bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,321
- 4,671
Siku za karibuni kumekua kukiibuka wimbi la wasanii kujiingiza kwenye Matumizi ya madawa ya kulevya na mwisho wake either ni Kifo or kufilisika kabisa.
Hakuna budi hawa Wasanii watafutiwe washauri wazuri pindi wanapoanza kushika pesa nyingi kwa mkupuo baadhi yao wanakua hawana nidhamu na matumizi ya pesa wanazozipata kwani huja ghafla.
Wengi hawafikirii kuwekeza kwenye vitega uchumi ila kesho na keshokutwa music wake ukichuja awe na chanzo kingine cha mapato wanatumia chote wanachopata kwa Anasa mbalimbali bila kuangalia kesho yake.
Matokeo yake ndo pale Musiki wake unapoexpire na pesa zake kwisha wanajikuta kwenye Msongo wa Mawazo uliopitiliza na kuanza kujiingiza kwenye Ulevi kama njia ya kutibu Msongo wa Mawazo kumbe ndo wanajimaliza na polepole huanza na Ulevi kama Unywaji uliopitiza wa Pombe,na baadaye kujiingiza kwenye Matumizi ya madawa haramu yaliyopigwa marufuku duniani kote bila kujua madhara yake kwenye Moyo,Mapafu,Ubongo,na pia pua.
La Msingi ni Wasanii kutafuta washauri wazuri watakaowashauri kuhusu Maisha yao ya badaye na umuhimu wa kuweka Akiba na pia kuwekeza kwenye Mambo mengine zaidi ya musiki pindi wapatapo pesa ili kuepuka mambo kama msongo wa Mawazo ambaye baadaye hujipata wakijiingiza kwenye matumizi ya madawa haramu ambapo mwisho wake huwa ni mbaya sana.