Nasikitika, ni aibu kila mtu analia, wananchi wananung'unika na serikali inanung'unika, hakuna njia mbele.”

Kitu kimoja ambacho mzee Mzindakaya amesahau ni kwamba njia ipo, tena si moja tu. Zipo nyingi. Tatizo ni kwamba wanaopaswa kutuonyesha njia hizo, wamepoteza uwezo wa kuona.

Kwa hiyo, kama tunakubaliana na falsafa ya mambo manne muhimu ambayo Mwalimu Julius Nyerere alisema tunahitaji ili tuendelee – ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora – kikubwa tunachokikosa hapa ni uongozi bora.

Wanazuoni wataendelea kubishana kama tuna siasa safi. Wananchi wa kawaida watakubaliana haraka kwamba siasa safi zinazohitajika katika zama hizi tunazo - ni siasa za ushindani katika mfumo wa vyama vingi.

Lakini zinaongozwa na wazoefu wa mfumo mkongwe wa chama kimoja, wasiotaka kujifunza na kubadilika! Kibaya zaidi, kundi kubwa la wakongwe hawa limezama katika kujilimbikizia mali kwa kasi ya kutisha. Hawana muda wa kuwaza upya visheni ya taifa.

Wanafanya siasa za uchumaji, ambazo zimewajengea hulka ya kujiamini katika makosa na kudharau wananchi. Ndizo hizo zimewafanya wawe washirika wa ujambazi na wizi wa rasilimali za umma, na kuwahujumu walipa kodi wa Tanzania.

Kila mara yanapozuka masuala ya ufisadi, naitazama ile orodha ya mafisadi waliotajwa na Dk. Willibrod Slaa, katika viwanja vya Mwembe Yanga, Dar es Salaam, Septemba 15, 2007. Narejea pia kauli kongwe ya Aristole, mmoja wa wanafalsafa wa awali katika Ugiriki, aliyeishi miaka 384-322 Kabla ya Kristo.

Aliwahi kusema: “Ukitaka kujua sisi ni akina nani, tazama yale tunayotenda kila mara.” Taratibu nawaona viongozi walioamua kujigeuza majambazi’ dhidi ya umma.

Tunarudi pale pale nilipowahi kuandika huko nyuma nikimnukuu mtumwa mmoja wa Kigiriki, Aesop, aliyeishi kati ya miaka 620 na 560 Kabla ya Kristo, kwamba: “Tunawanyonga vibaka na kuwachagua wezi wakubwa kuwa viongozi wa umma.”

Na baadhi ya wasomaji wa safu hii wamekuwa wakinihoji: “Sasa tufanye nini?” Labda kwa sasa ningeweza kuwapa ushauri wa dharura: Tuwaache vibaka, tuwanyonge viongozi wa umma. Tukutane Jumapili ijayo.

+447847922762
ansbertn@yahoo.com
 
Politician: One who shakes your hand before elections and your Confidence after?
 
Mfano wa wazi ni bwana MUTEMBEI anayemiliki shule za ST.Mathews alikuwa akikodisha silaha kwa majambazi na akafukuzwa kazi polisi kituo cha Ilala.

hivi sasa ni mweka hazina wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani na ndiye mlezi wa Umoja wa vijana wilaya ya Mkuranga. mwaka 2005 jina lake lilifutwa kutokana na tuhuma na ujambazi ambazo hazijafutika hadi leo hii.cha ajabu mwaka jana kapewa uweka hazina wa Chama huku anatuhuma nzito za ujambazi.CCM imekuwa chaka la majambazi kama hawa kina MUTEMBEI.
Said Mwema kamata majambazi kama haya.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom