Hawa viongozi waliopo CCM ndio waliokuwa na chama tangu enzi za TANU na kuundwa kwa CCM 1977 na wametawala taifa mpaka leo hii. Inamaana CCM wanajua kama kuna watu waliodhulumi au kunyanyaswa na wanawajibu wa kujibu hilo kwani hakuna watu wengine waliowahi kutawala TZ zaidi yao. Huwezi kutoa malalamiko ambayo hujui unayemlalamikia ni nani, kama ni serikali basi waliotawala miaka ya nyuma na wanaotawala sasa wapo waulizwe wajibu hoja na siyo watu wanalalamikia rai wenzao huko wakiogopa kuigusa serikali ambayo ndio mhusika mkuu. Bahati nzuri raisi anayetawala alikuwa kiongozi ndani ya CCM tangu miaka ya sabini hivyo kama kunadhuluma anazijua then aziweke wazi kwa mamlaka aliyonayo ili kila raia ajue na aliye dhulumiwa apewe haki yake. Sioni sababu ya kulalamika huku unaogopa kupambana na aliyekudhulumu kama serikali ipo , CCM ipo na sehemu ya waliotawala tangu uhuru wapo waulizeni hao na siyo kuwasumbua raia wasiojua hata mnacholalamikia ni nini. Kulalamikia raia wa kawaida kuhusu dhuluma ya watawala haiwezi kusaidi chochote wewe pambana na watawala waliokudhulumu kama unogopa kupambana nao kwa sababu ni wenzako basi ni bora ukae kimya.
Vumbi,
Naomba nikuulize mwaka 1995 kwenda chini ni nani aliyekuwa madarakani? CCM ilikuwa inatambulika kama Chama gani? Chama kama chama hakiwezi kuwa na tatizo kwasababu ndani ya chama wapo watu wabovu na wazuri. Hivyo kulaumu chama ukaacha washirika wakuu ni kama vile unalaumu nyumba wakati mjenzi ndie anayekaa humo ndani. CCM walikuwapo wazuri na watu wabaya hivyo basi wa kulaumiwa ni wahusika wakianza na baba yetu wa Taifa.