moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 135,666
- 728,072
Wanajamvi, mchezo wa soka unahusisha timu tatu uwanjani.ukiacha zile mbili zinazochuana pia kuna timu ya waamuzi. timu hii ni sehemu muhimu ya burudani ya mchezo huo. hivyo tukumbuke majina yaliyotamba kwenye kupuliza filimbi na kunyoosha vibendera na matukio ya kusikitisha na kusisimua yaliyofanywa na waamuzi wetu wa soka.nitawaletea orodha ya waamuzi nanyi mtajazia pamoja na matukio ambayo waliyafanya na pengine lilikuburudisha ama kuhuzunisha. Mimi nitaelezea tukio ambalo limetokea kati ya mwaka 1985 au 1986 (sikumbuki vizuri). Uwanja wa taifa sasa Uhuru, watani wa jadi waliumana. Kariakoo derby, simba na yanga. kwenye mchezo huo refarii alikua ni Abdulrasul Ismael toka morogoro. beki wa yanga salum kabunda baada ya kupata usumbufu mwingi toka kwa mshambuliaji machachali Edward chumila, akamrukia miguu yote kifuani. Chumila alipoteza fahamu kwa muda na akakimbizwa hospitali. Cha kushangaza wakati kila mmoja akijua kuna red card ya moja kwa moja, lakini haikuwa hivyo mwamuzi alitoa kadi ya njano kwa kabunda ambaye tangu siku hiyo akaitwa "ninja". mashabiki wa simba walihamaki na kuzomea. mchezo ulipoisha mwamuzi huyo ambaye sasa ni marehemu alipata ulinzi mkali asidhuruwe na wapenzi hao. baadaye mwaka 1995 na 1996 refarii huyo aligombea nafasi ya mweka hazina wa simba. Mara zote mbili Abdulrasul aligonga mwamba. Kila alipogombea aliulizwa swali moja tu. "Ulitumia sheria gani kutoa kadi ya njano kwa faulo aliyochezewa chumila na kabunda"? Hakuwa na majibu. refarii huyo hakubahatika kupata uongozi simba mpaka mauti yalipomfika. Tuwakumbuke ;- Nyama, Manyoto Ndimbo, Meja Gwaza Mapunda, Msafiri Mkelemi, David Lugenge, Danstan Daffa, David Okoth, Mussa Lyaunga, Abdulrasul Ismael, John Mwambembe, Abdallah Malipula, Abdul Kawambwa, Bakari Bendera, Mustafa Nyakiraira, Taji Bakari, Bakari Mtangi, Nassoro Hamduni, Hafidhi Ali, Omar Abdulkadir. Jazia tuwakumbuke